Tuesday, May 29, 2012

YANAYOJIRI MSIKITI WA MBUYUNI HIVI LEO HII 29/05/2012.KWA 1.18 UM

 1. zenj 29/05/2012 kwa 1:18 um ·
  Salma Said: Nipo katika msikiti wa Mbuyuni na tayari waumini wameshakusanyika katika msikiti huo na tayari viongozi wa Uamsho akiwemo Sheikh Farid Hadi Ahmed na Sheikh Mussa Juma wameshafika katika msikiti huu na watu wengi wamehudhuria katika sala ya laasiri na matarajio baada ya kumaliza wataanza mhadhara wao kwa mujibu wa ratiba. na huku jeshi la polisi limeweka ulinzi wake kwa kupitapita na magari yao pembezoni mwa msikiti huu kwa upande wa uwanja wa Malindi. hatujui nini kitatokea salma inshallah
 2. zenj 29/05/2012 kwa 1:21 um ·
  Salma Said: watu wanaingia kwa wingi sana
 3. zenj 29/05/2012 kwa 1:22 um ·
  Salma Said: Watu wameshamaliza kusali na sasa wanafanya mhadhara hapa hapa msikitini
 4. zenj 29/05/2012 kwa 1:23 um ·
  Salma Said: Amir Haji Khamis, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi mbali mbali wa tasisi za kidini
 5. zamko 29/05/2012 kwa 1:36 um ·
  @Salima
  ahsante sana kwa habari. naomba tutuilishe zaidi kitakachoendelea.
 6. Rocket 29/05/2012 kwa 1:37 um ·
  Musisahahu kututumia VIDEO haraka baada ya muhadhara.
 7. zenj 29/05/2012 kwa 2:21 um ·
  Salma Said: MC Sheikh Fikirini anaongea kutoa maelezo na baadae ataongea sheikh suleiman haji na kisha kupewa fursa sheikh mussa juma na baadae sheikh fard hadi kumalizia mhadhara huu
  Salma Said: anaongea Sheikh Suleiman Haji
  Salma Said: Sheikh Mzee Suleiman anasema kuna chama kimoja kinasema kwamba sisi tunachochewa na vyam alakini sio kweli sisi hatutuwmi na chama tunatumwa na nafasi zetu na dini yetu, msikubali kuymbishwa sisi tuna uwezo wetu wa kufanya kazi kwa ajili ya Allah na tunasema hakuna kitakachobadilika tumeshasema hakuna jeshi hakuna polisi hakuna lolote inshallah tunaomba tawfik na msimamo wetu ule ule hatusikii lolote mpaka kieleweke.
  Salma Said: Sheikh Suleiman Haji hapa kunapigwa takbir nyingi sana
  Salma Said: Sheikh Suleiman Bin Haji anasema nyumba mbovu haipakwi rangi, kila mmoja atumie akili yake vizuri asitawaliwe na jazba asiawaliwe na siasa, wazanzibari tunakupongezeni sana kwa haya yanayotokea siku tatu tupo tupu ndani,
  Salma Said: Sheikh Suleiman Haji anasema jeshi la polisi lilizowea kuingia katika unyanyasaji wa raia, nakumbuka wakati wa wanasiasa, kuna siku niliwaambia wakuu wa polisi kwamba sheikh Mussa ameshakamatwa basi kila ninayemwambia kwamba huku mambo yameshaharibika hakusikia
  Salma Said: Natoa pongezi kwa wazanzibari, mtihani waliopata
  Salma Said: wanataka kuibinya zanzibar lakini nawambia kuwa msikubali kudhulumiwa hata mara moja hata mkitiwa ndani msikubali msikubali
  Salma Said: mwenyeenzi mungu habadilishi mpaka pale wanapojibadilisha wenyewe
  Salma Said: tunachodai ni nchi yetuna hatukubali mpaka dakika za mwisho, kitendo kutufanya sisi kama ni wala unga hatukubali hata siku moja tena ninasema kitendo hichi hakikubaliki nilisema mtu atakayenipiga nikatoa kisu nitamtoa utumbo haikubaliki mpigwe na nyie mkae hivyo hivyo, Nabii Mussa alinyonyonyesha na akamtia katika sanduku
  Salma Said: Sheikh Suleiman Haji tumefurahi sana hata kama tunakubali tukamatwe, tushasema atakayetuharibia tutakwenda nao, mkipigwa mabomu basi msikubali kama ni gari choma moto asiyekugusa msimguse lakini anayekugusa nenda naye sambamba
  Salma Said: Sheikh Mussa Juma, tuachie tupumue anaongea …ameanza kuongea anaanza na shukrani
  Salma Said: misimamo wtu ipo pale pale na kukamatwa kwangu ni sawa na kupewa shahada maana nilikuwa chuoni na sasa nimeshakabidhiwa shahada yangu, tutadai haki yetu mpaka mwisho wa kudai tunataka uhuru wa kutoa maoni kwa watu na ndio katiba yetu inavyotufundisha
  Salma Said sisi tunamadai yetu, tunataka kukusanyika na kuzungumza kwa sababu tumezuwiwa tunataka uhuru w akukusanyika kama inavyosema katiba yetu na uhuru wa kutoa maoni yetu kila mmoja awe na uhuru wake wa kutoa maoni yake
  Salma Said: sisi tuna nguvu moja ambayo wao hawaiwezi hakuna mwenye uwezo ni Allah tu ndio tunayemtegemea peke yake
  Salma Said: watu wapo wengi sana hapa
  Salma Said: tumeshasema
  Salma Said: Nilisema tunadai chetu na tumeshasema kwamba haiwezekani kwa hapa imani imeturuhusu tunaendelea kudai ni mtandio tu ukichukuliwa hatukubali
  Salma Said: hebu twambieni leo hii tunambaka mselem au farid itafahamika hapa……wanasema hapakaliki? hivi nilipokuwa najaribiwa tu kidogo wanakuhoji kama wanakulazimisha vile
  Salma Said: hapa tunadai chetu kwa hivyo hatusikii lolote, na tunasema kwamba tumeshajitolea mimi nimeshaaga kwa wazee wangu na wake zangu, maana kule jela walikuwa wakinipeleka kule wanapotaka kama kunishurutisha mimi nikawaambia siko huko lakini walikuwa wanajifanya,
  Salma Said: wanasema wanataka kusema kuileta ile issue ya uislamu ili watunasibishwe na alkaida
  Salma Said: Shekh Mussa Juma anasema baada ya kuwekwa ndani wakati akihojiiwa alikuwa akilazimishwa kusema wanayoyataka wao
  Salma Said: akitoa mfano heshima za kulina zanzibar katika uislamu
  Salma Said: hata wakati wa Mtume alimgonga kafiri mmoja wakati akimgusa mtume, wazanzibari wanawatukana viongozi na wana kashfa kubwa hawafanyiw chochoe lakini sisi hatukubali kwa sababu huu ni mwanzo na mwisho kuwaachia wakatukamata
  Salma Said: watu wameshachoka hata wafungwa, maana wafungwa wanasema sisi tunataka viongozi wa uamsho tu maana tumeshachoka
  Salma Said: Sheikh Mussa anasema wafungwa wanauliza kwa nini huko chini ndio tukawaambia kwamba huko nje kuna watu wamekamatwa basi wananchi wamekasirika sana kukamatiwa kiongozi wao kwa hivyo wale wala unga waliokuwa wamefungwa wamekasirishwa nao kutokana na hilo, tunasema tena sio kama tunawatisha serikali lakini tunasema tunahitaji kusikilizwa
  Salma Said: anasema sisi tunataka kuwaambia ili yasitokee yale basi tunawaambia wafate taratibu wakati wa kuwakamata viongozi wa dini na sio kuwachukua kama wahuni kwa sababu watu wameshachoka, leo hii mnakuja kunichukua tu hamjanambia lolote nipeni simu niwaambie jamaa zangu na masheikh wangu wamekataa wao wamenichukua tu jee mimi ningejitoa pale na nikawanadia wezi jee ingekuwaje
  Salma Said: Sheikh Mussa anasema ugomvu unakuwa mkubwa inapotokea mambo kama hayo waumini hawataki kungilia katika imani zao, kweli zanzibar kuna haja ya kuletwa helikopta au kifaru? sisi mahodari sana tukiitwa tu ssi tunasema tunakwena kuwaambia kwamba watulie na waitunze amani
  Salma Said: Sheikh Mussa anasema kuna watu wanahatarisha amani kuvunja baaa au kwenda katika makanisa muwaepuke lakini sio hawa, sisi tunaripua mabaa na tuna komandoo wetu ambaye anarpua mabaa lakini anayaripua kisheria
  Salma Said: Muislamu akipata misukosuko ndio anazidi imani kwa hivyo sisi tunaata msukosuko kutokana na imani zetu na haturudi nyuma kwa sababu ssi ni waislamu safi na hatutaki kuvunja sheria lakini tunahitaji uhuru wetu
  Salma Said: serikali au polisi wasituchagulie lugha za kusema maana wanatwambia sisi kazi yetu kusema takbir ndio, sasa tumekuja hapa kukumbushana kwa njia za kiislamu huna utakalolifanya waislamu wasizungumze kumtaja mola wetu kwa sababu yeye ndio atakayetupa nguvu, jambo la msingi ni umoja na hilo ndio muhimu, kura ya maoni ndio tunayoitaka Zanzibar
 8. zenj 29/05/2012 kwa 2:26 um ·
  Salma Said: Sheikh Farid Hadi Ahmed anaongea nani mwneye hatia, kwa sababu kama ni suala la kutukana kachorora wanatukana kila siku wanawatukana viongozi kwa kuwatukana wakisema wapemba wende kwao jee Dk Shein ni nani? Makamu wa kwanza ni nani? hao ndio wanaostahiki kukamatwa
  Salma Said: wazanzibari wanahitaji nchi yao na sio mambo mengine na hilo nataka lijulikane
 9. zenj 29/05/2012 kwa 2:33 um ·
  Salma Said: kama ni maandamano ya amani tumeshayaomba sana hatupewi lakini tunasema kwamba tunataka maandamano tarehe 26 tunataka maandamano tunakuomba wewe IGP maana kamishna wewe huna uwezo, sisi tunawaomba jeshi tunataka litulinde bila ya kuwa na kuwa na silaha
 10. zenj 29/05/2012 kwa 3:10 um ·
  Salma Said: ssi tunaambiwa kwamba sisi tunachoma makanisa lakini wapo wenye kufanya mambo hayo hebu chukuweni hayo mahubiri yao wanaofanya mikutano waambie wakupe CD zao halafu tusikilize CD zetu mtasikia mambo hayo
  Salma Said: Sisi tunalaani vikali kuchomwa kwa makanisa kwa sababu hilo sio suala letu na hilo ni kosa, kwa hivyo IGP tunakuomba tafuta CD usikilize nakuomba sana
  Salma Said: jeshi la polisi wanakuja kuvunja milango ya watu, hivi kwnai sisi sio binaadamu hatudhuriki? defender zimekuja kurandaranda
  Salma Said: haya jeshi la polisi tunaambiwa wamekuja kupiga mabomu wamevunja na inaonesha ndio hao hao wamekuja kupiga mabomu makanisani ili wanataka kuonesha sisi ndio tumevunja
  Salma Said: sisi waislamu hatuwezi kufanya chuki kwa sababu mtume mwenyewe ameishi na wasio na waislamu
  Salma Said: Jeshi la polisi wamepiga risasi za moto msifanye maskhara, sisi tuna mtandao wa kupeleka taarifa kila pahala hapo hapo matembezi yanafanyika basi hapo hapo kila kitu kimeshakwenda kwa wallahi utakwena mahakama ya kimataifa
  Salma Said: Sheikh Farid anasema, tuliwakataza waumini wasiharibu mali zetu lakini leo hii tunaambiwa sisi ndio tulioharibu mali za raia,
  Salma Said: leo hii serikali inatembeza vifaru kwa jili gani? leo hii mnatembeza majeshi kwa ajili ya nini?
  Salma Said: ndugu waislamu nakuombeni wazanzibari wote, hapa jeshi la polisi tuliambiwa kuna utaratibu wa jeshi jamii nasema watu wakeshe maeneo yote penye kusaliwa fardhi isaliwe faradhi na penye kusaliwa sunna basi pasaliwe sunna
  Salma Said: Mheshimiwa IGP sisi madai yetu ni hatutaki muungano madai yetu ssi tunataka zanzibar yetu, lakini njia ipo ya kura ya maoni lakini waheshimiwa serikali wametia pamba, kwani kuna dhamibi gani kuulizwa wazanzibari kama tunataka au hatutaki muungano?
  Salma Said: Tunatoa salamu kwa wawakilishi wetu na tunatoa salamu kwa rais wetu dk shein kwamba wazanzibari wanataka kupewa fursa na heshima yao, tunataka tuwe huru na hilo tunataka uhuru wetu ambao umetajwa katika katiba, sisi tumekuja kwa utaratibu wetu maalumu sisi hatutaki madaraka tunataka tuulizwe tu kama tunataka muungano bas halafu tunawaacha wengine waendelee na uongozi wao hatuna tatizo
  Salma Said: waislamu wanadai haki yao na hatutaki mtu aje kutudaia haki yetu na kwa nini tusisikilizwe?
  Salma Said: Mimi nikikamatwa sina tatizo nikitwa polisi nitakuja na sina tatizo lolote kama nikiitwa polisi na polisi mkifuata taratibu mkitaka nije nitakuja ukinipeleke mahakamani nipelekea kwa heshima kwa adabu, lakini mkija kuleta vurugu wallah huu sio wakati wa kufanyiana vurugu, msije kunikamata kama wanavyomfanyia sheikh mussa juma
  Salma Said: MImi nilichukulia kwa pindu na kutupwa tu kwenye rova na nikatupwa paje nikapelekwa sehemu ambayo huwezi kuijua na jeshi la polisi wakanipiga mikwaju mpaka wakachoka lakini kwa sasa hivi tufanyiane hayo wallahi nasema roho mbichi zitatoka wallahi kama wanangu wakikaa mayatima na nyinyi watoto wenu watakaa mayatima
  Salma Said: hatukubali hata siku moja tuchitakini tutakuja huko lakini na sisi tuna kesi zetu tunazo zimekuandameni hizo hatusameheee…..watu wanajibu hawasamehewiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii…tusiwasameheeeeeeeeeeeeeeeeeee
  Salma Said: sheikh farid hadi ahmed ansema kuna msemo waadui wangu vipi watanifanya ..wakinitia jela basi wananipa faraja maana mimi nilipotiwa jela ….wallahi nimepata faraja wakati mimi nimeshapigwa kinyama basi nikakumbuka hii aya isemayo usidhanie kwamba mwenyeenzi mungu ameghafirika kwa hayo wanayoyatenda madhalimu ije siku ya kiama na huko watakuja madhalimu macho yamew0akodoka….
  Salma Said: ikiwa Mandela alikuwa ndani na alipotoka akapata alichokitaka au hajakipata? msidanganywe kuwa litakuja jeshi hapa ipo haja ya ya kuwa kitu kimoja, nasema tuwe kama jeshi la misri walipooa rais na serikali wamevutana wao wakaingia kat lakini hawajatmia nguvu kwa sababu kwa nini itumie nguvu?
  Salma Said: jeshi likija kuvamia hapa basi ndio mapindui hayo, sisi tunasema tunataka hati ya muungano na hilo tunakuomba wewe IGP
  Salma Said: jumuiya za kiislamu zimekutana zotena zimetengeneza kamati na viongozi walioteuliwa humo watatu, katika kamati hiyo ni Amir Msellem
  Salma Said: mihadhara bado inaendelea kama kawaida na na tunasema kwa kutumia katiba hatusimamishi katu kudai haki zetu, tunaanya kwa hiari na tutaacha kwa hiari, jumapili tutafanya lumumba
  Salma Said: mhadhara utafanyika saa 10 jioni siku ya jumapili na tumeshasema na tarehe ya 26 tunataka maandamano na tunaahidi yatakuwa yametulia na wala hatufanyi fujo,
  Salma Said: hapa watu wanaomba dua maana mkutano umeshakwisha. jeshi la polisi tunawaomba wasidhani kama wanadamana na tunakuombeni mkiondoka hapa muondoke kwa usalama bila ya matatizo
  Salma Said: mhadhara utafanyika saa 10 jioni siku ya jumapili na tumeshasema na tarehe ya 26 tunataka maandamano na tunaahidi yatakuwa yametulia na wala hatufanyi fujo,
  Salma Said: taasisi za kiislamu Amir Msellem, na mimi ndio naibu amir na ndio msemaji wakinikabidhi mimi basi huku nje hakuna msemaji sawa ehhh

No comments:

Post a Comment