Saturday, July 28, 2012

WAZANZIBAR WALIO NJE WATAKA HARRISON MAKYEMBE NA MKURUNGEZI WA BANDARI YA TANGANYIKA,BALOZI ALI IDDI NA MOHAMMED ABOUD WOTE HAWA KUSHTAKIWA KESI YA MADAI


· Ni lazima Wawajibike kisheria.
· Wadai Wazanzibari wanaoishi nje:

Na Free-Zanzibar People From Mkoloni Mweusi
Wazanzibari wanaishi nchi za nje na ambao jamaa zao walipoteza maisha yao na wengine kuathirika kiafya katika msiba wa kuzama boti ya MV Skagiti na MV Spice wamezungumza kwa sauti moja kutoka London, Toronto na Washington,Berlin,Paris,Dubai,na waliokuwepo nchini  ya Malesia baada ya kuhojiwa na muandishi wetu na kusema kwa pamoja kuwa watampeleka Mr Harrison Makyembe na mkurugenzi wa bandari ya tanganyika plasi VIP2 Balozi Ali Iddi na Mohammed Aboud kwa kile walichokiita kutowajibika na kutokufanya kazi zao sawasawa kama alivyohitajika na ile Kamati ya Sheini ya mwanzo iliyoundwa baada ya meli ya mwanzo kuzama iliyokuwa ikielekea Pemba katika mwaka 2011.
Wameelezea Wazanzibari hao kuwa kwa wakati huu wa uwazi na ukweli,kujiuzulu kwa Hamad Masoud ilikuwa ni vizuri sana lakini hata hivyo wahusika haswa bado wako madarakani waliofanya dungu zetu watoke roho zao mbichi na haya ni makosa ya jinai yametokea chini ya uongozi Mr Harrison Makayembe na mkurungezi wa bandari ya tanganyika na huyu VIP2 Balozi Ali Iddi n Mohammed Aboud. “Kwa kweli hawajawajibika bado mpaka watakaposimama mahakamani na kuwaeleza wote wale waliopoteza jamaa zao na ndugu zao kwanini meli iliachiwa kujaza watu kuliko kiwango chake ilipokuwa ikiondoka Dar Es Salaam.” Wameelezea Wazanzibari hao kwa uchungu sana walipohojiwa kwa njia ya simu na muandishi wetu wa Free Zanzibar People From Mkoloni Mweusi.
 alitakiwa Mr Harrison Makyembe n Mkurungezi wake wa bandari ahakikishe kuwa meli hazijazi abiria zaidi ya kiwango lakini imedhihirika kuwa wao hawajali wazanzibari wakifa na inaonyesha wanafurahia wazanzibari wakifa maana hata meli ilipoanza kuza walitowa tarifa ili wasaidiwe kuokowa watu lakini tanganyika haikufanya kitu chochote. ” Waliendelea Wazanzibari hao huku wengine wakilia kwenye simu.
“Ni kweli Mr Harrison Makyembe asingeliweza kuizuwia hali ya hewa kuchafuka au kuzuwia kasi ya mawimbi ya bahari, lakini kama boti ile ingelikuwa na abiria 250 tu ambao ndio kiwango chake basi msiba ungelikuwa mdogo kwa wananchi kuliko ulivyokuwa hivi sasa.au kama wangelitowa boti zao za uwokozi kwenda haraka kuokowa watu. baada ya tarifa waliopewa yasingelitokea haya ila ni wazanzibari wanao zama sio watanganyika ndio maana hawakujali hata baada ya kuwa na tarafa kama meli ya MV Skagit inazama” Waliendelea Wazanzibari hao
Wazanzibari hao wanakusudia kwa pamoja kumpeleka Mahakama Kuu ya Dar-Es-Salaam ‘a class-action lawsuit’ dhidi ya Mr Harrison Makyembe na Mkurungezi wake wa bandari ya dar es salaam,ambayo itamtaka awalipe ndugu wote wa Wazanzibari wote waliopoteza maisha yao na wale walioumia kwenye hili balaa, kwasababu wanasema yeye wao wanahusika moja kwa moja Mr Harrison Makayembe  na Mkurungezi wa Bandari ya dar es salaam.
Pia, wanaeleza kuwa kama Mr Harrison Makyembe angelisimamia vizuri usafiri wa meli baina ya Bara na Visiwani kushirikiana vizuri na Hamad kama walivyotakiwa na ile Kamati ya Sheini basi maafa yaliotokea yasingeli kuwa makubwa hivyo.
Wazanzibari hao wanastaajabu vipi baada ya kuelezwa na Kitivo Cha Hali ya Hewa cha DSM kuwa bahari itakuwa chafu boti ndogo kama hii ya MV Skagit iliweza kuruhusiwa kuanza safari yake na huku ikiwa imechukuwa watu zaidi ya kiwango chake. “ Hii ni miradi ya wakubwa na kama boti isingelisafiri watu wangelikosa sehemu yao”, ndio maana wakairuhusu iende ingelikuwa ni katika ziwa victoria wangelianchiya kweli ..? walihoji Wazanzibari hao.
Wazanzibari hao walivyoulizwa watadai kiasi gani walipwe kwa kila aliepoteza ndugu/jamaa yake walisema kwa sauti moja kuwa ” Nia yetu sio kutafuta uchumi bali kuwapa fundisho hawa wakubwa wa kitanganyika walio zoea kutuuwa”.
 Wazanzibari hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe kwa sababu lawsuit bado haijaenda Mahakama Kuu,Dar Es Salaam.
Wazanzibari hawa walisema Mr Harrison Makyembe  tokea hapo alikuwa akijipendekezesha sana kwa wale wenye kumiliki vyombo vya usafiri Visiwani”, alieleza jamaa mmoja, kwa simu yake ambayo ilikuwa Aionyesha amehadhibishwa sana na tokeo la meli hii ikiwa ni ya pili kuza. ” Vipi  mwaka mmoja nyuma alipoulizwa juu  yakuwa unafikiri litatokea tena akasema no no no  na  meli mpya ya Azam alisema eti kuwa meli hio inakuja na itafanya safari kwa kukuwakikishia wazanzibari usafiri wa usalama na kusaidia wananchi. Huu ni uwongo na inaonesha vipi Mr Harrison Makyembe alikuwa anajikomba na wamiliki wa biashara za usafiri hapa Visiwani”na kujipingia hisabu za mamillioni mangapi atajiingizia meli hii ikija hapa nchini.
“Hawa wote ni wanyonyaji na wanajaza abiria kwenye meli/boti zao kama dagaa.” Alieleza huyu Mzanzibari mwenye simu hasira kweli kweli, huku akionesha kufoka zaidi na zaidi na  hasira kwenye matamshi yake.
“Ni lazima Mr Harrison Makyembe na Mkurungezi wake wa bandari ya dar es salaam pamoja na VIP2 Balozi Ali Iddi na Mohammed Aboud wafikishwe kortini kujibu hoja za wananchi, kama sio hivyo midudu hii Tanganyika siku zote itakuwa wanatumaliza na baadae kulazimisha mawaziri wetu wanajiuzulu tu” Alinena Mzanzibari mwengine kwenye simu kutoka nje.
Wachunguzi wa siasa wanasema kama hii class-action lawsuit itapelekwa Mahakama Kuu huko Dar es salaam basi labda itakuwa ni onyo kwa wale wote wanaopewa madaraka nchini nchini humo Tanganyika.

No comments:

Post a Comment