Friday, July 27, 2012

HILI NDIO FIRAUNI LILILOTOWA AMRI WAISLAMU WAPINGWE MABOMU MSIKITI WA MBUYUNI

“Alaisallahu biahkamil haakimiina.”Kwamba, “Je, Mwenyezi Mungu si Hakimu muadilifu kuliko mahakimu wote?”Ikiwa na maana kuwa lazima atawalipa watu wote kwa uadilifu kutokana na matendo yao.Kamanda Azizi Juma Mohamed, amesema kuwa“wafuasi wa Uamsho wakiwa
M O J A y a A d h k a r iwaliyoleta Waislamu pale Masjid Mbuyuni ni kusoma kipande cha aya ya suratut tiin inayosema:
na bendera walianza vurugu,kupanga mawe barabarani na kuchoma moto matairi.Kufuatia hali hiyo, Jeshi
la Polisi likaamua kutumia nguvu kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na maji yenye kemikali za kuwasha.”Vyombo vingine vya habari vikadai kuwa Uamsho walianza kuwashambulia Polisi kwa mawe.
“Alaisallahu biahkamil haakimiina.” Hapana shaka ipo siku ukweli utadhihiri na kila aliyeumia siku ile ama kupotelewa na kitu,atasimama kudai haki yake.Yote mpaka kauli hii kwamba Masheikh wa “Uamsho wakiwa na bendera walianza vurugu, kupanga mawe barabarani na kuchoma moto matairi”, itadhihirishwa na kutolewa hukumu na Hakimu Muadilifu.Hiyo ndiyo Siku ambayo vitafunuliwa vitabu ambapo“ u t a w a o n a w a k o s e f u wanavyoogopa kwa yale yaliyomo humo (katika vitabu vyao). Na watasema:Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika? Na watayakuta yote waliyo yatenda yamehudhurishwa hapo. Na Mola wako Mlezi h a m d h u l u m u y e y o t e . ”(18:49).Hata hili la Msikiti wa Mbuyuni nalo limeandikwa? Watahoji na kushangaa w a l i o a m u r u k u p i g a Waislamu mabomu na wale waliotekeleza amri hiyo.“Watasema: Ole wetu!Kitabu hichi kina nini!Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika.”Tunaambiwa Yeye ndiye Mfalme pekee siku hiyo-Maalik yaumiddiin. Siku hiyo hatakuwa na nafasi Obama, Kikwete wala Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi.L e o K a m a n d a w e t u Azizi katika matukio kama hili la kupigwa waumini wakiswalia maiti, ndio msemaji. Ndio tunamsikiliza atupe taarifa rasmi. Ila Siku hiyo tunaambiwa“laayatakallamuuna ila man adhina lahur rahmaanu waqaala swawaaba.”Hiyo ndiyo siku ambayo Qu’ran imeisifu ikisema siku watu watakapoiona “kila mwanamke anyonyeshaye atamsahau amnyonyeshaye (mwanawe) na kila mwenye
mimba ataiharibu. Utawaona watu wamelewa, kumbe hawakulewa, lakini ni adhabu ya Mwenyezi Mungu kali mno.”Niseme kuwa ilikuwa ni msiba juu ya msiba pale p o l i s i w a l i p o w a v a m i a Waislamu wakiswali Swala ya Maiti Ghaibu na kuwapiga mabomu ya machozi. Binafsi nilibahatika kuwepo katika
swala ile. Nilishuka bandarini kiasi saa tisa kasoro na kuelekea moja kwa moja katika Msikiti wa Mbuyuni.
Nilipofika nilikuta Waislamu wakiendelea na Adhkari mbalimbali.“Hasbunallah waniimal w a k i l ” , n d i y o a d h k a r i niliyoikuta ikafuatiwa na kusoma kipande cha aya ya surat tiin inayosema:“Alaisallahu biahkamil
haakimiin.”Baada kumaliza adhkari,m s h e r e h e s h a j i ( M C )alitangaza ratiba ambapo alisema kuwa tutaswali swala ya maiti ghaibu,kisha itapigwa adhana na kufuatiwa na rakaa mbili za suna kabla ya kusimama kwa ajili ya swala ya Alasiri.Aidha ilifahamishwa kuwa baada ya swala kungekuwa na nasaha kwa ufupi kabla ya kuomba dua ya pamoja kufunga shughuli.Mpaka sasa najiuliza, lakini bado sipati jibu. Kitu gani kiliwafanya polisi kuvamia na kuwapiga mabomu Waislamu waliokuwa pale Mbuyuni?Katika kutafakari, nikasema labda ni kutokana na yale yaliyosemwa na Masheikh waliopata fursa ya kutoa nasaha. Hata hivyo kwa vile nilikuwepo, nilisikia mwenyewe kilichosemwa,sio maneno ya kuambiwa,bado nashindwa kukubali kwamba hiyo ndiyo ilikuwa sababu.Wa l i o p a t a f u r s a y a kuzunguza walikuwa watu wawili, Sheikh Farid na Ustadh Suleiman. Ilikuwa asimame Sheikh Msellem baada ya Sheikh Farid, lakini ile anakaa tu Farid, Mvua ya mabomu ikaanza.Sheikh Farid aliongea mambo mawili tu. Kwanza
alisema kuwa wanajitahidi katika yale wanayosema k u y a w e k a p i a k a t i k a maandishi maana baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha.Akatoa mfano wa Mwakilishimmoja katika Baraza la Wawakilishi ambaye alidai kuwa Uamsho wanawahimiza watu wakatoe maoni katika Tume ya Katiba na waseme kuwa hawautaki muungano.Akasema, wao wanasema na wanachofanya ni kutetea haki ya Wazanzibari, kutetea
heshma ya Rais wa Zanzibar kama Rais wa nchi. Kwamba w a t u w a k a t o e m a o n i ambayo yatawahakikishia Wazanzibari haki yao ya kuwa na nchi huru na serikali yenye mamlaka kamili (Sovereign
State).Jambo la pili akaeleza kwa ufupi ni kwa nini wanaungana na Waislamu Tanzania Bara kukataa zoezi la sensa ya watu na makazi mpaka kipengele cha dini kiinginzwe. Hoja alizotoa ni zilezile ambazo zinatolewa na Waislamu Bara. Binafsi sikusikia neno lolote ama linaloweza kuitwa kuwa ni tusi, kutukana au la
uchochezi.Ustadh Suleiman ndiye aliongea kwa muda mrefu kidogo na ndiye aliyeanza.Yeye alizungumzia mambo matatu: Kwanza alieleza ni kwa nini wameamua Waislamu kufanya dua ya peke yao kuliko kungoja ile ya kiserikali ambayo hukusanya Waislamu, wanasiasa na Wakristo. Akasema, katika dua hiyo ya watu wa imani tofauti, kuna wanaoanza kwa kumkufuru Mungu.Akatoa mfano kwa Wakristo ambao huomba kwa jina la Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.Katika ufafanuzi wake akanukuu aya ya Qur’an isemayo: “Na (makafiri)h u s e m a : “ ( M w e n y e z iMungu) Mwingi wa rehma amejifanyia mtoto. Bila
shaka mumeleta jambo lichukizalo kabisa (kwakusema hivyo). Zinakaribia mbingu kutatuka kwa (tamko)hilo na ardhi kupasuka na vipandevipande. Kwa kule kudai kuwa (MwenyeziMungu) Mwingi wa rehema ana mtoto.) (19:88-91).Ndio akasema, itakuwaje t u k a e m a h a l i a m b a p o yanasemwa maneno ambayo
mbingu zinakaribia kuanguka k w a u z i t o w a d h a m b i inayotokana na maneno hayo,kisha tunanyanyua mikono tunamwomba Mwenyezi Mungu awarehemu maiti wetu. Akatoa mfano wa kibinadamu, kwamba jaaliya mtu kaja nyumbani kwako akakunasa kibao au akakupiga bakora safi, kisha anakuomba maji ya kunywa. Ni katika kuzingatia hayo akasema kuwa wao waliona ni bora Waislamu kufanya dua ya peke yao.
Na hili ndilo alilofanya pia Rais Dr. Ali Mohamed Shein katika swala ile iliyoongozwa na Mufti Sheikh Swaleh Omar Ka’bi pale Masjid Mushawwara,Muembe Shauri. Hapana shaka katika waliokufa wapo pia Wakristo, lakini mara hii serikali haikufanya Dua ya mseto w a Wa i s l a m u n a Wa k r i s t o.Walifuata nyayo z a Wa i s l a m u waliokusanyika Masjid Mbuyuni Ijumaa iliyopita.Jambo la pili alilozungumza n i k u o n y e s h a jinsi viongozi w a s e r i k a l i wanavyohusika na majanga haya ya kuzama meli na watu kupoteza maisha. Alisema,watu wasikimbile katika Qadari y a M w e n y e z i M u n g u.W a s i p e l e k e
l a w a m a k w a A l l a h , b a l i w a t i z a m e kwanza, iwapo hawana mchango k a t i k a j a n g a h i l o ? A l i t o a mfano wa mtu kuacha mlango w a z i h a l a f u unatawakal.K a t i k a uchambuzi wake mdogo akasema k u w a a n a o n a kuna uzembe.Kwamba taasisi z a s e r i k a l i h a z i w a j i b i k i
ipasavyo. Akatoa mifano ya meli mbovu ambazo h u r u h u s i w a k u f a n y a k a z i wakati vyombo vya usimamizi vipo. Lakini pia akazungumzia uzembe kwamba b a a d a y a a j a l i k u t o k e a h a p a k u w a n a u h a r a k a w a vyombo husika k u p e l e k a h u d u m a z a uokozi. Vyombo vya uokozi vilikwenda
takriban masaa matatu baada ya tukio. Akasema kuwa hata pale walipokuja watu binafsi wazamiaji wakataka wapelekwe kwenye tukio,wakasaidie kuokoa watu,waliambiwa vyombo havina mafuta. Na hili limesemwa n a k u t h i b i t i s h w a n a waokoaji wenyewe. Ndio alipofika hapo akasema, hivi wangeambiwa kuna meli inaondoka imebeba karafuu za magendo, wangesema vyombo havina mafuta? Na
mbona magari ya kuwavamia Uamsho hayakosi mafuta hata siku moja! Mbona magari yao
(wakubwa) hatujaambiwa kuwa yanakosa mafuta?Ila mafuta ya vyombo vya kuokoa watu, ndiyo kila wakati hakuna mafuta. Lakini pia akasema kuwa katika jambo linalozua maswali mengi yasiyo na majibu ni
pamoja na hili: Kwamba m e l i i m e z a m a e n e o l a Tanzania Bara, kwa nini havikuja vyombo vya uokozi kutoka Tanzania Bara? Na hili alilisema akinunukuu katika yale wanayozungumza na kuhoji watu mitaani na watu waliohusika na uzamiaji kuokoa watu na kuopoa maiti.Lakini akasema pia kuwa hakubaliani na hoja ya serikali kwamba haina fedha za kununua meli kubwa na mpya ambayo ingesaidia kuondoa tatizo la usafiri kwa Wazanzibari.Kwa msisitizo kabisa akamuelekea Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dr. Shein akiwakumbusha kuwa kwa mujibu wa Dini wanayoifuata,yaani Uislamu, mtu akiuwa
mtu mmoja ni sawa na kuuwa watu wote. Kwa hiyo, waone umuhimu wa kuwawajibisha wale wanaofanya uzembe na wale wasiowajibika katika nafasi zao hadi kusababisha vifo kama hivi vya ajali ya meli. “Msiwafanye watu dagaa tonge”, alisema msemaji akimaanisha kuizindua serikali kujali maisha ya watu.
Akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa kwa jinsi hali inavyokwenda, itafikia mahali watu watachoka. Watatoka mitaani kama serikali inataka iwauwe wote. Wabaki wao wenyewe viongozi wa serikali na wake zao asibakie mtu wa kuwabughudhi.Binafsi naamini kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesikia kilio cha Ustadh Suleiman na Waislamu wote ndio maana
amekubali ombi la Waziri Masoud kujiuzulu. Ingekuwa alichofanya Ustadh Suleiman Dua ya kuhitimisha, hapo ndipo vijana wa Nchimbi w a l i p o v a m i a . G h a f l a zilionekana gari za FFU zikivamia eneo hilo na k u a n z a k u v u r u m i s h a mabomu. Kutokana na kizaa zaa hicho,watu walianguka na kukanyagana wakiwemo w a n a w a k e n a w a t o t o.Wachache waliobaki kutaka kujinusuru hapo hapo ndani ya msikiti walikuta kuwa napo hakukaliki kwa sababu ya moshi wa mabomu.Kutoka eneo la Msikiti wa Mbuyuni, polisi walianza kuranda mitaani na kupiga mabomu ovyo, hali iliyowatia m o r i n a k u w a c h e m s h a vijana mitaani nao wengine wakaanza kuchoma moto matairi barabarani. Nikitokeameneo la Mbuyuni, nilipita vichochoroni hadi kutokea e n e o l a M a s j i d S a l a m nakutembea kando kando ya barabara kuelekea Michenzani.Hapo nikakuta FFU wakipita na gari zao huku wakipiga mabomu ovyo. Kwa hakika
ilikuwa vigumu mtu kujua nini kilikuwa kikiendelea. Watu wanapita mitaani, wengine wapo katika sehemu zao za biashara na katika makazi yao wanaendelea na shughguli zao, mara zinapita gari za FFU wanarusha mabomu. Hali hiyo iliendelea mpaka usiku wa manane hali iliyosababisha watu wengine kushindwa kabisa kutekeleza ibada yao ya Tarawehe na Qiyamul laili.Wakati napita mitaani,nakutana na watu wanalaani.“ T u m e w a f a n y a n i n i ?Tumepotelewa na ndugu zetu na mpaka hivi sasa maiti hawajapatikana, tunapigwa
mabomu. Tumekosa nini?“Msiba haujamalizika wanatupiga. Tumefiwa,tuna majonzi, wengine hata maiti hatujapata, tunapigwa.Haya ndiyo (Rais) Kikwete aliyokuja kutuletea! Haya ndiyo Waziri wake Emmanuel
Nchi aliyokuja kutuletea!K u m b e z i l e s a l a m u n a masikitiko ilikuwa sawa machozi ya mamba.”“ H a t u t a k i c h o c h o t e,unasema hivi sasa hatutaki chama chochote, sisi sote  t u n a k i m b i l i a U a m s ho,
tumechoka.”Hiyo ilikuwa kauli ya msafiri mmoja katika boti ya Kilimanjaro 2 iliyoondoka Zanzibar Jumamosi saa moja asubuhi kwenda Dar es Salaam.Na kwa hakika haya ndiyo yalikuwa mazungumzo katika boti hiyo kila mmoja akieleza kwa namna yake lakini ujumbe ukiwa mmoja: kuwa watu wamechoka. Hawathaminiwi.W a n a d a n g a n y w a .Wanaonewa. Wanahujumiwa na kudhalilishwa.Haya ndiyo aliyovuna M h e s h i m i w a Wa z i r i Emmanuel Nchimbi kwa ule ‘ubani’ wa mabomu kwa wafiwa Zanzibar pale Masjid Mbuyuni.Ipo kauli ya Qur ’an kwamba mengi ya majanga yanayowakumba wanadamu,wanayachuma kwa mikono yao. Ubani huu wa mabomu kwa Waislamu wanaoswalia maiti na kuwaombea Dua, ndio unayowafikisha Wazanzibari kuwaona viongozi wa Serikali ya Muungano Tanzania kama maadui wa Wazanzibari. Na hii huzidi kupandisha lile joto la kutaka nchi huru yenye mamlaka kamili.

No comments:

Post a Comment