Tuesday, April 3, 2012

BADALA YA KUJENGA HOSPITALI,VYUO VIKUU,VIWANDA,NYUMBA KWA JILI YA WANANCHI

SERIKALI YA ZANZIBAR KUJENGA  GEREZA JIPYA                                               NA KHATIB SULEIMAN – UNGUJA

KATIKA kuhakikisha inapunguza msongamano kwa wafungwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inakusudia kujenga gereza jipya la kisasa lenye uwezo wa kuchukua wafungwa wengi kwa wakati mmoja na kuondosha msongamano uliopo magerezani.
Hatua hizo zinakwenda sambamba na mikakati ya kuimarisha dhana ya utawala bora na haki za binaadamu ambayo inasisitiza suala la kuimarisha mazingira bora ya wafungwa katika magereza.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakar Khamis Bakari wakati akijibu swali aliloulizwa na mwakilishi wa Jimbo la Muyuni, Jaku Hashim Ayoub (CCM) aliyetaka kujua mikakati ya Serikali ya Mapinduzi ya kuondoa msongamano wa wafungwa katika magereza yake.
Abubakar alifafanua na kusema kwamba tayari Serikali imeanza kazi ya kutafuta kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa gereza hilo huko Hanyegwa Mchana, wilaya ya kati mkoa wa kusini Unguja.
Alisema ujenzi wagereza hilo utakapo kamilika litakuwa na nafasi kubwa ya kuchukuwa watuhumiwa na wafungwa wengi kwa wakati mmoja na kuondoa tatizo la msongamano lililopo katika magereza ya Unguja na Pemba.
“Nakubaliana na mheshimiwa kuhusu suala la kuwepo kwa msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza yetu ya Unguja na Pemba…mipango ya kujenga gereza jipya kwa sasa imekamilika na tunatarajia kupata fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi,” alisema Abubakar.
Hivi karibuni Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, alifanya ziara katika Magereza mbali mbali ya Unguja na kukagua sehemu ya kiwanja cha gereza jipya huko Hanyengwa Mchana wilaya ya kati Unguja.
Makungu alisema kumalizika kwa ujenzi wa gereza hilo jipya litaondosha moja kwa moja msongamano wa wafungwa na mahabusu lililopo sasa huku akitaka kuwepo kwa kuharakisha kusikilizwa kwa kesi za watuhumiwa mbalimbali.
MUNAJENGA MAGEREZA MAPYA ILI MUMFUNGE NANI..?MAANA MAMBO MUHIMU YA KUIJENGEA JAMII NA RAI WA ZANZIBAR HAMUFANYI HAO MUSHAKURUPUGA KUJENGA GEREZA JIPY AMAKWELI NYINYI SIO SEREKALI YA KUITEGEMEA BALI NI MAKABURU WAKUBWA NYIE

Mtoto huyu anahitaji huruma, imani, na mapenzi ya uangalizi wa maradhi yake. Fikiria ikiwa Dr Husika inapofika saa 2.30 hajafika ofisi khatma yake itakuwaje?
Hapa mlango wa kuingia kitengo cha macho umefungwa huku wagonjwa wakiwasilisha mafile yao kwenye kibaraza cha jengo
Wagonjwa wengi wakisubiri kuingia katika eneo la kitengo cha macho. Hapa inaonekana bado mlango umefungwa na wao wakiwa wamesambaratika hata pa kukaa hakuna jiuliza mzanzibar
Sehemu ya mapokezi kitengo cha wagonjwa wa mifupi Mnazimmoja Hospital hata huyo mpokeaji hayupo na haya mabuku ati ndio kadi za wagonjwa je kweli mzanzibar unataka kuishi maisha haya mpaka lini..?
Wagonjwa wamesambaratika katika floor ya Hospital ya Mnazimmoja wakisubiri kupata matibabu. Kwa mbali mfanyakazi wa hospitak akiingia na pikipiki yake.

No comments:

Post a Comment