Saturday, July 21, 2012

JESHI LA KIKURIA LAWAPIGA MABOMU WAZANZIBAR KATIKA MSIKITI WA MBUYUNI NA MIJINI MOTO KWA KUWAOMBEA DUA MAITI NA WALIO FIKWA NA AJALI YA KUZAMA MELI



Jeshi la kikuria (FFU) limezua mtafaruku mkubwa katika nchi ya Zanzibar na vitongoji vyake baada ya kuzunguka mji mzima wakiwapiga mabomu ya machozi wananchi.wa nchi hii ya zanzibar Mabomu hayo yalipigwa baada ya kufika kwenye msikiti wa Mbuyuni ambako waumini wa dini ya kiislam walikuwa wakiwaombe dua watu waliokufa kwa ajali ya meli Mv Skaget.hii ni kujulisha kuwa wazi jeshi hili ni la kikafiri na hali paswi kabisa kuwa jeshi la zanzibar pia hii ni kuonyesha wazi kuwa sisi wazanzibari tunatawaliwa na wakoloni weusi tanganyika sasa tuwaulize wafalme wetu tanganyika kuwaombea dua maiti pia ni vibaya ktk utawala wenu wa kimabavu hapa nchini kwetu zanzibar...?
Askari hao wakiwa kwenye magari yao walifika eneo la msikiti huo ambapo waumini wakiongozwa na viongozi wa Taasisi za Kiislam chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (Jumuki), walikuwa wakiomba dua maiti walio zama na meli.
Dua hiyo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed ilikuwa na lengo la kuwaombea maiti na majeruhi waliopata ajali ya meli.
Askari hao walipofika kwenye eneo la msikiti huo walianza kurusha mabamo na kuzuwa mtafaruku mkubwa je kishein hichi kiraisi kifupi kama firauni hakijuwi kama kuna ramadhani je kisheini hujuwi kuwadhibiti watwana wako wawahishimu wananchi angalau katika ibada zao.
Baada ya kuendelea na ibada yao ambapo walikuwa wamemaliza sala na kuendelea kuomba dua, ndipo polisi walipoanza kurusha mabomu ya machozi na kuwatawanya watu waliokuwemo ndani ya msikiti huo je sasa nchi hii ishakuwa ndio nchi ya kwanza duniani kukataza watu wasiabudu wala wasiswali..?
Baada ya kuwatawanya waumini hao, magari yanayokadiriwa kufikia sita ya jeshi la kikuria (FFU) yakiwa na askari waliovalia nguo za kujihami, walianza kurusha mabomu katika  maeneo mbali mbali ya mjini.
Baadaye magari hayo yalianza kuzunguka katika vitongoji mbalimbali vya mji wa Zanzibar na kuwashangaza wananchi ambao wengine walikuwa hawaelewi kilichokuwa kikiendelea.
“ Sasa tumekosa nini hadi wanakuja kuturushia mabomu huku tumewakosea nini,” alihoji mwanamke mmoja wa makamo baada ya kusikia mabomu yakipiga mfululizo.
Watu walikuwa wakikimbia na watoto huku wafanyabiashara wa eneo la Darajani wakisomba vitu vyao na kufunga maduka.
Katika maeneo ya mitaa ya Kikwajuni na Michenzani, magari hayo ya polisi yalikuwa yakizunguka na kurusha mabomu hadi katika vichochoro vya mitaa hiyo.

No comments:

Post a Comment