Thursday, May 3, 2012

TUME YA MAFISADI YAANZA KAZI RASMI((TUME YA KATIBA AMBAYO Z,BAR HATUTAKI HATA KUISIKIA))

 

TUME ya Katiba jana ilizinduliwa rasmi na kukabidhiwa ofisi huku, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akieleza kuwa itapewa zana za kisasa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ikiwamo kila mjumbe kupewa gari jipya na nyumba Dar es Salaam.Akizungumza wakati wa kukabidhi ofisi hiyo, Balozi Sefue alitaja mambo 10 ambayo Serikali itayafanya kwa tume hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati alipoiapisha Aprili 13, mwaka huu.“Serikali inafanya utaratibu wa kununua magari mapya 30 ili kuwarahisishia wajumbe usafiri wa kuwafikia wananchi. Leo (jana) tutakabidhi baadhi ya magari hayo kwa tume,” alisema Balozi Sefue.Aidha, alisema makamishna hao hasa wale wanaoishi nje ya Dar es Salaam watapewa nyumba ili wasipate shida ya pa kuishi wakati wa kutekeleza majukumu yao.
“Najua wapo baadhi ya wajumbe ambao wanaishi nje ya Dar es Salaam, hao watapewa nyumba mpya na zenye samani ili wasipate shida ya kutafuta mahali pa kuishi wakati wa kazi,” alisema.Alisema Serikali itahakikisha Tume hiyo inafanya kazi katika mazingira ya utulivu na kwa kuanzia, ndiyo maana imeipatia ofisi yenye vifaa vyote vinavyohitajika.Ofisi ya Makamishna hao itapewa ulinzi wa polisi, mawasiliano ya simu, vifaa vya kutunzia kumbukumbu na tovuti.Sherehe hizo ziliingia dosari baada ya umeme kukatika hivyo kusababisha ratiba ya wajumbe kutembelea ofisi hiyo kuvurugika, Balozi Sefue alizungumzia hali hiyo akisema Serikali itanunua jenereta kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la umeme katika ofisi hiyo.Muungano
Suala la Muungano limeendelea kuichanganya Tume hiyo hasa baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani kurudia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba Tume hiyo haiko kwa ajili ya kuvunja Muungano huku akisisitiza kuwa maoni ya wananchi yaheshimiwe.Akizungumzia kauli hiyo, mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo kutoka Zanzibar, Awadh Ali Said alisema hata kama maneno hayo yalizungumzwa na Rais, siyo kikwazo cha wananchi kukubali au kuukataa Muungano.“Sisi tunakwenda kuwauliza wananchi, wao ndiyo watakaoamua kama wanautaka au hawautaki Muungano. Kama hawautaki tutaleta majibu hayo. Maneno hayo hata kama yamezungumzwa na Rais, siyo sheria, wananchi ndiyo watakaoamua,” alisema Said.
Kuhusu suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi alisema lengo la kuweka msisitizo kwenye Muungano ni kuwaongoza wananchi waamue aina ya Muungano na siyo kuuvunja.“Lengo la kuweka msisitizo huo ni kuwaongoza wananchi waamue Muungano wanaoutaka. Wengine wanataka Serikali moja, wengine serikali mbili, tatu au mambo ya Muungano yamekuwa mengi tupunguze, nia ni kurekebisha siyo kuvunja.” alisema Balozi Sefue na kuongeza:“Kuna mambo yamewekwa katika ile sheria, kama urais, mnataka tuseme tusiwe na rais? Hapana ila tunaweza kusema labda madaraka yake yamekuwa madogo tuongeze… kama hivyo.”
Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar , Abubakar Khamis Bakar aliitaka Tume hiyo kutoa elimu ya Muungano kwa wananchi.“Nakumbuka katika hotuba ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa Julai 6, 1970 akihutubia Bunge alisema; ‘watu wengi hawaujui Muungano. Ila sishtushwi na wageni wasioujua muungano, bali Watanzania wasioujua muungano wetu’… Tume mna kazi kubwa ya kuwaelimisha Watanzania kuhusu muungano wetu,” alisema Bakar.Jaji Warioba Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba aliahidi kwamba watatumia uwezo wao wote kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata fursa ya kutoa maoni yao.
“Tutatumia uwezo wetu wote kutekeleza yote ambayo Watanzania wanayataka. Tunakwenda kwa Watanzania watuambie wanataka Tanzania ya aina gani,” alisema Jaji Warioba na kuongeza:
“Mmetupa kazi ya kusuka Katiba, wananchi watakuwa na hoja zao, watataka kujua uzuri wa Katiba ya sasa na upungufu wake. Hayo yatasaidia Watanzania kuifahamu zaidi Katiba.”
mwananchi

UFISADI TU ATI WANUNULIWE MAGARI NA NYUMBA MPYA SHENZIII TAIPU WANANCHI WANAKUFA KWA HALI NGUMU MAISHA WAO NDIO KWA NYUMBA NA MAGARI ATI WAELIMISHE WATU KUHUSU MUUNGANO WETU MIAKA 48 HAMUJAWAELIMISHA WATU MPAKA SASA WANADAI HAKI YAO NDIO WAELIMISHENI MBWA NYIE AMAKWELI HAKUNA CHA KUELIMISHANA WALA KATIBA NA KAMA HAMUTAKI KUTOKA KWA KHEYARI MUTATOKA KWA NGUVU GADDAFI YUKO WAPI..?

No comments:

Post a Comment