Thursday, May 17, 2012

MASHAITWANI MAWILI YAZUKA PEMBA KUZUIA UAMSHO KUTOKUELIMISHA WANANCHI

Mkuu wa Mkoa ya Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi
Ujio wa mchakato wa katiba mpya na katazo la baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar kuzuia mikutano ya hadhara ya wananchi na Asasi zisizokuwa za kiserikali kuzungumzia suala zima la mchakato wa katiba ni mwendelezo wa kubana uhuru wa kujieleza. Tumewasikia Wakuu wa Mikoa ya Pemba,Dadi Faki Dadi wa Kaskazini na yule wa Kusini, Juma Kassim Tindwa wakiweka masharti magumu na urasimu usiokuwa wa lazima eti kama Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam(JUMIKI) mikutano yake haifai. Wakuu hao wa Mikoa wamekataza kabisa kufanyika kwa mikutano ya aina yoyote katika Mikoa yao.Tunaomba wananchi wote wa pemba na unguja kuzingatia sana sana viongozi kama hawa kuwa sio viongozi bali ni majambazi wakubwa wa umaa wa zanzibar na majitu kama haya ndio yaliyo itia umasikini zanzibar yetu.kwa hiyo duwa ya maisara inaendeleya kufanya kazi yake inawafichuwa wanafiki na wasaliti wote wa wazanzibar nasi tuwajuwe maana tulikuwa hatuwajuwi tukiona ni viongozi wetu kumbe ni mazimwi.hayataki hata siku moja wananchi wafaidike na neema ya nchi wanataka wao tu ndio wale wakinenepa lakini mwaka huu waula na chuyaaa wananchi funguweni macho na tuwakumbuke hawa uchanguzi ujao hata wazikiri uchi wa mnyama tusiwapa kabisa maana wao hawataki kutupa sisi uhuru wetu.

No comments:

Post a Comment