Saturday, June 16, 2012

KINIMACHO NA CHANGA LA WATANGANYIKA KUWAMALIZA WAZANZIBARI KWA KATIBA MPYA

Unajua kama utafuatilia sana suala zima la Muungano (ukiachilia ule mkataba halisi wa 1964), mazonge yamekuwa mengi, udanganyifu, ujanja na hadaa zinazofanywa na Tanganyika zinachupa viwango – yaani Tanganyika wameilalia sana Zanzibar – wameidhulumu kwa kila hali.
Mtakumbuka kuwa mwaka 1992/93 ulipoanzishwa mfumo wa vyama vingi TZ, ilipitishwa sheria maarufu Bungeni inaitwa ‘Mabadiliko ya 11 ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa TZ”,(tanganyika) mabadiliko haya – Ibara ya 11, ndio yalimuondeshea Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais TZ (na kuvunja mkataba wa Muungano wa 1964). Dhulma na ujanja huo.
Hii haikuletwa BLW wala BLM wala popote pale Zanzibar – Zanzibar kuweza kuijadili na kuipta ridhaa, na hata Wabunge wa Zanzibar wakati ule pia hawakuipigia kura maana walitoka nje na kususa kikao. Spika wa siku zile, Msekwa alisema kwa dharau kuwa ‘ni kweli wabunge wa Zanzibar hawakuipa ridhaa mabadiliko ya ibara hii ya 11 kwa sababu walikwenda kusali’. Mnaona dharau hiyo?
Hii ya jana na juzi, Mabadiliko ya 8 -2012 ya Katiba eti inaletwa BLW kama ‘taarifa’ – hii kali na inaonyesha kini macho cha hali ya juu kwa Tanganyika v.s Zanzibar. Mimi hii sijawahi kuisikia popote duniani kuwa bill /au sheria inaletwa Bungeni/BLW kama ‘tarifaa’ – dharau ya mwisho!
Kama nilivyosema ‘bad start or wrong approach haiwezi kuleta good results’.
Msimamo wa Tanganyika ni kuwa Zanzibar si chochote si lolote; lakini wao wanaitumilia sana Zanzibar kwa kupata tija halisi hasa kipato na kuijenga nchi yao na kuiwacha nchi yetu ikidorora.
Mfano, ilipovunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki 1977, Edwin Mtei alikuwa Ganava wa Benki Kuu ya TZ;(tanganyika) siku zile EAC ilitoa mgao wa pesa kwa Zanzibar tu, ambazo ndizo zilizoanzisha BoT. Msekwa aliandika barua kwa EAC na kudai pesa za ziada na sehemu ya barua yake ilisomeka hivi (roughly) kuwa “….sisi ni nchi mbili tofauti, na mgao mliotupa ni kidogo sana kwa nchi mbili kwa hivyo tunaomba sehemu mgao wa Tanganyika kama nchi…..”. Naam, EAC walitoa kasma nyengine kwa ajili yao. Haya leo ni nchi ‘moja’; yakiwepo maslahi – zinakuwa nchi mbili? Kiini macho hicho.
[naomba mtembelee archive ya Nairobi, Kenya mtaziona na hata katika report ya tume ya Amina Salim Ali ameziweka kama appendix/annex]. Hii report SMZ wameificha maana imefuchua mambo mengi mazito juu ya Muungano hasa kuhusu pesa.
Msekwa yupo hai, na Edwin Mtei yupo hai – waulizwe kama ni kweli au uwongo, record za barua zipo na record za malipo zipo (unless wazichakachue leo na kesho). JK upo?
Sasa, tunapodai haki zetu za msingi – iwe UAMSHO au Jumbe, au Maalim Seif na timu yake (enzi zile, sio leo tena), au Kamandoo Salmin au yeyote yule – inakuwa NOMA. WHY WHY WHY kikwete..?
Tanganyika wajue kuwa tuna madai mengi kwao, na wajue kuwa hizi ni haki zetu za msingi na sio ‘kiini maacho au lele mama au sumsumia’.
BLW limepokea mabadiliko ya katiba kama ‘taarifa’ huo ndio upumbavu wa mwisho kwao na Wazanzibari.
Wallah ingalikuwa tuko serious hawa wote wawakilishi wangalipaswa kujiuzulu na BLW kuvunjwa kama kitu ‘constitutional crisis’ .
Kwa nini basi ile ibara ya 11 iliyomuondoshea rais wa Zanzibar kuwa makamo haikuletwa BLW, kwa nini sheria ya kuanzisha TRA 1998/99 haikuletwa BLW na zinafanya kazi hapa Zanzibar kwa mabavu..?
Hata hivyo, haya yote ni makosa yetu – tumezubaa mno; vipi BLW ikubali upuzi huu, vipi Katibu wa BLW, Mh.Yahya Khamis Hamad — tunayemjua sisi akubali comedy kama hii?
Suluhisho
Kama kweli JK na serikali yake wana dhati ya nchi ya TZ na hasa Zanzibar – basi nakubali kura ya maoni ya watu kulizwa kama WANAUTAKA au HAWAUTAKI au basi bill ile aliyoitia saini irejeshwe AG office DAR ifanyie a small review au mapitio, na iende tena bungeni as an emregency document, bunge waijadili tena – (kidogo tu) na halafu irejeshwe BLW kwa kupata idhini, then aitie saini kama sheria – plus aivunje tume ile fake ya kukusanya maoni aliyoiyunda maana ile sio tume ni majambaza natulishasema mwisho msasani tume ile,au aunde nyengine (kwa sababu hii iliyopo sio halali kabisa, as sheria yenyewe kama ilivyokuwa sio halali).
Wazanzibari wengi wana shaka na uundwaji wa katiba mpya maana haukufuata utaratibu – lakini jana Maalim seif, VP1 amewatoa ‘shaka’ wananchi na kusema kuwa eti ‘tume itafuata kile kitachosemwa na wananchi’wananchi washasema HAWATAKI MUUNGANO wanataka kura ya maoni kusikia husiki basi hata kuona huwoni maalim...?  I doubt Maalim Seif – wewe unawajua vizuri wajomba zako akina Kikwete, Pinda, Msekwa, Mwinyi, Mkapa n.k – hawa kukubali HAKI kwao ni mwisho – ndio wameumbwa hivyo na wameumbika hivyo.
Mimi nitaona ajabu sana kama watachosema Wazanzibari ndicho kitachosikilizwa na kukubalika. I bet! Kwa sbabu watanganyika wameondosha uaminifu kwetu tokea 1964, wao wamechukua nafasi kama ndio wafalme, watawala, mabosi na wakoloni badala ya Mngereza; and not otherwise.

No comments:

Post a Comment