Saturday, June 2, 2012

JESHI LA POLISI LA KIKURIA NA VIJIBARAKA WAO LASITISHA UAMSHO NCHINI ZANZIBAR NA UAMSHO WASISITIZA MHADHARA UTAKUWEPO NANI ATASHINDA WATU WA M/MUNGU AU MASHETWANI YA KIKURIA..?


Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
JESHI la Polisi Zanzibar limepiga marufuku maandamano na mihadhara ya aina yoyote visiwani hapa hadi hapo itakapotangazwa tena.
Taarifa ya Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, imesema kuwa hatua hiyo inatokana na agizo la Serikali la kusitisha shughuli zote za mikusanyiko ya vikundi vya kidini vikiwemo vile vyenye usajili na ambavyo havina ili kuepusha uvunjifu wa amani.
Akisisitiza msimamo huo wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema Jeshi la Polisi litachukua hatua kali kwa mtu ama kikundi chochote kitakachokaidi agizo hilo kwa lengo la kudumisha amani na usalamawa viisiwa hivyo.
Kamishna Mussa amesema Jeshi la Polisi limelazimika kutoa msisitizo huo kufuatia taarifa za viongozi wa kikundi cha Uamsho kuwatangazia wananchi kuwa kesho wangefanya mhadhara kwenye viwanja vya Lumumba kinyume na maagizo ya Serikali.
Amewataka Wananchi wakiwemo waumini wa dini zote kutojitokeza kushiriki mhadhara huo na mihadhara mingine itakayotangazwa katika kipindi hiki cha marufuku ya mikusanyiko ya aina hiyo.


Jana akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar, Kiongozi wa Kikundi cha Uamsho Sheikhe Farid Hadi, alisema wangefanya mhadhara mkubwa hiyo kesho jioni na kufanya maandamano Jumanne ya Juni 26, mwaka huu.
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU (JUMIKI) للجنة الدعوة الإسلامية THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com MKUNAZINI ZANZIBAR
Afisi ya Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mjini/Magharibi, Sanduku la Posts 237 Zanzibar. KUH:
KUZUILIWA KUFANYA MHADHARA WA AMANI KATIKA VIWANJA VYA LUMUMBA NA JESHI LAKO LA POLISI
Tafadhali rejea barua yako yenye kumb:RPHQ/MJN/58/VOL.V/59 ya tarekh 01, JUNE, 2012 ambayo ina kichwa cha maneno kuhusu Taarifa ya Mhadhara.
Jumuiya yangu imesikitishwa saana na hatua yako pamoja na Jeshi lako la Polisi ya kutuzuilia kufanya mhadhara wa amani ambao kwa mujibu wa Sheria za nchi ni haki yetu na imeonelea ikuandikie barua hii kwa kuwa sababu ulizozitoa za kuzuiya mhadhara huo si za msingi wala si za kisheria.
Baada ya kukaa pamoja na kujadili hoja ulizozitoa na zilizopelekea jeshi lako kutuzuilia kufanya mhadhara huo wa amani tumeonelea kukuomba wewe pamoja na jeshi lako la Polisi kuyazingatia mambo yafuatayo na tunaomba majibu rasmi juu ya hayo-:
(a). Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari pamoja na magazeti ya ndani ya nchi, aliyetoa amri ya kuzuiya kufanyika mihadhara, makongamano, maandamano pamoja na mikusanyiko ya aina yoyote ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi ndugu Mohammed Aboud ambaye kisheria hana nguvu juu ya hilo.
(b). Kauli iliyotolewa na Mheshimiwa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh Doctor Ali Mohd Sheini kwa waandishi wa habari siku ya tarekhe 31/05/2012 ikulu mjini Zanzibar haikusimama katika kuzuiya Mihadhara, Makongamano wala Mikusanyiko ya aina yoyote bali ilisimama katika kulinda na kudumusha amani, tunampongeza Mh Raisi kwa hilo na hilo kwa kuwa amelitambua wazi ndilo lengo pamoja na dhamira ya Jumuiya yetu.
(c). Barua yako uliyoitowa kwa Jumuiya yangu ya tarekh 01/06/2012 haisimami kunizuiliya kufanya na kuendelea na shughuli zangu za Mihadhara, Makongamano bali imesimama zaidi kunipa taaarifa juu ya Kauli ya Serikali ambayo kama nilivyokuelezea hapo juu imetolewa na mtu ambaye Kisheria hana nguvu za kufanya hivyo.
Kwa mantiki ya hoja nilizokuelezea hapo juu inaonekana wazi kuwa Jeshi lako la Polisi limeazimia kufanya uvunjifu wa amani pamoja na kufanya mauwaji kwa raia wasio na hatia, hii inatokana na kauli ya Jeshi lako katika barua uliyoniandikia ya kuwa jeshi lipo tayari kuzuiya kwa nguvu za aina zote mhadhara huo.
Napenda kukufahamisha kuwa kufanya mihadhara, makongamano pamoja na Maandamano ya Amani katika nchi yoyote ile inayofuata Demokrasia ya kweli ni kutii sheria na sio kuvunja sheria kama haya yanathibitishwa katika Katiba zote, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar, tafadhali rejea ibara ya 18 (a,b,c,d) na pia rejea ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia ibara ya 18(1) na 20(1).
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, Jumuiya yangu bado inayofursa ya kufanya Mihadhara pamoja na shughuli zake kwa kufuata Katiba ya nchi na kufuata katiba ya Jumuiya iliyoitunga, hii ni kwa sababu mpaka sasa haina ushahidi wowote wa Kimaandishi juu ya kuzuiliwa kufanya shughuli zake.
Kwa kuwa Jumuiya yangu ni Jumuiya yenye lengo la kukuza na kudumisha amani katika nchi, viongozi wa Jumuiya wapo tayari kukaa chini pamoja na viongozi wakuu wa Jeshi lako la Polisi kulijadili suala hili na kulipatia ufumbuzi kabla ya madhara makubwa ya umwagaji wa damu ambayo yameazimiwa kufanywa na Jeshi lako la Polisi yasije kutokea.
Kumbuka ni wajibu wa Jeshi la Polisi wanatakiwa wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu.
Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu. Polisi wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.
Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.
WABILLLAH TAWFIQ
Natanguliza Shukrani …………………………
ABDALLAH SAID ALI. KATIBU MKUU. JUMIKI.
Nakala: MUFTI MKUU ZANZIBAR
IGP – Tanzania CP – Zanzibar
RPC – Mjini Magharibi RCO – Mjini Magharibi
OC FFU Mjini Magharibi RSO – Mjini Magharibi
DC – Mjini Unguja. DSO – Mjini Unguja.
Balozi mdogo wa Marekani Nchini Zanzibar

No comments:

Post a Comment