Thursday, March 8, 2012

DR MWINYE HAJI MAKAME AULIZWA SWALI LAKITOTO AJIBU UTUMBO NA KUSIMAMISHA UMAPINDUZI USIO NA MSINGI KWELI DR SHEIN ZANZIBAR NDIO ITAENDELEA.....?

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara ya Fedha na Uchumi ambapo alionesha ubaguzi wa waziwazi kwa waandishi wa habari wa BBC, Ally Saleh na Salma Said wa DW waliokaa viti vya mbele wakati akijibu masuala ya waandishi hao aliyoulizwa katika mkutano huo,

Wachaa niazie hapa tokea mabadiliko makubwa ya kisiasa ya 1964 kufuatia Mapinduzi nimekuwa
nikisema mara nyingi Zanzibar kama nchi ilishindwa kuandaa mikakaati ambayo
ingesaidia kuondosha tatizo la chuki za kisiasa zilizojengeka kabla ya
Mapinduzi hayo.
Chuki za Zanzibar Nationalist Party ZNP, Zanzibar and Pemba Peoples Party
ZPPP kwa upande mmoja na upande mwengine ikiwa ni chama cha ASP, nja ambazo
zilifikia kilele pale vyama hivyo vilipouungana na kuchanganya kura zao na
kwa hivyo kuchukua Serikali ya kwanza ya Uhuru hapo 1963.ikiwa zanzibar ni nchi huru kabisa.
Ubaya ni kuwa chuki hizo zimeachwa zikuwe na zimee, pengine wengine
wamekuwa wakifaidika nazo na ndipo maana mpaka leo tuna serekali ya (SUK)LAKINI BADO MIJITU KAMA HII DR MWINYI HAJI MAKAME inataka kuirudisha chuki na hasama ili wao wale wananchi wateseke na pia zikajitokeza zaidi wakati siasa za vyama vingi 1992 ziliporudi na kuzagaa kwa hatari sana hata katika kizazi kipya ambacho hakikuwa kikijua ZNP, ZPPP wala Afro Shirazi zaidi ya ngano
walizokuwa wakisikia.Chuki hizo zilipelekea maovu mengi kutokea katika jamii na familia abayo hata hayasimuliki kabisa ni aibu haswa kwa kikwetu hapa zanzibar lakini yametokea. Mizizi yake iliingia katika uendeshaji wa Serikali ambapo mtu yoyote ambaye angedhaniwa asie wa chama kilicho madaraka imemuia vigumu kupata ajira au kupata cheo.Baada ya muda mrefu na jamii na nchi kutanabahi kuwa tumekuwa tukienda kusiko na hilo si jambo la tija kwetu, viongozi wawili wakuu wa vyama kinzani, Dk Amani Karume na Maalim Seif Shariff ambavyo kwa sababu zisizo za msingi vilikuwa vikiendelea kuhusisha na siasa za kabla Mapinduzi vilipoamua kuwa imechosha na imetosha.Wakasema chuki na ubaguzi iwe basi. Wakasema ni hatari kwa maslahi na mustakbali wa nchi ambapo athari yake ilionekana pia katika kila msimu wa
uchaguzi kwa kukosekana mshindi aliyepata imani ya nchi na kwa hivyo kuwa vigumu kushika hatamu za uongozi.Wakachoka kuonekana kila siku kuna magomvi katika nchi na kuona nchi inaendelea kugawika nusu kwa nusu na kuwa wanaofaidi fursa za nchi ni upande mmoja tu wa siasa na mwengine ukiula huu,chembilecho msemo maarufu wa Mombasa hapo zamani.Lakini wiki tatu nyuma nilibahatika kuwasilisha makala katika semina ya REDET ambapo nilitakiwa nitizame suala la ushirikishi tokea kuundwa kwa Serikaliya Umoja wa Kitaifa (SUK) , ambayo moja ya jukumu lake lilikuwa au
lingekuwa kujaribu kumaliza suala la ubaguzi ndani ya jamii kutokana na siasa.Ilikuwa ni fikra yangu kuwa hapana juhudi maalum iliyochokuliwa kuhakikisha chuki kama hizo zinazikwa na ndio maana hakuna kikubwa kilichobadilika kwa sababu ushiriki wa kujenga nchi bado una masharti na unalalia upande mmoja
na hilo linaiweka SUK njia panda.Katika mkutano huo ilitokana kauli ambayo mpaka leo inanitetemesha pale
nilipotoa hoja ya kukata mizizi ya ubaguzi kwa kuondosha kipingamizi cha Wazanzibari wasio na asili ya Kiafrika kuweza kujiunga na vikosi vya ulinzi kama watapenda, lakini kauliya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Mustafa Muhammd kusema, “ Haiwezekani kwa bunduki na risasi kupewa kwa mpinzani.”Ilibidi nifungue darasa kuelezea tofauti ya mpinzani na raia. Kwamba raia wote katika nchi wanatakiwa wawe na haki sawa bila ya kujali asili zao, na nikatoa mfano wa Marekani ambapo hata raia wenye asili Iran wana haki
kamili ya kuingia jeshini.Kumbe kauli ya kiongozi huyo bado inaashiria kuwa hali haijabadilika ndani
ya jamii na kuwa bado chuki za kisiasa zipo na mara hii zikijitokeza kupitia kiongozi ambaye ni Waziri tena katika Ofisi ya Rais, Dk. Mwinyihaji Makame.Katika sehemu kubwa mno ya maisha yangu nimekuwa nikibaguliwa hapa Zanzibar. Nimefukuzwa kazi, nimezuiliwa kuingia sehemu kadhaa, nimetishiwa
maisha hadharani hata mbele ya Rais Mkapa, nimebandikwa majina mengi,lakini hili alilonifanyia Waziri Dk Mwinyihaji nimeshindwa kulistahamilia kwa sababu nilikuwa najaribu kujenga imani kwamba ubaguzi unaondoka, ingawa najua bado upo.Nilisikitishwa kauli ya ubaguzi kutoka kwa Waziri ambaye ni msaidizi muhimu wa Rais na bila kisisi, aibu wala majuto yoyote akatoa kauli kama jambo la kawaida tu, kitendo ambacho kimedhihirisha labda pengine yeye si muumini mzuri wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo msingi wake mmoja ni kuondosha ubaguzi wa kisiasa.Tulikuwa katika mkutano wa waandishi wa habari ambapo Dk. Mwinyihaji alikuwa akikaimu nafasi ya Waziri wa Fedha na kuitishwa kueleza hali ya
nishati ndani ya nchi ambapo kulikuwa na uhaba mkubwa wa petroli.Nilimbana Waziri katika hoja mbili. Kwanza kitendo cha Serikali kukaa wiki mbili bila taarifa ya si uhaba bali ukosefu wa nishati hiyo na nikasema hilo haliwezi kukubalika. Pili nilijaribu kujenga hoja kuwa uchumi wa nchi ulisimama nikimtaka Waziri atoe takwimu Serikali imekosa mapato kiasi gani na uchumi umeathirika kiasi gani nikitaka takwimu.
Kwa kiasi kikubwa mkutano huo ulikuwa mkali na mimi na mwandishi Salma Said tukawa hatumpi Waziri nafasi ya kuvuta pumzi, na kwa kiasi aliona huo ni utovu wa nidhamu kwa kuwa pengine amezoea mikutano ya waandishi wa habari ambapo anasema mpaka anakwisha bila ya kukatishwa au kutupiwa suala la
kumkinza. Katika hili nafikiri anapaswa kupata mafunzo upya.Basi Waziri hakuweza kuchukua na usthamilivu ukamshinda na hapo akajivua gamba na kujionyesha rangi zake halisi, Ah…utanambia nini bwana…nyie
kama baba mmoja mama mmoja mna yenu mengine twambieni….sio haya bwana. Sote((anaposema sisi sote wazanzibar kuna mtu kamuliza kama wewe sio mzanzibar au anajishuku)) Wazanzibari bwana msitudanganye bwana…Wewe Buto (albarto yaani ally saleh) nakufahamu toka uko wapi mpaka leo…na huyu (mwandishi salma said)nakufahamu toka zamani mpaka leo”Sote Wazanzibari bwana msitudanganye. Wewe
Albarto nakufahamu toka uko wapi huko mpaka leo…na wewe Salma nakujua
uzuri…”Kwa hakika nilimuonea huruma sana Waziri Dk. Mwinyihaji kwa kuwa mpaka leo
ana fikra kuwatizama watu kwa kuamini anawatia kwenye dema la kisiasa.badala ya kujibu swali alilo ulizwa. Kwa wageni wa siasa za Zanzibar alichokusudia kusema Dk Mwinyihaji kuwa anatua
kwamba mimi na mwenzangu anatuhusisha na chama cha CUF na kwa hivyo ni wapinzani hata sasa ambapo CUF imo ndani ya Serikali.je upinzani ni haramu au ndio moja ya njia ya kujenga nchi...?Upande mwengine niliumia kuona kuwa bado kunaweza kuwa na mawazo kama hayo miongoni mwa watu ambao Dk. Ali Muhammed Shein amewapa vyeo vya uwaziri na unajiuliza kwa mtizamo huu nchi inakwenda wapi na kweli ubaguzi nchi hii utaondoka....???????????

No comments:

Post a Comment