Tuesday, May 29, 2012

CCM YATAKA JUMUIYA YA UAMSHO NCHINI ZANZIBAR IFUTWE MARA MOJA VUAI ALI VUAI ASEMA KAMA ALIYE PAYUKWA KWA SABABU YAKUHIFADHI TOGE NA FUPA LAKE


VUAI ALI VUAI AHARA AKIJIPAKA KWA UTAMU WA MADARAKA

Chama cha Mapinduzi kimetoa shinikizo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kumtaka Waziri wa Sheria na Katiba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Abubakar Khamis Bakar ajiuzulu kwa madai ya kushindwa kuishauri vizuri Serikali katika suala la kudhibiti asasi za kiraia ikiwemo kikundi cha “Uamsho”.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi kimetaka kufutwa mara moja kwa Jumuiya ya “Uamsho” kwa sababu imekwenda kinyume na malengo yake ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ambayo kazi yake kutoa elimu kuhusu mihadhara ya Dini ya Kiislamu tu.
Akizungumza na waandishi wa habari hapo makao makuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai  amesema leo, kuwa kikundi cha kutoa mihadhara ya Dini ya Kiislamu cha “Uamsho” kimesajiliwa kwa ajili ya kutoa mihadhara ya mambo ya dini tu na sio kujishungulisha na siasa za majukwaa, ikiwemo kuwahoji wananchi kuhusu uhalali wa Muungano wa Tanzania na kuwakashifu viongozi wa Serikali, wakiwemo Waasisi wa Taifa hili.
Alisema kitendo cha Waziri wa Katiba na Sheria kushindwa kuishauri vizuri Serikali kuhusu mwenendo wa kikundi hicho, ndiyo kimesababisha maafa makubwa na kuiingiza nchi katika wasiwasi mkubwa kiasi kuvurugika kwa sekta ya biashara na utalii, “Chama Cha Mapinduzi, kinamtaka Waziri wa Sheria na Katiba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kujiuzulu mara moja kwa sababu ameshindwa kumshauri vizuri Rais pamoja na Serikali kuhusu mwenendo wa kikundi cha “Uamsho” ambacho kinafahamika kwamba kazi yake kutoa mihadhara ya kidini tu na siyo siasa,” alisema Vuai.
Akifafanua zaidi Vuai alisema, kwa mfano, vyama vya hiari vyote vilivyopata usajili wa kudumu wa kufanya shunguli zao vinasajiliwa katika Ofisi ya Katiba na Sheria ambayo ipo katika Wizara yake.
Aidha, alisema Mawaziri wa Sserikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walikutana pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa na Viongozi wa “Uamsho” tarehe 25 Aprili na kutaka kikundi hicho kuacha kufanya mihadhara inayohusiana na mambo ya siasa au kitachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Kwa mfano, alisema hivi karibuni Jeshi la Polisi lilizuia utoaji wa vibali kwa Viongozi wa chama hicho, lakini vibali vilitolewa katika Ofisi za Mufti ambazo zipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria, “Tulimtaka Waziri wa Katiba kulifanyia kazi suala hilo kuona kwamba kikundi hicho hakifanyi mihadhara inayohusiana na mambo ya siasa ikiwemo kuwakashifu viongozi na kuhoji uhalali wa Muungano, lakini hakufanya kazi hiyo,” alisema Vuai.
Vuai alisema, hivi sasa Chama Cha Mapinduzi kimetambua na kufahamu kwamba Jumuiya ya “Uamsho” ipo katika kivuli cha chama kimoja cha siasa na ndiyo maana kimekuwa kikifanya kiburi na jeuri kiasi ya kutamka kwamba hakuna mtu wa kukifuta.
Aidha, Vuai alisisitiza na kuitaka Serikali kuifuta Taasisi ya “Uamsho” mara moja kwa sababu imekwenda kinyume na dhamira yake ya kuanzishwa, “Tunaitaka Serikali kuifuta mara moja Taasisi ya “Uamsho” kwa sababu imekwenda kinyume na malengo ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo,” alisema Vuai.
Aidha, Vuai aliwataka wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi kuwa watulivu katika kipindi chote na kuacha kujishungulisha na vurugu hizo ambazo zinahatarisha amani na utulivu.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya “Uamsho”, Taasisi hiyo itakuwa na kazi ya kutoa mihadhara ya kidini kwa waumini na wafuasi wake na kulinda haki za binaadamu kwa makundi ya Waislamu mbalimbali.
Aidha, Jumuiya hiyo kazi yake ni kusaidia kutatua matatizo ya kijamii, ikiwemo migogoro na majanga mbalimbali yakiwemo waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI. Katiba ya chama hicho inapiga marufuku Taasisi hiyo kujishungulisha na mambo ya kisiasa, ikiwemo viongozi wake.
HAYA SASA HUYU DUWA YA MAISARA ISHAMNASA ANAPAYUKWA KAMA ALIYE KUNYWA CHIBUKU NA VOTKA KWA WAKATI MOJA HAWA WOTE SIO VIONGOZI KABISA WANAO ITAKIA ZANZIBAR MEMA HAWA NDIO MAZIMWI NA MADUWA WA NCHI YETU YA ZANZIBAR NA SISI RAI MASIKINI PIA ALA DUWA NDIZO ZITAKAZO WAMALIZA MOJA MOJA.

No comments:

Post a Comment