Thursday, June 28, 2012

KISHEIN HAKIOGOPI WAZANZIBARI ANAOGOPA WAKURIA WALIOMUWEKA MADARAKANI!!!!!


WAZANZIBAR MUSIMKASIRIKIA KWA ANACHO SEMA LAZIMA ASEMA HIVI KUWAFURAHISHA WATANGANYIKA SISI UZI ULE ULE TUNATAKA NCHI YETU KAMA WEWE UNATAKA MUUNGANO NENDA BARA NA WEWE PIA USITUCHAFUWE NA KUMBUKA M/MUNGU ANAKUONA NA ATAKULIZA SIKU YA KIYAMA ULIWAOGOZA VIPI WAZANZIBAR UTASEMA NINI NILIRUHUSU UTALI,UNGA (DRUG)MALAYA,POMBE,MISIKITI KUPINGWA MABOMU NA WAUMINI KUPINGWA NA KUVULIWA MASHUNGI WANAWAKE WA KISLAMU HAYO NDIO UTAKAYO MUAMBI MWENYE MUNGU KWA JILI YA KUKA MADARAKANI NA KUWAFURAHISHA MABWANA ZANGU TANGANYIKA WANAO NILINDA HIVYO NDIVYO UTAMUAMBI M/MUNGU SHEIN..?
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema ataendelea kuutetea Muungano na hakuna atakaemlaghai wala kumchezea katika uongozi wake. Kauli hiyo ameitowa jana katika mkutano wa Jumuiya ya Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Bwawani mjini Unguja.
Dk Shein amesema kwamba yeye ndie rais wa Zanzibar na ndie mwenye mamlaka na hatomuogopa mtu wala kusita kuwachukulia hatua kwa wale wote ambao watakwenda kinyume na matakwa ya kikatiba.
Alisema kuwa dhamana ya nchi hii pamoja na ile ya Jamhuri ya Muungano imo mikononi mwao kati yake na Rais Jakaya Kikwete na ndio maana wakawa wanashirikiana na kushauriana kwa yale yote ambayo yana maslahi na nchi.
“katika kuiongoza Zanzibar mimi ndie rais simuogopi mtu yeyote”, alisema kwa kujiamini Dk Shein.
Dk Shein alisema Zanzibar ni nchi ya kidemokrasia inayotoa uhuru wa maoni kwa kila mtu, lakini kwa upande wake pia  yeyé ndio mwenye dhamana kubwa ya  kuendesha nchi kwa mujibu wa katiba iliyopo. “Mimi  ndio rais siogopi mtu katika kuendesha nchi, siko tayari kuirudisha nchi katika misukosuko na kuirejesha Zanzibar kule ilipotoka wakati iko katika hali ya amani hivi sasa,” alisema katika mkutano huo.
Hata hivyo alisema kuwa Muungano upo na utaendelea kuwepo na kwani yeye ndiye rais ambaye anatokana na chama cha mapinduzi na pia ameingia madarakani chini ya ilani ya chama chake hivyo lazima afuate ilani ya chama chake ambapo alisema changamoto zilizomo zinahitaji kujadiliwa ili kuweza kuziondoa na sio kuvunja muungano.
“Hakuna mtu asiyejua kuwa kuna kero za Muungano hivyo ni vizuri tukajitokeza kwa wingi katika kutoa maoni yetu juu ya katiba na sio kukaa pembeni yanazungumzwa mengi kuhusu mimi lakini yote nimeyapokea kwa kuwa ukubwa ni jaa”, alisema Dk Shein bila ya kutaja jina lakini alikuwa akijibu hoja zilizokuwa zimeibuka kuwa hana uwezo wa kuchukua maamuzi magumu katika suala la uongozi.
Aliwaeleza wastaafu hao kwamba Muungano una kero, zinazojadiliwa na ndio maana njia nyingi, ikiwemo ya mawasiliano baina ya Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeanzishwa ili kuzitafutia ufumbuzi ambapo alisema njia hizo zitaendelea kutatua mambo ya muungano.
Aidha Dk Shein alisema kazi hiyo anaifanya kwa umakini ili kuhakikisha kuwa Muungano upo na unazidi kuwepo na kwamba wasioutaka wasubiri tume ikija  ndio watoe maoni yao na sio kuanza kutoa maoni hivi sasa kabla ya wakati hufika.
“Hakuna asiyejua katika Muungano kuna kero,…wananchi wazijadili kupitia tume ya mabadiliko ya katiba, na kwa nini tunaanza kusema sema… subirini tume mkatoe maoni yenu” alisema.
Katika hatua nyengine Dk Shein alisema kwa sababu hiyo anaagiza kutokufanyika kwa maandamano ya aina yoyote kuhusiana na suala hilo na  kuwataka wazanzibari  kutoshiriki hadi pale wanaotaka kufanya hivyo wanaporuhusiwa kuandamana na jeshi la polisi kwa kufuata taratibu za kisheria.
“Naagiza maandamano  yasifanyike,…wakiruhusiwa kufanya basi msiende kushiriki,” alisisitiza Dk Dk Shein alikuwa akizungumza na zaidi ya watu 500, waliohudhuria katika mkutano huo,  ambao ni wastaafu wa taasisi za Muungano waliopo Zanzibar.
Katika waliohudhuria katika mkutano huo ni taasisi mbali mbali pamoja na Bunge, Ulinzi na Uslama,  Mambo ya Nje, Mamlaka ya hali ya hewa (TMA), Mamlaka ya Kodi na mapato (TRA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Idara ya Uhamiaji, Shirika la Posta na Simu, na taasisi za masuala ya elimu na ufundi.
Sambamba na hayo aliwataka vijana kuthami ni jitihada, michango na maelekezo ya wastaafu kwa kutambua kuwa uzoefu wao katika maisha ni sehemu muhimu kwa maendeleo yao.
“Sote hatuna budi kuelewa kuwa iko siku tutakuwa wastaafu hivyo ni muhimu kujitayarisha hasa kwa kujenga tabia ya kujiwekea akiba na matayarisho mengine ya lazima kwa maisha ya wastaafu”, alisema.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa jumuiya hiyo , Mohamed  Ali Maalim, alisema miongoni mwa majukumu ya jumuiya hiyo ni kudumisha Muungano kwa sababhu unalinda maslahi ya wastaafu wote nchini.
Katika risala yao wastaafu hao wamesema kwamba wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ndani ya Jumuiya yao ikiwemo uwezo mdogo wa uendeshaji na usimamizi wa ofisi ikiwemo ukosefu wa ofisi ya kutosheleza mahitaji.
Katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Rashid Ali alitaja changamoto nyengine ni kukosekana kwa wataalamu na waratibu wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya Jumuiya, ukosefu wa vitendea kazi, ukkatika kutekeleza malengo yao.
Jumuiya ya wastaafu Zanzibar imeanzishwa mwaka 2009 ina wanachama 537 ambapo 486 kati ya hao ni wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment