Saturday, July 21, 2012

ZANZIBAR HATUNA SEREKALI TUNA WAHUNI TU VIONGOZI WOTE WAHUNI KANZU NA KOFIA NI GERESHA TU

NCHI ZOTE DUNIANI ZINA MARAISI SISI ZANZIBAR TUNA BOYAA LIMEWEKWA NA WATANGANYIKA HALINA LIJUWALO ZAIDI YA MAPINDUZI OOYEEEE
Nikiwa na masikitiko pamoja na huzuni kubwa kutokana na msiba mwengine mkubwa uliotokea Zanzibar na kupoteza tena maisha ya watu na mali zao,nimepigwa na mshangao mkubwa na kujiuliza hivi Zanzibar inaelelekea wapi ? Kuzim! Janga hili limenifanya nishindwe kuelewa hasa kuhusu Viongozi wetu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanafanya nini katika kuona maisha ya Raia zao pamoja na mali zao zinapotea kwa urahisi kama hivi,hili limekuwa ni jambo la kawaida kwa Wazanzibar na serikali yake.Huu si wakati wa kulaumiana lakini huu ni uzumbe mkubwa ambao unaonesha wazi wazi kwamba serikali ya Zanzibar haina matumaini kwa Wazanzibar.
Baadhi ya Viongozi wameanza kupokea fedha za zawadi, maanake mimi binafsi sioni kwamba ni fedha za maafa ili iweje huku wengi wa Viongozi wakiwa hawana hata hisia za huzuni moyoni na nyusoni mwao , niseme wanafurahia kwa hilo. Ni hivi karibuni baada ya MV. spice kuzama na kupoteza maelfu ya watu zaidi bilioni na nusu zilichangwa lakini cha kushangaza Serikali inatoa eti ubani laki moja kwa wafia, hizi fedha zinaenda wapi na zinatumika vipi,tumechoka na mikono ya rambi rambi, huu ni uzembe na kushindwa kwa Serikali kuwajibika.
Hivi kweli Serikali ya Mapinduzi na wale mabwana zao Tanganyika ni maskini wakushindwa kupata meli ya uhakika ya kusafirishia watu kwa usalama. Lakushangaza ni kwamba Serikali hii ya Tanzania ilinunua rada ambayo hatuna hata matumizi nayo kwa mabilioni ya fedha za kigeni kwa ajili gani,huku sisi binafsi hatuna hata ndege hivi si vichekesho. Fedha zile kama tungenunulia meli basi hata meli kumi zingelinunuliwa, vifaa vya uokozi, boti za kisasa hata ndege za uokozi majini , leo hii Zanzibar hata mafuta ya kutia kwenye mtumbwi hatuna, hii ni serikali au genge la wahuni linawaibia wananchi wasio na hatia.Kwa nini kama tuna serikali huru tushindwe kununua meli ? Kama hatuna uwezo basi hata kuomba tushindwe,mbona bajeti ya serikali inaomba nje ? Si aibu kuomba meli kwa wahisani kuliko siku zote kushuhudia vifo vya raia kwa uzembe.
Hivi Serikali ya Zanzibar itueleze sisi mbumbumbu hawa KM KM Zanzibar wanakazi gani.Nilifikiria kwamba moja ya kazi yao ni ulinzi wa Nchi ,mali,na usalama wa raia pia na suala la uokozi pale inapotokea majanga ya baharini. Leo hii Serikali ya Mapinduzi ndio askari wanaowatumia kwenye majukwaa ya siasa kuwazuia watu wanaodai haki zao na kupinga THulma za serikali na kudai taifa huru lao,kazi hizi kwa vikosi vya KM KM wapi na wapi Wazalendo! Serikali yetu isiwe hodari katika utesaji wa Raia bali iweke ufanisi katika kuimarisha maisha ya Wananchi wake na mali zao pamoja na usalama wao kama Binaadam huru. na hii ndio haki ya raia katika Nchi.

Serikali ijifunze,angalieni baada ya Serikali za kileo kupata taarifa za ajali tu, tayari mabalozi kutoka nchi husika wameshafika kusaidia Raia wao, lakini ndio kwanza serikali yetu inawashambulia raia wake kwa risasi za moto,maji ya muasho misikitini na kupiga mabomu misikiti, kuwadhalilisha vijana,jee hivi ndio kuwapenda raia zao au ndio hivyo munalinda maslahi yenu..?waangalieni hao mabalozi,hao ndio wenye Nchi,serikali huru ambazo hazikutawaliwa na wanaojua maana ya uongozi na thamani ya raia wao,jifunzeni. Imekuwa ni fahari kwa viongozi wa Afrika kusifiwa kwa mauaji,uzembe,ukatili na ulaji rushwa pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe,tamaduni hizi mpaka lini ?
Serikali zote mbili hazina imani na Wananchi wake na wala misiba hii inayotokea wao hawasikitiki wala hawashughuliki kwani kipindi hichi ndicho mavuno kwa baadhi ya Viongozi,zawadi za maafa zimeshaanza kutolewa muda si mrefu,matumbo yatajaa wanyonge wajinyonge kwa kuondokewa na wale wanaowapenda, vikosi vya askari vinaandaliwa kuwa tayari kuwakandamiza wavuja jasho.Hii yote ni kwamba wao misiba hii haiwagusi,kwani usafiri wanaotumia ni wa uhakika,pesa wanayotumia na hawa wanaozama na maboti mabovu kila uchao.
Baya zaidi imefika pahala Serikali yetu inasema haina dini lakini kila mtu ukimuuliza atakwambia dini yake na Mungu wake na sehemu anayoabudu,wakati huo huo tunaambiwa Serikali ni watu,sasa kama ni hivyo kwa nini Serikali isiwe na dini na serikali ni ya watu ?Lakini hapa utapata picha kwamba serikali hizi mbili ziko sahihi ,wao raia sio watu ni majuha na sisi hatuna maana kwao, kinachotakiwa hapa ni ulaji na ulwa wa madaraka tu.Ni wajibu wa Serikali kuona kwamba huku tunakoelekea ni kubaya na Wazanzibar wameshachoka,kwa maana hiyo ni vyema wakijiweka tayari kukabiliana na upinzani mkubwa kutoka kwa Wananchi hili sio siri,kila kitu kiko wazi, raia wanahitaji kuthaminiwa kama Nchi nyengine sio kuburuzwa mpaka kiyama.
Inapofika kuona Serikali inawadhalisha Raia zake na Nyumba za ibada na kuzinajisi, basi elewa Viongozi hao wameshaishiwa kilichobaki tusubiri bakora ya Mola wetu. Iwavyo naiwe lakini hatua ya Kiongozi Muislam,askari muislam kuingia kwenye Nyumba ya ibada ya Mola wake alomuumba na kuinajisi ni kuvuuka mipaka, jee Serikali na Viongozi wa Zanzibar wamejiumba au na wao pia wameumbwa?Kama ni hivyo basi waelewe kwamba hili ni jukumu lao, na iko siku watalijibu hili wakiwa peke yao,bila askari wa kuwalinda na wale wanao tuliza fujo.
Serikali zetu lazima zielewe kwamba wanaowaongoza sio mizoga bali ni wanaadam waliombwa na mola wao na wala hawana makosa ya kufanyiwa udhalilishaji kama huu unaoendelea hapa Zanzibar. Huu sasa sio uongozi bali ni ubabe na uhuni uliopita mpaka. Na hili kwa wote wahusika basi wasifikirie kwamba mola atawaachia hivi hivi tu bali hesabu yao itaanzia hapa dunia na kesho mbele ya haki, wanachokifanya serikali hii ya Zanzibar sio sahihi na mwisho wake utakuwa ni mbaya kwa Nchi yetu na kwa wao vile vile hili walielewe kwamba tunasafiri kwenye boti bovu pamoja na dalili za kuzama zote zimeshajitokeza,na vyombo vya uokozi havina mafuta tena.
Zaidi kinachonitia uchungu nikuona baadhi ya Mawaziri na Wabunge wanapopitisha bajeti zao wanaomba matrioni ya fedha za Wananchi, matokeo yake fedha hiyo inatumika kwa mambo ambayo hayana faida na Wananchi hao,Serikali ina agiza silaha zakuwauwa na kuwajeruhi raia zao. Hivi haya maji ya muasho na silaha za moto zinatengenezwa wapi Zanzibar ? Vitu vyote hivi vinatoka nchi za nje kwa fedha nyingi za Wananchi kuja kuwakandamiza lakini ikitokea ajali, mafuta ya kutia kwenye boti yanakosekana,sherehe za mapinduzi kila mwaka mabilioni ya pesa yanatumika kwa upuuzi,sasa hii ni serikali au ni genge tu la wababe, linawakandamiza wanyonge.
Hatuombi lakini kwa Serikali za kikandamizaji kama hizi zetu hatuna budi kuchimba makaburi tayari tayari ,kwani ajali kama hizi ZANZIBAR ni jambo la kawaida sasa,hatusomi kutokana na makosa yetu yaliopita bali vichwa vyetu vimejaa kutu,ubaya,uoga wa kuwaogopa mabwana zetu kudai haki zetu. Tusubiri tupewe siku tatu na Rais wa Tanganyika tuomboleze na bendera nusu mlingoni,huu kama si ujuha ni kitu gani, hii itasaidia nini kwa Wananchi ambao kila kukicha wanapoteza ndugu zao kwa uzembe wa Serikali mbovu.
Naamini kuna watu watachukia kwa hili lakini ukweli ni ukweli na utabakia kuwa ukweli, Zanzibar hatuna viongozi wala serikali. Tunavishwa vilemba vya ukoka na makoti makubwa tu. Sisi ni watawaliwa wa Serikali ya Tanganyika ndio maana hata hizo amri za kupigwa watu basi lazima zitoke kwenye serikali yaTanganyika,serikali yetu haihoji hilo.Hivi inakuwaje kama kweli tuna serikali SPIKA wa bunge Tanganyika ashindwe kusimamisha bunge kwa dharura pale ilipofika habari ya kuzama kwa meli. Tujiulize kama ajali ile imetokea Lake VICTORIA asingehairisha bunge hilo?Jee haya maombolezo mpaka atowe Rais kikwete na huyu Raisi kishein mamlaka yake kwa Wazanzibar yako wapi kama kiongozi wa nchi ?

No comments:

Post a Comment