Tuesday, May 29, 2012

HAKUNA MGAWANYIKO UAMSHO! WANAFIKI M/MUNGU ANAWAONA


ASSALAMU ALAKUM
Kila sifa njema anastahiki M/Mungu rehma na amani zimshukie Mtume Muhammad (S.A.W) Na ahli zake na maswahaba zake na waliowema katika uislamu.
nachukuwa fursa hii kukanusha uvumi unaoenezwa na wanafiki na mafisadi wasiotakia mema zanzibar na uamsho kuwa kuna kutofahamiana baina yetu na mimi nimeondoka kinyemela kwenda Oman.
Nasema hizi ni khabari za uongo safari yangu ya oman nilipanga zamani na niliikhairisha ili niwahi dua ya pamoja maisara na baada ya dua na kuhutubia niliondoka siku hiyo hiyo na viongozi wangu wote wajuu wanajuwa kuwapo safari hii nia ya safari yangu ni kufanya uchunguzi wa afya yangu na nishawahi kwenda india mara mbili kwa ajili hiyo na ilikuwa nikae oman wiki tatu lakini nimeamua kurudi nyumbani haraka iwezekanavyo na Sheikh Mselem safari yake ya Pemba ilikuwa imepangwa wala yeye hakukimbia wala hatukugawanyika sote tuna mawasiliano na mashauriano wao wametaka nibakie kidogo kutizama Afya yangu lakini nimeamua kurudi nyumbani haraka niungane na wenzangu katika harakati za kukomboa nchi yetu kwa amani na utulivu najuwa kuwa polisi walivunja nyumba zangu kunitafuta mimi niliondokea katika kiwanja cha ndege cha zanzibar kwa taratibu zote za sharia siku ya ijumaa ya 25/05/2012 wale wanaovumisha kuwa tumegawika wajuwe sisi hawawezi kutugawa kwa sababu tumeungana kwa ajili ya mungu na naamini mungu yuko pamoja nasi.
Nasaha zangu kwa wanzanzibar tutulie viongozi wenu tuko salama tusikubali kugawiwa tukarudishwa tulikotoka zanzibar ni nchi yetu tukiiharibu hatuna nyengine maaduwi walikuwa wanatafuta siku nyingi sababu ya kutugawa kwa hivyo tusiwape sababu tuilinde amani tuilinde nchi yetu tumuenzi rais wetu mungu ibariki zanzibar wabariki na watu wake AMIN
ndugu yenu
AZZAN KHALID HAMDAN
NAIBU AMIR
JUMIKI

No comments:

Post a Comment