Wednesday, May 2, 2012

SERIKALI YA GNU (SUK) YASEMA MIHADHARA NA MAKONGAMANO SASA BASI JE NI GNU((SUK))HII TULIYO ICHANGUA AU KUMBE NI MKONO WA NYERERE ULIJIFICHA....???

 WATOTO WA FIRAUNI UTAWAJUWA TU HATA UWATIYE NDANI YA CHUPA WATATOWA KIDOLE WASEME NIKO HAPAAAA


Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed leo amezungunza na waandishi wa habari Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeleza kuwa Tume ya marekebisho ya Katiba iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi imezinduliwa rasmi leo na Mawaziri husika na kuanzia sasa itaanza kazi yake rasmi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Akitoa taarifa rasmi ya Serikali Ofisini kwake Vuga mbele ya waandishi wa habari, Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed amesema katika kufanya kazi zake Tume inaongozwa na hadidu rejea mahasusi ambazo madhumuni yake ni kupata maoni ya kuwa na Katiba muafaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Amesema maoni yatayotolewa nje ya hadidu rejea yanaweza kusikilizwa na Tume lakini inaouwezo wa kuyakataa, hivyo ni vyema wananchi wazingatie sana msingi huo. Waziri Aboud amesema kabla ya kuanza rasmi kwa kazi za Tume, baadhi ya vikundi vya kijamii na taasisi zisizo za kiserikali zilikuwa zimeanza harakati za kushajiisha na baadhi yao kuelimisha wananchi juu ya suala zima la maandalizi ya Katiba mpya, hivyo serikali imetanabahisha kwamba kuanzia sasa kazi ya kuelimisha, kushajiisha na kuhamasisha wananchi juu ya maandalizi ya katiba mpya yanapaswa yafuate utaratibu maalum uliowekwa katika sheria ya marekebisho ya Katiba ya mwaka 2012.Amesema sheria hiyo inawataka watu, vikundi au taasisi zinazotaka kuendesha programu za kujenga uwelewa kwa wananchi kuhusu suala hili kutoa taarifa kwa maandishi kwa Tume, au kwa niaba yake kwa Mkuu wa Wilaya, au Afisa Tawala wa Mkoa, au Mkurugenzi wa Manispaa au Katibu wa Halmshauri za Wilaya na katika taarifa hiyo ielezwe wazi chanzo cha fedha za kuendesha programu hizo, tarehe, muda na pahala patakapotumika na mada zitakazotolewa na kujadiliwa.Ameongeza kuwa baada ya kupata ruhusa ya Tume na iwapo programu hizo zitahusisha mikutano ya hadhara, maandamano au mikusanyiko ya aina yoyote ya watu ni lazima Sheria za nchi zinazohusika na mikutano ya hadhara zifuatwe kwa kutoa taarifa na kupata ruhusa ya Jeshi la Polisi.Taarifa hiyo imesisitiza kuwa mtu ama kikundi kitakachoendesha shughuli ya kuelimisha wananchi kuhusu Katiba mpya bila ya kufuata utaratibu uliowekwa adhabu ya kosa hilo ni kifungo kisichopungua mwaka mmoja au faini isiyopungua shilingi milioni mbili au adhabu zote mbili kwa pamoja hivyo imewataka wananchi kufuata sheria ili kuwaepusha kuingia katika makosa..Waziri Aboud amesema ili kulinda amani, utulivu na umoja wetu, Serikali inawahakikishia wananchi kwamba itachukua juhudi zote ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa yenye utulivu na amani na vyombo vya ulinzi na usalama vitakuwa makini kuhakikisha kuwa wale wote wenye lengo la kuvunja amani wanadhibitiwa na kuchukuliwa hatua zinazostahiki. Hivyo amewaomba wananchi wote kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kwa Tume kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa na Tume.

No comments:

Post a Comment