Wednesday, May 30, 2012

SHEIKH FARID ANGURUMA KAMA SIMBA ASEMA HATURUDI NYUMA


Kiongozi wa Maimamu Zanzibar, Farid Hadi Ahmed akiongea na waumini katika msikiti wa Mbuyuni Zanzibar jana baada ya sala ya alaasiri.

Wananchi wa Zanzibar wenye asilimia 99% ya dini ya kiislamu wakiwa ndani ya msikiti wa Mbuyuni
wakionesha mabango ya kukataa Muungano wakati Sheikh Farid (hayupo pichani) akizungumza


JUMUIYA ya Mihadhara ya kiislamu (Uamsho) imetoa msimamo mkali zidi ya Serikali ikisema kuwa haitarudi nyuma katika kudai uhuru wa Zanzibar.
Wakizungumza katika msikiti wa Mbuyuni uliopo eneo la Darajani mjini Zanzibar, viongozi wa Uamsho wamewataka Wazanzibari kutolegezamsimamo wao hata kama jeshi la polisi limezingira mji wao.
Umoja wetu ndiyo utakao tukomboa nchi yetu, msikubali kuyumbishwa na kitu chochote wala kulegeza msimamo wetu. Jambo moja tu, ni mpaka kieleweke.
Bila hivyo hakuna jeshi, hakuna polisi atakaye tuyumbisha” alisema Sheikh Mussa Juma wa msikiti huo na kuitikiwa na wafuasi waliokuwa wamefurika katika msikiti huo “ndiyooooo!”
Wafuasi hao walikuwa wameshikilia karatasi zilizoandikwa “hatuutaki muungano, tunaitaka Zanzibar yetu”.
Naye Sheikh Mussa Juma aliyekuwa amekamatwa na jeshi la polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana aliwapongeza wanachi waliotoka na kuandaa na akisema kuwa hawatarudi nyuma, Tunawashukuru Wazanzibari kwa sababu meonyesha kutotaka kutawaliwa” alisema na kuwauliza wafuasi hao “mko tayari” nao wakijibu “Tuko tayariii”
Naye Sheikh Farid Hadi Ahmed alisema kuwa kundi hilo linafuata taratibu hivyo halipaswi kulaumiwa kwa kufanya vurugu. Aliwataka pia Wazanzibari kutogawanyika kwa vyama vya siasa,Muone katika silaha kubwa wanayotumia maadui ni kutugawa kivyama na kikabila au kirangi, inasikitisha sana.”
Huku akinukuu Katiba ya Zanzibar ibara ya 23 sheikh Farid alisema kuwa kila Mzanzibari anapaswa kuhifadhi mamlaka na uhuru wa Zanzibar.
Aliwahamasisha wafuasi hao kuonyesha mabango waliyokuwa wameshikilia na kumtaka mkuu wa jeshi la polisi kutambua hitaji kubwa la Wazanzibari.
Hebu mwonyesheni IGP mlichonacho….. mnautaka muungano hamuutaki? (wote wakajibu) “hatuutaki!).
Huku akitoa mifano, Farid aliendelea kusema kuwa kilichopo ni wimbi la Wazanzibari kudai nchi yao.
Alisema kuwa kama vile maji ambayo yakizibwa katika njia yake husambaa mitaani, hivyo ndivyo Wazanzibari wanavyosambaa mitaani kudai nchi yao.
Alitetea kitendo cha jumuiya hiyo kuandamana akisema kuwa si kosa kisheria kutembea barabara.
Kwani mtu akitembea kwenye nchi yake anatembea kwa kibali? Sisi tumeamua kutembea… waliokuja na wake zao wametemebea na Mwenyezi Mungu kajalia tumetembea kwa furaha yote. Mbona timu zinafanya mazoezi, zinachukua vibali, watu wanakwenda hitimani wanapewa vibali?” alihoji.
Sheik Faridi alitangaza siku ya  26 kuwa ni ya maandamano kwa Wazanzibari na kuwataka wanajeshi wa Kizanzibari kujiandaa kuwaunga mkono katika maandamano hayo.
Huku akikwepa lawama kwa kundi hilo kwamba limekuwa likichoma na kuharibu makanisa, Sheikh Farid aliwalaani watu wanaounganisha kundi hilo na tuhuma hizo, Tunamwambia IGP kamishina hana uwezo hana uwezo. Wanajeshi tunao…. Vikosi vina watu 8000 waambie wajindae wasibebe silaha ni ndugu zetu… waje wakae barabarani wala sisi hatuhitaji ulinzi” alisema na kuongeza,
Lakini tuna wasi wasi na hawa wanaolipua makanisa na sisi tunawalaani vibaya, hawa tunaamini ndiyo wale wale waliokuwa wakisimama na kutukana matusi, tena wana visu, wana nondo, wana pesa Mheshimiwa IGP waambie wakupe rekodi.”alisema Farid.
Licha ya Waziri katika Ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais Mohammed Aboud kukemea mihadhara hiyo, jeshi la polisi halikuthubutu kuingilia mkutano huo.
Magari yaliyosheheni askari polisi yalionekana yakipita mbali na eneo hilo bila kuwabughudhi.

No comments:

Post a Comment