Friday, June 1, 2012

SHEIKH FARID AWAPA UKWELI WANDISHI WA HABARI


Sheikh Farid Hadi Ahmed akizungumza na waandishi wa habari leo nje ya msikiti wa Mbuyuni hapa NCHINI ZANZIBAR
 Mahojiano ya Sheikh Farid na Waandishi wa Habari – Msikiti wa Mbuyuni
Baada ya shukrani kwa Mwenyeenzi Mungu anasema Uislamu umefundisha uadilifu na heshima na hivyo uislamu hauhusiki kabisa na sala hilo
Sisi kama viongozi wa dini tunakanusha kuhusika na uchomaji wa makanisa na tunalaani uharibifu wa mali za watu na tunalaani vitendo vilivyofanywa na jeshi la polisi
Uislamu haujakataza waislamu kuishi na watu wasiokuwa waislamu
Sheikh Farid anasema vyombo vya habari havikutenda haki bali vimekuwa vikifanya kazi kwa kutumikia upande mmoja Jambo ambalo kimaadilini ni kosa
  1. sheikh farid anasema amekamatwa imamu wa msikiti na kuingizwa katika gari kwa nini wakati sheria za kumkamata mtu sio hivyo kabisa bali nikumvujia heshima yake.
    sheikh farid anasema watu wameingia mitaani na kuanza kufanya huduma mbali mbali ni nani aliyefanya mambo hayo? hayo ni shindikizo kutoka chama tawala na walisema wazi kwamba haiwezekani waendeleea na mihadhara ya kiislamu na iwapo haitasita basi wapo vijana watajitokeza kufanya fujo
    na hilo limetendendwa na vijana wanaojulikana na hao wanajulikana waliofanya hivyo jeshi la polisi limetoa taarifa zao wanasema kwamba pamoja na kuwa na dhamira ya kufanya mkutano lakini kumefanyika matendo vya uvunjifu wa amani jee kulikuwa na uvunjifu wa amani uliofanywa na jumuiya ya uamsho?hakuna fujo iliyofanywa na aumsho kabisa.
    jeshi la polisi wanasema uongo kuwa wamezima maandamano wakati sio kweli hajakamatwa
    taarifa za jeshi la polisi ni uongo mtupu na sio kweli, wanasema lugha za matusi kwa viongozi, nani tumemtukana cd zetu tunazitoa kila pahala na umepewa uhuru na cd tunaziuza kila pahala na zipo mitaani habu chukuweni mukangalia kama tumtukana mtu sisi tunadai nchi yetu tu basi.
    jeshi la polisi wanasema uongo kuwa sisi tumezuwia njia. kwa hakika sisi hatujazuwia njia tumetumiya bara moja tu angaliyeni video zetu muone kama tumezui njia pia sisi hatutaki uongozi mnatushangaza sana, akili gani hiyo jamani
    jeshi la polisi mnatwambia kuwa tumetembea na vingora, sasa tunawauliza hivi vingora vya dulani vinakushughulisheni? hivi kweli vingora vyetu vinawashughulisha? wakati sisi tumetembea kwa usalama na kuweka usalama njiani kwa lengo la kuchunga amani na sio jengine
    jeshi la polisi linasema tumewachoma watu kwa ncha kali. nani kachomwa kwa nchi kali sio kweli sisi tumejaribu sana kuwaambia watu wasichokozeke
    jeshi la polisi linasema kuwa sisi tumewatuma watu wavamie vituo. hiyo ni vibaya sana hakuna mtu aliyetumwa na sisi wallahi wametupigia simu vijana vipi sheikh tuvamie vituo vya polisi tukawaambia hapana chagueni vijana wawili watatu mwende polisi kuulizia sheikh wenu kwa nini akakamatwa jeshi la polisi linasema kituo cha polisi kimevamiwa, kwani kimevamiwa vipi hemu watupe jawabu wamevamiwa vipi?. mheshimiwa shein kuwa makini na usikubali kupewa taarifa zisizo sahihi
  2. sheikh farid. jeshi la polisi linasema kuwa polisi wanatutafuta kwa gharama zozote,
    sheikh farid mimi niliitwa na jeshi la polisi na nikatakiwa nende polisi na sikumpa taarifa mtu yeyote kwa ajili ya kuwa sikutaka amani ivunjike,
    kiufupi hivyo ndivyo ilivyoendelea na taratibu zetu zitaedelea kama tulivyozipanga
    sisi nguvu yetu ni kumuelekea mola wetu na tunafanya ibada kucha nzima
    sisi tutafanya maandamano na tutaomba kibali na huo ndio uhuru wetu, jumapili tutafanya mikutano kama kawaida, hii jumuiya imesajiliwa rasmi na inafanya kazi kwa taratibu za kisheria ibara ya 29 kila mmoja ana uhuru wa mawazo na uhuru wa dini bila ya kuathiri sheria zinazohusika je sheikh sio mtu je hana uhuru kazi ya kueneza dini na shughuli za mtu binafsi, jumuiya imeshafanya taratibu zake kwa jeshi la polisi lije kutulinda na sio kwa sababu nyenginei
    makamo makuu ya polisi ipo bara na sio hapa. na hili ndio moja ya kero za muungano na hii ni moja ya dharau pia
    watu wanawasiwasi sijui kwa sababu gani au wanadhani yakifanikiwa haya mimi ndio nitakuwa amiri jeshi mkuu ..?tukifanikiwa wao ndio watabaki kuwa na kazi zitazidi haswa nini wacheni mambo yenu.
  3. Tunawaambia waanchi na viongozi kwamba tumeshafanya mihadhara mbali mbali, mikutano makongamano na kila kitu kwa salama na amani na hilo tumeshafanya sana na wanatoa wito kwamba mje kwa wingi
    gazeti la mwananchi limesifiwa
    Gazeti la zanzibar leo limeandika uongo kuhusu sheikh Nassor Bachu na wenyewe wameshatoa taarifa kwamba wamekerwa na watakwenda mahakamani na nyinyi pia hamuja andika mpaka sasa ndio munandika wewe siumetoka bara kuja hapa kwa dugu zako ili ujuwe kuna nini sasa mbona unasema zanzibar hakuna kitu..?
    sheikh farid anasema lengo la itikafu ni kuwaombea dua wananchi wote waliofikwa na maafa
    kuna vijana wamekamatwa na watu hao hawana uwezo
    leo hii inamwambia mtu atoe fedha au apatiwe dhamana unadhani watazipata wapi wakati mtu fedha ya kula hana mnamwambia akatoe fedha ya millioni 2 au liki 3 na nyinyi masheha na tawala za mikoa chungeni sana watu kuja kwenu kisha nyinyi mukawazungusha angaliyeni sana.
    jeshi la polisi muwe makini mmewakamata watoto watu, chungu nzima kuna familia hapa watoto wao wapo ndani lakini wazee watashindwa kuvumilia kwa hivyo tunakuombeni mahakama na jeshi la polisi kuwa makini katika hayo sheikh amemaliza na sasa ni wakati wa kuuliza masuali,
  4. Anauliza juma mohammed kutoka idara ya habari maelezo: sheikh mmezungumzia mambo mengi lakini mmetwambia kuwa kuna watu wamechoma makanisa ni watu gani kutoka kikundi gani na wanatoka katika kikundi gani? na suali jengine ni lini jumuiya zitafikia kikomo katika kutoa elimu na katiba? na suala la tatu ni jee jumuiya zote zina kauli moja kuhusiana na madai yenu?
    mwandishi wa daily news Sariboko anasema tume ya katiba ndio itakayokuja kukusanya maoni kwa nini mnashindwa kufuata subira mkasibiri tume ya katiba?
    mwandishi mwengine wa TBC, Juma Bwegege anauliza tokea tafrani hizi zimetokea jumuiya ya uamsho ilipewa kibali kuendesha mihadhara na imejiingiza katika siasa kuongelea mambo ya muungano, suali la pili uchomaji wa makanisa lakini wale wafuasi wanajinasibu kuwa ni jumuiya ya uamsho na wakati mwengine wanasema watanzania bara waondoke nchini jee jumuiya inakubali kwa kutoa matamko kama hayo?
    zamu ya mwandishi wa mwaananchi, Eliyas Msuya, kuhusu majina ya wachomaji kanisa mnaweza kuyatangaza? na kama kuna vijana wa umoja wa vijana jee mnaweza kututajia majina yao? suala jengine ni waraka umetolewa ambao nyinyi ni wapemba jee nyinyi asili yenu ni nini?
    Munir Zakaria kutoka chanel 10: rais alisema jumuiya yenu inatoka katika mstari na mnaingia katika kazi za siasa na sio dini, unazungumzia muungano kabla ya katiba mnataka watu wajadili muungano kama wanautaka au hawautaki jee uislamu unasemaje ukinambia mimi unataka kuuvunja muungano? na mimi sitaki uvunjike muungano kwa sababu mfano mimi nimezaliwa ndani ya muungano mfano watu kama mimi tupo maelfu ya watu hawataki kuuvunja muugano, tuangalie wale wazanzibari waliopo huko bara, jee kuna muungano wa unguja na pemba? na mwisho huu muungano ni wa kihistoria na ulikuwepo tokea zamani
  5. khatib suleiman kutoka gazeti la habari leo: uamsho inanasibishwa na chama cha siasa jee ni kweli? lakini jengine ni kuwa hao vijana wa ccm hebu tufafanulie
    mohammed mhina wa jeshi la polisi: tunaomba mtujulishe kuhusu kuchomwa makanisa lakini pia mtujulishe ni kina nani waliokuwa wakiweka magogo njiani na kuwasha moto
    mwinyi sadallah kutoka nipashe: jumuiya ya uamsho unasema hamuhusiki na vurugu sasa mtawasaidiane walioathirika na tokea kutokea kwa hilo mmekwenda kuwapa pole? mjadala wa katiba bado haujaaza na haya matukio hamuoni kuwa haya matukio yanayotokea kuwa amuoni kuwa mnafanya kazi za bure?
    Jacob anatoka hits fm anauliza: jumuiya ya uamsho kazi yake ni kueneza dini na siasa siasa na ndivyo ilivyosajiliwa kwa nini mnazungumzia suala la muungano, jumuiya inashutumiwa na moja kwa moja mmehusishwa lakini nyinyi mnakana sasa mnalizungumzaje suala hili?
    kuna watu wamevunjiwa baa na wamevunjiwa makanisa na wameumizwa sasa mnazungumziaje?
    mwajuma juma wa jumuiya ya uamsho anasema sijawahi kwenda katika mikutano wa uamsho lakini niliwahi kusikia katika mikutao ya uamsho au laa maana nilisikia kupitia radio nuur nikasikiliza kuwa mnautaka muungano au hamuutaki? na jengine nikasikia kuwa wanawataja viongozi wakisema nyerere laanatu llah jee hao ni uamsho au ni watu wengine waliojinasibisha na uamsho? naomba kupata ufafanuzi
  6. masuala yalioulizwa jumla kama 15 na yanaanza kujibiwa
    sheikh farid anajibu kuhusu suala la kuchomwa makanisa anasema sisi tunalaani vikali kuchomwa moto makanisa sio makanisa tu hata katika nyumba kuchomwa hatukubaliani nalo, lakini hatuwezi kutoa majina lakini tunasema vipo vyombo husika wao watatoa taarifa sisi tutawasaidia kuwatafuta
    kuhusu mihadhara mpaka lini tunajibu kuwa mpaka kieleweke na tutaendelea kwa sababu katiba haina kikomo cha muda tutaendelea mpaka tuseme tumefanikiwa zanzibar imepata heshima yake na mamlaka yake
    suala la jumuiya na, maimamu, uamsho, markaz, zanzibar islamic center, jumuiya ya omar abdulaziz,
    suala la tume kwa nini tususibiri,jibu ni kuwa ndani ya katiba ya zanzibar tunasema ipo wazi tuna haki ya kisheria, mtu au asasi yoyote ambaye atataka kufanya programu za elimu atoe taarifa katika tume pamoja na kueleza chanzo cha fedha lakini siku hizi sisi hatufanyi kazi hiyo hiyo tumeshamaliza sisi tumekwenda katika hatua nyengine kabisa
  7. sisi tundai kura ya maoni na hilo sio jambo geni hasa hapa znz imeshawahi kufanyika maana tumewahi kuwa na kura ya maoni,
    Sheikh farid anasema kila mzanzibar anayo haki ya kushiriki
    katiba yetu inasema tuna haki kwa sababu kila raia ana haki ya kutoa na kupokea maoni kwani sheikh sio raia na wauliza nyinyi wandishi wa habari sheikh sio rai..?wakajibu ndio raiiii. sasaba
    uislamu na siasa hakuna tofauti kwa sababu uislamu ni mfumo kamili sisi hatuna ya mungu mpe mungu na kaisari mpe kaisari hayo sisi mambo yetu sisi uislamu ni mfumo kamili
    na ukitaka kujua zaidi kaangalie katika miaka ya dharuba kitabu cha aboud jumbe ameelezea kuhusu dini na siasa na akasema huo wimbo umeandaliwa na watu maalumu na amaeelezea kwamba hakuna tofauti dini na siasa na ikiwa kuna mtu anasema dini na siasa ni vitu tofauti basi mtu huyo ikipenda kusema huyo ni mnafiki wa yote maana hajuwi dini ni na siasa ni nini yeye yopo yopo tu.
    sheikh farid, kelele yetu sio ya bure sasa tumeamka
    kuhusu suala la kuwa sisi tunawafukuza watu wa bara hilo sio kweli, sisi hatujamfukuza mtu na wapo wazanzibari walioowa bara sisi sio maadui kati yetu kwa sababu sisi na watanganyika ni ndugu na hilo halina mjadala ikiwa utakubuka katika mihadhara nilimpandisha mtanganyika iliniwaonyeshe kuwa sisi hatuwafukuzi watanganyika Na hao ni ndugu zetu na damu hatuwezi kuwa maadui zetu,
    sisi tuna historia kubwa sisi na watanganyika hatuwezi kutengena nao lakini tukivunja muungano tunazidi kupendana na watakuwa wametusaidia sana kwa sababu kila mmoja awe na nchi yake
    kuhusu suala la vijana wa ccm ndio wao wanahusika kwa sababu walikuwa wakisema wazi kabisa kuhusu suala hilo walisema waziwazi kwamba watatupiga
    kuhusu kabila sisi sote ni wazanzibari na tunafuata katiba na katiba ya zanzibar inasema kila mzanzibari ana wajibu kuhifadhi, kulinda na kuhifadhi uhuru wa zanzibar, sisi tunasema sote ni wazanzibari hatuna muda wa kutengana sisi ni wamoja bila ya kujali huyu anatoka wapi,
    hayo ni maneno ya kachorora ambao hawana kazi za kufanya na wanaeneza maneno ya ovyo ya kuwataka wapemba waende kwao
  8. kuhusu suala la uamsho kuwa kinafadhiliwa na chama cha kisiasa jibu ni kuwa sisi hatuna mtu yeyote anayetuongoza wala chama cha siasa na
    kuhusu uongozi wetu, sisi tunachaguana katika utaratibu wetu maalumu wa kuchaguana na kwa hivyo sisi hatukatai tukipewa uongozi
    kuhusu suala la tutawasaidia vipi watu walioathirika tunasema sisi ni maskini hatuna uwezo wowote wa kuwasaidia lakini tunasema kwamba tumehuzunishwa sana na matukio hayo
    kuhusu suala la kuvuruga mchakato ndio sisi tunataka hasa mchakato uvurugike
    viongozi lazima watambue kwamba wananchi wanataka madai yao yasikilizwe na vongozi wao
    kuhusu suala la nani aliyekuwa akiweka magogo njiani, jibu ni kuwa ni wazanzibari wenyewe ambao wamechoka na hilo jibu ni la jeshi la polisi
    kuhusu mchakato, sisi tunataka kwanza tuletewe kura ya maoni ya kuulizwa watu kama wanataka au hawataki muungano
    zanzibar sisi katiba tunayo na hatutaki katiba nyengine
    hakuna kulazimishana. kuna mbunge aliwahi kusema kwamba zanzibar ni koloni letu, serikali yote kimya basi kama wao wamefurahi sisi tumekasirika na hattaki majibu hayo na inatuuma sana
    kuhusu utaratibu wa kuitwa viongozi ni kuwa wanatuita na sisi huwa tunakwenda na wangekuwa wanatuita basi tunakwenda bila ya wasiwasi na hilo halina shida lakini hawafati taratibu
    kuhusu suala la kukaa na kamati kuhusu kero za muungano jibu kwa kweli sisi hatujadili kasoro za muungano
    kuhusu suala la kutaja viongozi kwa laana hiyo ni dua imo ndani ya quran na sisi tukimtaja kama ni kiongozi basi watu ndio wanaitikia hilo
    sheikh anamalizia na kusema laanatullah ni dua kutoka ndani ya quran
    na mwisho kabisa tunasema tutendewe haki maana na misikiti imepigwa mabomu na vyombo vya habari nendeni mkachukue picha
  9. Watu wa zanzibar ndio wapole lakini kwa sasa hamna tena yakhe yakhe na ammi ammi,

No comments:

Post a Comment