Friday, May 4, 2012

ZANZIBAR NA TANGANYIKA IRUDI KAMA ILIVYOKUWA KABLA YA APRILI 26,1964 TUSIMUOGOPE KARUME WALA NYERERE WOTE WASHAKUFA NA HATA KAMA WANGELIKUWA HAI

9903
NYERERE KASEMA KAMA WAZANZIBARI WENYEWE BILA YA MTU YOYOTE WA NJE KUCHOCHEYA KUUVUNJA MUUNGANO BASI SITAWALAZIMISHA WALA SITAWAPIGA MABOMU WATABAKI NA NCHI YAO NASI TUTABAKI NA TANGANYIKA YETU JE KIKWETE HAYA HUYATAKI UNATAKA KUWAPIGA MABOMU WAZANZIBAR KWA KUUKATA MUUNGANO FEKI...?SI UNAJITA RAISI MWENYE DIMOKRASI WEWE MBONA HUTAKI KUWAPA NCHI YAO ZANZIBAR..?
WIKI iliyopita muungano wa Jamhuri  feki isiyotakiwa na wazanzibar ya Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) ilitimiza miaka 48 tangu Aprili 26, 1964 ambapo zaidi ya robo tatu ya watu wa nchi hizi mbili walikuwa hawajazaliwa.Muungano huo umekuwa na matatizo kibao ambayo mzizi wake ni kutokuwepo aina ya muungano utakaokubalika pande zote,hususan Zanzibar watu hawajuwi kabisa muungano huu ni wa vipi au vipi watu wanaona ubabe tu na guvu za jeshi na polisi ukija bara yani Tanganyika kuna wanaotaka serikali moja yani Zanzibar imezwe kabisa kuwe hakuna tena z,bar, kuna wanaotaka serikali mbili na kuna wanaotaka serikali tatu bara huko nchini Tanganyika na ukija kwa Wazanzibar wengi wameonyesha kutaka serikali yao ya JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR IRUDISHWE KAMA ILIVYO KUWA HAPO AWALI KABLA YA KUNGANA NA TANGANYIKA KWA LUGHA YA SASA TUNASEMA KUMEZWA NA WATANGANYIKA, wakati viongozi wa Bara wamekuwa waking’ang’ania mfumo wa sasa wa serikali mbili kueleke moja na huu ndio mpango maalum toka hapo awali wakati wa nyerere kuwa ni serekali mbili kuelekea moja.Watu wenye busara wanatambua kwamba kuna Wazanzibar ambao hawautaki muungano huu katika hali yoyote, na pia kuna Watanganyika ambao pia wanataka muungano huu udumishwe katika sura yoyote ile ya amani au hata kutumiya guvu za jeshi kuwanyamazisha Wazanzibar kudai nchi yao haki yao.Hiyo ndiyo hali halisi,na kwa wazanzibar wanao penda amani sio vita washasema tuitishe kura ya maoni kwani hakuna mtu aliyewahi kuwahesabu watu wasioutaka muungano huu, wala kuwahesabu wanaoutaka muungano huu.Na hapo nchi hizi mbili zilipounganishwa Wazanzibar hawakuulizwa na hata hao Watanganyika pia hawakuulizwa walijiona wanaunganishwa tu basi.ila sasa kuna Watu pekee wanaofahamika wazi kuutetea muungano huu ni viongozi walioko madarakani nchini Tanganyika na wanafiki waliokuweko madarakani ktk serekali ya kuendeshwa kikoloni kutoka mkono wa chuma Tanaganyika mpaka Visiwani Zanzibar. Huutetea muungano huo kwa sababu wanazozijua wao!haswa za kujirudikia mali na kujijengea majumba ya kifahari na magari ya kila aina na kuwawacha wananchi wakiumiya na njaa kali na maradhi ya kila aina bila ya kuwa na madawa hospitalini wala ajira.Ikumbukwe kwamba muungano huu unaohusisha watu wapatao milioni 42 kutoka ktk nchi ya Tanganyika na milioni moja tu wa serekali ya Zanzibar. Kwa miaka yote muungano huu miaka 48 hakuna faida yoyote nchini Zanzibar umeifanya zanzibar kuwa masikini hahehohe na  woga zaidi nikumezwa nchi yao na ndiyo maana katika muda wote huo imepigana hadi kupata wimbo wake wa taifa, bendera yake, katiba yake na kadhalika.Wazanzibar bado wanapigania uanachama Umoja wa Mataifa (UN),ambao walikuwa nao toka 1963 ila mpaka leo haijulikani ilitoeka vipi na nani aliyetutowa ktk( UN) Pia Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), Jumuia ya Kimataifa ya Waislam (IOC), Shirikisho la Soka Afrika (Caf), na kadhalika.Kwa nini wanafanya hivyo? Wanataka utambulisho wa Zanzibar na historia yake viendelee duniani.Si hivyo tu, limejitokeza suala la mafuta kuwemo eneo la baharini Zanzibar ambayo Wazanzibar Wanajua ni mali yao ila Tanganyika imekuwa kinganganizi toka ijuwe zanzibar ina mafuta wakati wote huwo Tanagnyika ina gesi asili,maka ya mawe,thahabu,almasi,buga za wanyama na ardhi kubwa kabisa na vyote hivi wanavitumiya na wala hawajawahi kusema ni vya muungano na vyote vinawaingizia mabillioni kwa mabillioni ya dola. Pia kuna tatizo la rais wao kutokuwa na madaraka katika serikali ya muungano na kutokuwa makamu wa jamhuri ya muungano na hivyo ndiovyo walivyokubaliyana vingozi wa nchi hizi mbili wakati huo mzee karume na mzee kifimbo cheza nyerere.sasa imekwenda kwenda vipi mpaka raisi wa Zanzibar mwaka huu akavuliwa hayo madaraka ndio Wazanzibari wakazidi kuamka kuwa weee tunapelekwa kutoka serekali mbili kuelekea moja na hio sio haki. Hata nchi za ulaya zimeungana ila hujasikia hata siku moja waziri kiongozi wa nchi hii na raisi wa nchi ile kuvuwana madaraka ni hapa tu.Yote hayo na mengine, hayajapewa utatuzi, watawala wakiamini kwamba watu watayasahau.Mambo hayo hayasahauliki!Mwaka 1985, bunge la Tanganyika dodoma chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lilipitisha azimio la kuanzishwa kwa muungano wa serikali tatu, lakini Mwalimu Julius Nyerere alikuja na sababu zake na kulizima azimio hilo!Kwa heshima na woga waliokuwa nao kwa Nyerere, wabunge wakanyamaza!Ndivyo Watanganyika walivyokuwa. Kuzungumzia muungano ulivyokuwa, hasa enzi za Nyerere, lilikuwa kosa la jinai. Hivyo watu waliendelea kukaa kimya si kwa kuupenda sana muungano, bali kwa kuogopa kuukosoa wasije wakawaudhi watawala!au hata kupoteza maisha kabisa na hata mwili wako isipatikane tena hivyo ndivyo hali ilivyo kuwa.Hivi leo, Wazanzibar, hususani vijana, wanaamini sababu zilizounda muungano mwaka 1964 leo hii hazipo tena, hivyo wanataka Zanzibar iendelee na historia na utamaduni wake bila kuihusisha Tanganyika.Hali hii ni tofauti na kauli za watawala wanaotaka kuzima hisia hizo kwa visingizio kwamba “muungano ni tunu kutoka kwa Mungu” na hivyo usijadiliwe katika mchakato wa kupata katiba mpya.na ukisema kujadiliwe katiba unamanisha katiba ipi maana Zanzibar wana katiba yao na kama ni ya Tanganyika basi haina haja ya kujadiliwa na watu wa Zanzibar ijadiliwe na Watanganyika wenyewe katiba ni yao sio ya Wazanzibar ila kama unampango wa kufanya kuwe na serekali moja na kuimeza Zanzibar kabisa kabisa basi sawa tutakuelewa kuwa sasa katiba ya Zanzibar itiwe kapuni kisha watu wote wa serekali ya zanzibar na ya Tanganyika wajadili katiba hii na kuanzia sasa hakuna tena katiba ya Zanzibar wala bendera wala nyimbo ya taifa wala raisi wa Zanzibar na makamo zake laa sio hivyo basi hii katiba si katiba ni jini linalotaka kuanzisha umwagaji damu baina ya nchi hizi mbili ya Zanzibar na Tanganyika.Pia napenda kuwakumbusha kuwa Muungano huu haukutoka kwa Mungu. Ulianzishwa hapa hapa duniani na Nyerere na Karume, ‘full stop’!
Ifahamike wazi kwamba muungano ni kitu cha hiari, si cha kulazimisha au kulazimishwa au kulazimishana.
Hilo liko wazi kwa watu wenye busara na hikma.Mwalimu Nyerere na Karume hawakuwa malaika kwamba walichokipitisha hakijadiliwi. Vilevile, muungano si Biblia wala Koran, vitu ambavyo havihojiwi na waumini wake kuhusu uhalali wake.Wakati wa kuamua hatima ya muungano huu ni sasa.Bara yani serekali ya Tanganyika wajadili katiba yao na wasikilizwe na Wazanzibar kama wanataka nchi yao wapewe bila kujali kauli za wanasiasa ambao hujifanya wana busara zote mikononi mwao wakati wao ndio wanaofurahia mabaya yanayowakuba wananchi hivi sasa.Wazanzibar ambao wamekuwa wakiulalamikia zaidi muungano huu kuliko Watanganyika, wapewe fursa ya kuulizwa iwapo wanautaka au laa.Kama wanautaka waseme uwe wa aina gani, na kama wanaukataa hakuna haja ya kuendelea na muungano usiotakiwa upande mmoja.
Muungano uvunjike na maisha yaendelee kama yalivyokuwa kabla ya Aprili 26, 1964.
Mbona majirani zetu wa Kenya,Uganda,Malawi, Zambia, Msumbiji,Burundi,rwanda na kadhalika tunaishi nao kwa kuheshimiana na kupendana wakati hatuna muungano nao...????????????????????????
Muungano ni kitu chema, lakini kisilazimishwe kwa ajili ya kumwogopa marehemu Nyerere na Karume!

No comments:

Post a Comment