Tuesday, April 17, 2012

CCM YASEMA TUTAPAMBANA NA UAMSHO AMAKWELI BUNJU NI BUNJU TU HATA ILIWASHEYE TAA HALIONI NDIO HAWA CCM

 KASHINDWA FERAUNI MUTAWEZA NYINYI VISONOKO
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mkutano uliofanyika Magogoni kwa Mabata Mjini Unguja
Uamsho tunawagusa ka sababu kama wametumwa wafanye kazi hii basi sisi tutapambana nao na kama serikali imeshindwa kuwazuwia basi sisi tutawazuwia na tumeshajiandaa mikoa yote mitano tutapita wao wanakuja kutuchezea tunasema tupo tayari kwa lolote tumejiandaaa kwa lolote wanyama wale siwataji majina… tumefanya Mapinduzi hatutashindwa na wanyama wale ….tunasema mapema wapuuzi!!!!!! sisi wallahi tutapambana nao …waambiweeee. hapa hakuna vijana kuzungumza vijana wana kazi zao tulokuja hapa ni madingi maputu mmewaona …tutawatumia vijana wetu wapambane nao hao watu wanshabikia wanasema eheeee waambie wale…..
 Mkutano wa Jumuiya za wanawake, vijana wa CCM wa mikoa mitatu ya Unguja
 Salama Aboud Talib Aboud katika risala yake ya mikoa miwili ya Unguja amesema na kuwaambia wana CCM wasibabishwe na kikundi cha watu wanaotaka kuvunja Muungano wanaofanya mihadhara kwa kisingizio cha dini.Sheikh Juma Faki anasoma  Aya inayosema mnapotaka kufanya jambo basi watafuteni wenye akili, …… sio kila mtu tu anayekwiteni mnakubali tu ….Sheikh wa Uamsho wewe unasema unatuona sisi sio chochote sio lolote haaa haaaa CCM Oyeeee ….wallah nimepewa dakika kumi lakini haaaa CCM Oyeee….wanaijiita uamsho sisi tunawaambia tumeamka zamani na tumeamshwa zamani na Mzee Karume na Mwalimu Nyerere zamani sana tena.Wazee hawa walituamsha zamani ili wakati huo yeye Mzee Karume alipokwenda ulaya alikuwa anahusudu mambo ya huko na aliporudi ametuletea TV hatukuwa na radio tutakuwa na TV …HAAAA haaaa.Hapa kulikuwa na ngoma ya beni hapa ikipigwa na ndani ya beni lile kulikuwa na dua …Nyimbo inaimwa ‘mweheshimiwa twakupenda wewe lakini …….waafrika tutajitawala…..CCM… wana CCM wakapiga makofi na vigeregere alaaa, leo tumeshafika hapa hatukujua sisi kama tumeendelea leo tunapanda viscudo kina Pandu na Jecha …..CCM oyeeee.Ukitaka kufanya jambo ujiulize kwanza hili Jambo ninalolifanya lina faida gani kwa jambo hili leo wewe shekhe mzima na masheikh wenzio mnakwenda kusema rais wetu ni kibaraka yeye na kikwete hakheeee vipi yakheeee ahhhh na unasema unasomesha Quran,Fighi na masomo ya dini  ahhhh umeupataje usheikh huo?.Elimu na maarifa …wanachama wanasema wambie wambie……elimu sawa na fedha elimu walbaarifa. Elimu ufanye kwa maarifa …leo wewe muislamu hebu angalia pale Sayyid na Ibrahim alivyokabidhiwa pale Mji wa Madina aliomba ewe Mwenyeenzi Mungu ujaalie huu mji wa Madina uwe na amani leo nyinyi masheikh mnataka kutuchafulia amani alaaa, Na wewe Msellem mnataka kutuchafulia amani ahhhh wewe Msellem unavaa jokho leo?… akasema CCM OYEEE.Sheikh wewe Msellem upo airport kule tena sehemu muhimu sana, tumekupa dhamana lakini leo unafanya hivyo ……Hatujategemea, jamani nikuulizeni hivi CUF gani anayempenda CCM? Hakunaaaaaaaa.  leo mnasema Muungano uvunjike alaaaa umetizama weeeee umemurika weeeeeee alaaa sio unasema pweza sili lakini mchuzi unakula alaaaaa bara kule mnasema Tanzania bara hakuna wanalalamika kule alaaa watu hawapati viriri kama vile kwa nini? hivyo mnavyopiga nyie keleee uchumi unakuja chini, mnavyosema mnamdanganya nani? bara wenye pesa ilikuwa Mchaga peke yake akifuatiwa na Mpare lakini sasa Mzanzibari peke yake mwenye fedhaaaa ukikaa masaa mawili inakupitia mabasi ya mabwana makubwa…leo magari tele halafu mnasema Muungano hauna maana ehhhh…Muungano hauna maana eheee.Mwenyeenzi mwenyewe kasema …Sheikh ametoa aya inayozungumzia suala la mazingatia. Jeee do you think about that things, ndugu zetu mnakusanywa na watu wanaokutakieni maovu? watu wanakutieni pampu, nani anakutieni mori wanakuoneni mmestarehe katika nchi na Mwenyeenzi Mungu akikusudia kukupa anakupa lakini ……hamkupewa basi msignganganie.Nyinyi mnasema mmesoma ndio kusoma huko Sheik anatoa aya ya Ataamuruna nnsada bilbiri Mweyeenzi Mungu anasema ataaamuruna nnas ….bilbiri mmesoma ili muamrishe watu kufanya mazuri alioyaridhia Subhannah lakini leo mnasimamia ugomvi ili tuchukuane……ndugu hamjui kuwa tumeshaoana tumeshajukuu….wacheni kumchezea Mungu nyie…..Sheikh akatoa aya nyengine tena kuhusu ufisdi…Mwenyeenzi Mungu anasema inadhihiri fisadi baharini na nchi kavu kwa mambo manyoyachuma nyie wenyewe….akasema CCM Oyeeee.CCM Oyeee.
 Kama yule Mussa Sharifu (Hapa amekusudiwa Professa Abdul Shereef) kaja na mizani kule Bwawani eti anaupima uzanzibari anapima utanzania bara kuna mambo gani yametiwa huku na akayachukua ya kule na kutia huku, eti anasema mambo ya Zanzibar yameingizwa katika Muungano ndio mezani ikaja chini yote…hiyo mezani usiitupe tunakwambia kwani sisi hatujui upande ule Qurani na upande huu Shamba…Astaghafirullah …ah sio Qurani maandishi tu ya kiarabu….Sisi hatuitoi serikali hii ya Mapinduzi silaha zetu sisi tulikuwa na silaha na silaha zetu tuliotumia ilikuwa mapanga na nyundo hatukuwa na magobore wala bunduki sisi lakini baada ya kupindua tukaseja na sera na Mwenyeenzi Mungu alizipenda sra zetu maana tulisema katika sera tunataka amani na utulivu na hiyo Sayyid na Ibrahim alikuwa anataka amani na utulivu, tukaja na sera ya Elimu a hiyo Mwenyeenzi Mungu amehimiza ilmu, kaipenda Mwenyeenzi Mungu sera yetu ya kuondoa ubaguzi pia Mwenyeenzi Mungu akaipenda na hiyo.Sheikh: sema kweli japo inauma hii tutaisema wacha iwaumize sisi tumeikubali serikali ya Mapinduzi na Mapinduzi haya tumeyapata kwa rehema yake Mwenyeenzi Mungu sasa sisi tumeishapata neema tuifukuze? ….aya….tumekuwa tumbo ndani ya hasara sasa hivi mimi nina miaka 70 wallahi ingekuwa ninaendea mkongojo lakini sasa hivi wallah nipo very smart lakini ingekuwa utawala ule ule basi ningekuwa nimeshakwisha.Nasema tumekubali kuuwa na kuuliwa na waliobaki wambaki waliokufa wamekufa, tumefanya mapinduzi lakini wallah hatuitoi serikali hii hatutoi, eti tukakae pale Ikulu tumekaa katika vitu tuseme chukuweeeeeeni …..looo haaaa CCM CCM CCM …sisi hatukupiga kura kwa vyama bwana sisi tumeipata serikali hii ni neema alaaa tulivyoipata serikali hii tofauti na serikali ya Tanzania bara wao walitia bia katika chupa halafu wakaamina wakanywa na baadae Nyerere wakamwambia chukua serikali yako, walitaka kuuwacha utawala.Lakini sisi tulichua bado utawala na tukafanya mapinduzi wakati watawala wanaitaka nchi hiii tulibanwa watawala walikuwa wanaitaka …wallah thuma wallah hatuitoi tena, hapa Zanzibar kulikuwa na mabaraza ya kutunga sheria hapa kulikuwa na makureshi mabun saiddy na hakuna Pandu humo wala Jecha wallah.Wallah sisi CCM  ….. tulikuwa hatuna haja ya kufanya mikutano lakini wallah mmetufanya tufanye mikutano tutakujibuni moja baada ya moja ….ahsanteni…CCM CCM….CCM…Nyimbo inaimbwa …Januari huru jina Tanzaniaaaaaa….ameshuka jukwani.Viongozi wanatambulishwa yupo Bi Asha wa Balozi Seif Iddi, Asha Bakari, Waziri Machano Othman Said, Waziri Dk Mwinyihaji Makame, Waziri Ramadhan Abdallah Shaaban na wote wakatakiwa kuwasalimiwa wana CCM. WANASEMA.viongozi niliowataja hapo juu wanatajwa na kutakiwa wawasalimie wanachi wanasema kwa pamoja CCM Oyeeee Muungano Oyeeee wanajibiwa oyeeeee,
 CCM Oyeeee kidumu chama cha mapinduzi ….Muungano oyeeee …oyeee oyeeee…
 Ramadhan Abdallah (Kichupa) tunaishukuru serikali ya umoja wa kitaifa rais na makamo wake wote wanaendesha vizuri serikali, pili baraza la wawakilishi linatia hamu kulisikiliza na tunawaomba wajitahidi zaidi na majimbo yao yanajitahidi sana sana katika jitihada na jimbo zaidi lilivyonivutia ni jimbo la Balozi Seif Iddi la Kitope yeye na Mwakilishi wake Mshimba.Jamani sisi tumefanya uchaguzi mwaka jana 2010 sasa hebu tutazame mara hii wenye akili zake timamu watazame ni nchi imetulia hata wageni wanasifu na wengine wanakuja kujifunza kwetu sasa nasema utulivu huu umekuja na kila mmoja anafanya shughuli zake vizuri, tunakwena vizuri sasa niulize nani wa kujibu pindi hali hii ikiharibika?vyama vipo vimetulia sana CCM, CUF, na vyama vyengine, wametulia na wanazungumza lugha nzuri lakini viongozi wa dini ndio wanaotaka kuchafua hali hii lakini sisi tunawaambia kama wao wanataka kuwa wanasiasa basi hivi wanavyofanya wakachukue usajili kwa msajili wa chama kama walivyofanya wale waliojitoa CUF wameanzisha chama chao na wao wakaundwe chama chao.Lakini sio wawaambie watu wakatae Muungano kitendo hicho sio cha kiungwana huu Muungano sio zanzibar peke yake ni bara na Zanzibar naomba waombe kibali wakawaambie wenzao wapite kila mkoa wende kila pahali waaambie wazanzibari wa kule bara wakaseme tukatae Muungano.
 tuna wiraza ya ulinzi wakaseme wazanzibari rudini mkaseme hatutaki Muungano, wenye uhamiaji, wende wakaaambie wabunge kataeni Muungano halafu sisi mimi ni mstaafu wa Muungano maana tupo wengi tunakwenda kuchukua mishahara kila mwezi sasa utatwambia nini sisi wastaafu?na waaambie wale waliokuwa na majumba  kule bara wakatae Muungano na wajiandae mapema waondoshe mali zao na magari yao na nyumba kama zinaweza kuondoka basi ziondoke na mashamba yao waondoe maana watayaweka pwani kule maana huku ardhi imejaaa na pwani yenyewe kuanzia Nungwi mpaka Pemba ndio wakaweke magari yao.Sio watuulize sisi kama tunataka au hatutaki maana sisi tunajua faida za Muungano wao waliokuwa hawajui dini wala hawajasomeshwa inaonesha ndio wanaosema hawataki Muungao…..unapomkashifu Mwalimu Nyerere au Mzee Karume unakusudia nini?.Nashangaa hawa Uamsho wamekwenda Makunduchi kuwaambia watu wakatae huu Muungano alaaa wanawajua watu wa Makunduchi kuwa kule ni waasisi wa Muungano? tunaishukuru sana serikali yetu ya Muungano, kamati mmeiona ile nimefurahi sana kumuona mtu mmoja amechaguliwa mtu katika kamati ile ambaye kateuliwa katika kamati ile ya Kikwete alikuwa mkaidi sana kule Bwawani katika ule mkutano wao lakini nimemuona kule ….namsubiri nikikutana naye nitamuuliza vipi bwana?.….sisi ni binaadamu mataifa 50 ya Ulaya wameungana na kule nchi za kiarabu nchi zote ….zimeungana lakini leo kitoto kinatokea kwenye jukwaa eti kinasema  kataeni Muungano, tena wanatutisha maana wanasema mkisema kwiiii tutakuuweni nani mnamtisha alaaa na tuuweni basi kama na nyinyi mtabaki wafanye waone mwenye kutaka kufanya jambo hasemi bwana na wafanye waoneeeee hii.Tume sio ya kuulizwa mnautaka au hamuutaki Muungano, sasa tunasema Muungano upo na hakuna atakayeulizwa…wao Uamsho wanaogopa wanawaambia watu msende mtauliwa mnamdanganya nani hapa ….mimi nimewahi kuona Mapinduzi na nilishiriki kila kitu hakuna nilichokuwa sijakifanya na nilidhani nitakufa wakati wa Mapinduzi lakini siogopi mimi nikifa leo sina matatizo hebu tazameni hili wanaposema wanakheri kweli haya?….Tuwalaani kila wanapopita …tumekuja makusudi kama wametumwa na vyama vya siasa tunasema tutapambana nao……na kama wametumwa na vyama au wenyewe wanasiasa …tunasema tutakwenda kila pahala watakapokwenda wao ….kitakachokuja kuwapata shauri yao …..na tunaeleza mchana hakuna nyota….Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ramadhan Abdallah Ali (KICHUPA) anasema, tunababaishwa sana tukitajiwa muhadhara lakini neno muhadhara tunadhani ni wa kidini tu lakini ni neno la kiarabu tu lakini na iwe neno la kidini lakini neno la kidini unakwenda kuwaeleza watu maidha wakikubali au wakikataa, sasa kinachotushangaza wanachofanya hawa viongozi wa dini wanaojiita Uamsho wanakwenda mfano Makunduchi kwenda huko sasa hawa watu wengi wanakwenda na magari mengi kuna nini huko?.Hapa pana kichaka lakini wenzangu wameshazungumzia jambo jengine ni hawa wanaosema wanakwenda kutangaza dini lakini basi kwa nini waondoke mjini na magari 40 kwenda sehemu moja na watu ni wale wale kila siku?…….watu wanajibu kuwa hao ni  macuf ……Watu wanashabikia wanasema ndioooooooo. Waambiee. sisi CUF tumewaona kuwa wana heshima wamefanya mikutano yao bila ya kuwagusa CCM na sisi tunafanya mikutano yetu bila ya kuwataja wao CUF lakini Uamsho tunawagusa ka sababu kama wametumwa wafanye kazi hii basi sisi tutapambana nao na kama serikali imeshindwa kuwazuwia basi sisi tutawazuwia na tumeshajiandaa mikoa yote mitano tutapita wao wanakuja kutuchezea tunasema tupo tayari kwa lolote tumejiandaaa kwa lolote wanyama wale siwataji majina… tumefanya Mapinduzi hatutashindwa na wanyama wale ….tunasema mapema wapuuzi!!!!!! sisi wallahi tutapambana nao …waambiweeee. hapa hakuna vijana kuzungumza vijana wana kazi zao tulokuja hapa ni madingi maputu mmewaona …tutawatumia vijana wetu wapambane nao hao watu wanshabikia wanasema eheeee waambie wale…..Leo tumekuja kusema jambo kuna kijambo ndani yake wanatumia siasa kwa mgongo wa dini mimi ni Al-Hajj sisi sote waislamu hapa namuomba Mwenyeenzi Mungu anijaalie nimalize vizuri umri wangu …..watu hawa walianza misikitini kufanya hivi maana ukishasali kuna baadhi ya misikiti ilikuwa uondoke tu lakini ukisema unasubiri kusali basi utaona unalengwa wewe maaana CCM yuleeeee.….Lakini sasa tena wanakuja hapa majukwaani na kuanza kutukana viongozi wetu sasa wamevuka mipaka tunasema hiki chuo cha kiislamu ndipo waliposoma hawa lakini kile chuo kimejengwa na Mzee Karume na mtu akijenga chuo na watu wakisoma huwa anapata fungu sasa imekuwa hilo fungu halipatikani sisi tunasemahilo fungu tutalionesha hapa hapa tunasema kama wanatwambia watatuuwa basi Mwenyeenzi Mungu anasema anayekuja kukuuwa muue yeye kwanza kwa hivyo kama wanatwambia tukatae Muungano wallahi hatukubali kuukataa Muungano ……sisi Muungano tunaujua sana kuliko wao……..

1 comment:

  1. Je Zanziabr tutafika tuendako?

    Kama leo vijana wa ccm kwa kupokea maagizo au kwa hiari zao wanaamua kuzishambulia jumuia za kirai zilizowekwa kisheria, ati kisa kutoa elimu ya kiraia kuhusu muungano.
    Huu ni msiba mkubwa!

    Ukiangalia hawana hata uwezo wa kujenga hoja, wameishia kuwatukana viongozi wa dini. Kama hoja ni mzanzibar kuwa BARA na kujitafutia maisha hili hakuna atakaelipinga.
    kwani hapa ZNZ kuna wageni wangapi wanaotafuta maisha sembuse Wabara?

    Huu ni mpango wa siri ulioandaliwa kutukoroga na kutuvuruga. Je hii sio ile dera ya wagawe, wasahaulishe watawale?
    Bila shaka, ukiwaona vijana kama hawa wa CCM wakibweka kwa nguvu zote kushadidia Muungano hata ikibidi kugombana na viongozi wa dini, ujue lipo jambo!

    Hata huyo Karume wanaedai kumpenda na kumuenzi alinukuliwa akisema " Muungano kama koti likikubana unalivua" Je CCM ZANZIBAR mnalijua hili?

    Je hizi ni harakatia za kutetea posho mnazopewa DODOMA katika vikao vya kuivuruga Zanzibar?
    Je nyinyi ndio mapandikizi yaliyopewa kazi ya kuziuia mabadiliko Zanziba?

    Lipo jambo! Lbda CCM-ZANZIBAR watuonoshe faida lukuki za MUUNGANO huu badala ya kutukana watu.Hapo tutawaelewa.

    Taasisi za kiislamu ZNZ katika mikutano yote walijitutumua kujenga hoja kuhusu ubora ama udhaifu wa muungano. Mbona nyie hamfanyi ivyo?
    Mnaishia kutukana watu.

    Kwa masikitiko makubwa CCM-ZNZ HAWAMJUI ADUI WAO WA SIKU ZOTE (MUUNGANO)

    Au mnataka kutuaminisha kuwa nyinyi ni askari wa JANJAWEED walioendesha uharamia kuvuruga uchaguzi mkuu mwaka 2000?
    Nona kizazi hiki kimepotea kabisa.

    Mwisho Wazanzibari wajue kuwa huu ni muda muafaka wa kuleta mabadiliko ktk nchi yao kupitia marekebisho haya ya katiba.

    WAZANZIBARI TUUNGANE, TUTETEE NCHI YETU TUSIDANGANYIKE NA HAWA VIJANA WALIOJAA NJAA.

    KWAO WAO BORA CCM KULIKO ZANZIBAR.

    ZANZIBAR HURU BILA YA MUUNGANO INAWEZEKANA.

    Naomba kuwasilisha bila Jazba!

    ReplyDelete