Monday, May 28, 2012

JESHI LA WAKURI WAKUTOKA TANGANYIKA WARIPUWA MABOMU YA MACHOZI NCHINI ZANZIBAR


Zanzibar yaripuliwa kwa mabomo ya machozi na jeshi la wakuri kutoka tanganyika
Monday, 28 May 2012 FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA
ZANZIBAR imechafuka. Baada ya kuwapo kwa amani kwa takribani mwaka mmoja tangu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, vurugu na hali ya wasiwasi zimeibuka tena baada ya wanaharakati wa KIZANZIBAR kufanya maandamano kutaka uhuru wa NCHI YAO YA ZANZIBAR KUWA HURU.
Zanzibar ilijikuta katika hali tete kiusalama tangu mwaka 1995 baadaya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais, ambayo Chama cha Mapinduzi (CCM) kiilibuka kidedea kwa kuiba kura na kutangaza kuwa kimeshinda na Chama cha Wananchi (CUF) kupinga, lakini uhasama huo ulizikwa Julai 31 mwaka 2010, baada ya kura ya maoni ya kuunda Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa na wazanzibar wote kuungana na na kuwa wamoja.
Lakini kuanzia juzi usiku hadi jana jioni mji wa Unguja na viunga vyake ulitikiswa na mabomu ya kutoa machozi ambayo polisi waliyatumia kutawanya mamia ya wanaharakati hao wa KIZANZIBAR.
Mabomu ya machozi yalipigwa mfululizo juzi usiku na kuendelea kutwa nzima jana, hivyo kuathiri shughuli za biashara,na amani na utulivu kwa sababu ya mabomu hayo yaliyokuwa yakipinwa na askari wa polisi wakitokea bara na kuwapiga wanchi wa kizanzibar na kuwasaka na kusababisha hofu kwa wananchi wanaoishi katika nchi hii ya ZANZIBAR.
Kwa muda wa saa takriban mbili hivi kati ya saa 3:00 na saa 5:00 asubuhi, helkopta ya polisi ya watanganyika ilikuwa ikipasua anga la Zanzibar ambalo lilikuwa limetandwa na moshi uliotokana na mabomu ya machozi yaliyokuwa yakifyatuliwa na maskari wa kitanganyika waliyomwagwa zanzibar kuwathibiti wanaharakati wa kizanzibar wanao dai nchi yao kuwa huru kutoka katika ukoloni huu wa KITANGANYIKA KWA MUDA WA MIAKA 48 SASA TANGANYIKA INAITAWALA ZANZIBAR KWA MABAVU YA GUVU ZA KIJESHI NA POLOSI.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar,MNAFIKI   Mussa Ali Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa wafuasi hao wamefanya uharibifu mkubwa ikiwa pamoja na kuchoma moto makanisa mawili na kwamba, watu saba akiwamo Imamu wa Msikiti wa Bizeredi, Maalim Mussa Juma wanaotuhumiwa na matukio hayo wamekamatwa na jeshi hilo.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Askofu Dickoson Maganga alisema watu wasiojulikana walivamia kanisa lao eneo la Kariakoo Mjini Zanzibar mnamo saa 4.30 usiku na kuvunja ukuta, kuchoma viti vya plasitiki pamoja na gari yake.
Chanzo cha vurugu hizo kinatajwa kuwa ni wanaharakati hao wanaotaka nchi ya zanzibar kuwa huru juzi kufanya mkusanyiko na maandamano makubwa ya kushtukiza ambayo yalizistua mamlaka za usalama NCHINI HUMO, lakini baada ya kutawanyika jioni baadhi ya viongozi wa maandamano hayo walitiwa mbaroni bila ya kisa wala sababu hii nikuonyesha wazi kuwa ukoloni wa kitanganyika unaendelea kuwadidimiza wananchi wa zanzibar kusita kudai nchi yao.
Baada ya kukamatwa kwao, wafuasi wao walikusanyika makao makuu ya polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Madema, kushinikiza kutolewa kwa viongozi hao wanaoshikiliwa kituoni hapo.
Habari zaidi zinasema kutokana na hali ilivyo, askari polisi wakitanganyika walitarajiwa kuongezwa NCHINI HUMO ZANZIBAR, ili kusaidia kuimarisha hali ya UDIKTETA pia kuwadhibiti WANANCHI WA ZANZIBAR WANAO DAI NCHI YAO KUWA HURU ambao walikuwa wameanza kuelekea nje ya maeneo ya mji.
Tayari kuna taarifa kuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa TANGANYIKA (JWT) kutoka Tanganyika jana mchana walingiaNchini Zanzibar kisirisiri kwa ajili ya kuongeza utawala wa kimabavu katika mji wa Unguja.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza hakuna kiongozi yoyote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) aliyetoa kauli kuhusu hali hiyo MIJINAFIKI MIKUBWA.
Kauli ya Polisi
MNAFIKI Kamishna Mussa alisema jeshi lake litaendelea kuwasaka na kuwatia mikononi wote waliopanga KUDAI UHURU WA NCHI YA ZANZIBAR  pamoja na viongozi wote wa JUMIKI.
“Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar ndio iliyohusika na kuwachochea vijana kukusanyika na kufanya uharibifu ikiwemo kuchoma moto gari, kupanga mawe barabarani na kufanya hujuma mbalimbali kinyume cha sheria alisema MNAFIKI HUYO KAMISHA MUSSA. Tutaendelea kuwasaka kwa gharama zote,” aliapa Kamishna Mussa.
Alifafanua kwamba kwa sasa mikusanyiko yote ya mihadhara ya kidini na vyama vya siasa, lazima ipate kibali cha polisi vyinginevyo jeshi lake lawakuria wakutoka tanganyika litatumia nguvu za ziada kutawanya mikusanyiko hiyo ili kulinda utawala wa kitanganyika kuendele na kudumisha nchini humo zanzibar,
Hata hivyo, kamishna huyo wa polisi alijizuia kuhusisha harakati za Uamsho na chama cha siasa wala kutaja majina ya viongozi ambao tayari wanashikiliwa na jeshi lake kuria kutoka tanganyika.
“Mpaka sasa hivi sina majina yao kwa jumla, lakini tumewakamata viongozi wa Uamsho na tunatendelea kuwasaka lakini jina moja tu ndio ninalo ambalo ni Mussa Abdallah Juma,” alisema Kamishna huyo.
Hali bado tete
Wakati jeshi la wakuri litoa onyo hilo, hali ya usalama ilionekana kuwa bado tete huku maeneo kadhaa ya Mji wa Zanzibar hasa Darajani na Michenzani ambako muda wote ni sehemu zenye harakati nyingi za biashara, jana zilikuwa zimebakia bila pirikapirika kutokana na askari wa kikuri waliojazwa nchini zanzibar walioamuwa kufanya doria katika mitaa yote na kulipua mabomu kila penye kikundi cha watu waliokusanyika wakinywa kahawa au hata batata za orojo wakuri walikuwa wakifyatuwa mabomu ya machozi.
Mitaa hiyo ilikuwa imechafuliwa kwa mawe, matofali na magogo yaliowekwa barabarani ili kuziba njia kwa ajili kuzuia magari yasipite huku mipira ya magari ikiwashwa moto na vijana hao ambao ndio rai halali wa nchi hii ya zanzibar sio jeshi la wakuri linalo leta ubabe.
Kwa upande wake Askofu Maganga     akizungumzia uvamizi kanisani kwake alisema:
“Nasikitika sana kwa tukio hili ambalo tayari tumeiarifu polisi ambao jana (juzi), usiku walifika hapa wakishirikiana na kikosi cha kuzima moto na kufanikiwa kuuzima moto huo ambao kwa habati nzuri haujaathiri paa la kanisa letu,” alishukuru kiongozi huyo.
Alisema kundi la watu ambalo lilikuwa likitoa maneno ya kashfa na kutishia maisha ya waumini waliokuwa wakifanya ibada usiku huo, lilikatisha ibada hiyo pamoja na kusababisha uharibifu wa mali ya kanisa hilo yenye thamani ya zaidi ya Sh 100 millioni.hata mimi muandishi ilibidi nicheke kwanza ati nini zaidi ya sh 100 million hahahahaha au anazisikia tu ndio akamuwa kuzisema ni kacheka tena hahahaha.
Kauli ya JUMIKI
Kutokana na hali hiyo, jumuiya hiyo jana ilitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari ikikanusha kuhusika na kuchochea watu kuchoma kanisa wala kuharibu mali za watu.
Hata hivyo, Katibu wa Jumuiya hiyo, Abdallah Said alisema katika taarifa hiyo kwamba jeshi la polisi linapaswa kubeba lawama kwa yote yaliotokea kutokana na kuvunja sheria na kuwakamata viongozi bila ya utaratibu wa busara.
“Uislamu ni dini ya amani na inahimiza ushirikiano na utulivu na hatuwezi kuwatuma watu kwenda kuvunja makanisa na kuharibu mali, kwa sababu ndani ya imani zetu tunajua hilo ni kosa na jambo ambalo halifai katika maamrisho ya dini yetu,” alisema Sheikh Abdallah.
Taarifa hiyo ilisema pia kwamba jumuiya hiyo imekuwa wazi katika kudai maslahi ya Zanzibar na sio vinginevyo na kuahidi kufanya hivyo kwa njia za amani, na iwapo watakuwa wamekosea basi wapo tayari kufikishwa katika vyombo vya sheria.
“Ni lazima polisi wajue kwamba tupo tayari kufanya kazi kwa misingi ya kisheria na hata kwa kujisalimisha tupo tayari, lakini ukamataji bila kufuata busara na sheria haukubaliki. Tunachokitaka ni kura ya maoni haraka na hilo tutaendelea kulidai,” alisisitiza katibu huyo wa JUMIKI.
Wakati viongozi wa Uamsho wakiendelea kutafutwa na jeshi la polisi, wa kikuri waliojazwa nchini humo zanzibar nyumba ya kiongozi aliyeongoza maandamano juzi Sheikh Farid Hadi Ahmed inadaiwa kuvunjwa milango usiku wa manane alipokuwa akisakwa jeshi hilo la wakuri wa kitanganyika. polisi waliofanya kitendo hicho manastahiki kushatakiwa lakini watashtakiwa vipi na wao ndio wakoloni weusi..?, wanafamilia wanasema waligongewa milango na kutakiwa wafungue baada ya kutofungua walisikia kishindo kikubwa cha kusukumwa milango katika eneo la Mbuyuni Mjini Unguja.
Vijana katika mitaa ya Zanzibar jana walionekana wakiwa na hamasa kubwa wakidai kuendelea kuungana na viongozi wao kudai haki ya Zanzibar, pamoja na kutaka Zanzibar huru kutoka ndani ya mikono ya  wakoloni weusi wa kitanganyika kwa kuvunja Muungano.
“Sisi tunachokitaka Zanzibar yetu watupige mabomu, watuue, watukamate lakini tunataka Zanzibar yetu na hatusikii lolote,” walisikika baadhi ya vijana hao wakisema wenye uchungu na nchi yao ya zanzibar.
Hadi jana jioni vurugu katika badhi ya maeneo hususan Kwerekwe na njia ya Baa ya Amani zilikuwa zikiendelea na gari moja lilichomwa moto karibu na ofisi ya CCM.
Matukio kabla
Zanzibar imekuwa ikitawaliwa na matukio ya ghasia ambayo licha ya mihadhara hiyo ya Kiislam ilikuwa ni uhasama wa kisiasa kati ya vyama vikuu vya CUF na CCM, hatua ambayo iliwahi kusababisha mauaji ya Januari 27, mwaka 2001.
Lakini, uhasama huo wa kisiasa ambao ni wa kihistoria ulizikwa baada ya kura hiyo ya maoni na uchaguzi mkuu wa 2010 hatua ambayo imemfanya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa SMZ huku baadhi ya mawaziri pia wakitoka katika chama hicho.
Hata hivyo, wanaharakati hao wanye uchungu na nchi yao ya zanzibar wameanza upya kudai uhuru wa  Zanzibar wakishinikiza visiwa hivyo viwe taifa huru kwa kujitenga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.ambao wengi wao sasa wameamka na kujuwa kuwa sio jamhuri ya muungano wa tanzania bali ni utawala wa kimabavu wa kitanganyika zaidi ya nchi hii dogo ya zanzibar
Zitto ataka tume ya uchunguzi
Katika hatua nyingine Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemtaka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aunde kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti
vurugu hizo na kuanza mazungumzo na pande zote kwa kuwa, “Hiki sio kitendo cha kudharau
kabisa.”
Alifafanua kwamba waliochoma nyumba za ibada wasakwe na kufikishwa mbele ya sheria mara
moja na kuongeza, “Tusiruhusu hata kidogo wapuuzi wachache kutuingiza katika vurugu za
kidini ili kufikia malengo yao ya kisiasa.”ati wapuuzi wachache zanzibar nzima inadai uhuru wa nchi wanawake na wanaume vijana na wazee kisha anasema wapuuzi hii nikuthibitisha wazi kuwa hawahishimu kabisa zanzibar.

No comments:

Post a Comment