Friday, July 27, 2012

JAHAZI LAZAMA LILILOKUWA LIKITOKEA PEMBA JE WAZIRI MPYA ATAJIUZULU PIA...?


Mtoto Isack Hamis Suluhu (5), amefariki dunia na wengine saba wamenusurika baada ya jahazi walilokuwa wakisafiria kutoka Pemba kwenda Unguja kuzama katika Bahari ya Hindi.
Tukio hilo limekuja wiki moja tu tangu boti ya MV Skagit ilipopinduka na kuzama katika mkondo wa dar es salaam na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Pemba, Hassan Ali, alisema jahazi hiyo inayojulikana kama Safina ilizama katika eneo la mkondo wa Nungwi juzi jioni.
Alisema kati ya walionusurika mmoja hali yake ni mbaya na amelazwa katika hospitali moja mjini Pemba na kwamba wengine saba wakiwemo watoto wawili hali zao ni nzuri.
Kamanda Ali alisema chanzo cha ajali hiyo ni kujaza mizigo na abiria wengi kupita uwezo wake na kwamba watu hao kwa kuwa ni wazoefu na shughuli za uvuvi walijiokoa wenyewe kwa kuogelea.
Kumekuwa na mfufulizo wa matukio ya meli na jahazi kuzama katika Bahari ya Hindi hali ambayo inatishia usalama wa maisha ya watu wanaotumia usafiri wa majini.na hasa hasa uzembe uliyo kuwa mkubwa ni kujaza vyombo hivi kupita kiasi.kubwa zaidi ni kampuni hii ya mapinduzi zanzibar kuwa haijali kuchunguza chombo kipi ni cha abiria na kipi ni cha mizigo imekuwa kila chombo sasa ni abiria na mizingo na kujazwa kupita kiasi lawama zote tunazitupia hii kampuni ya mapinduzi daima maana sio serekali hii ni kampuni tu.

No comments:

Post a Comment