Friday, July 27, 2012

ZANZIBAR ISHAKUWA SYRIA KWA SABABU HATUNA RAISI


Siku ya tarehe 20 july jumuiya ya uamsho iliamua kufanya sala ya maiti na dua maalum kwa ajili ya kuwaombea marehem waliofariki katika ajali ya kuzama kwa meli ya mv skigat karibu na eneo la kunduchi linalijuilikana kwa jina la fungu yasini, ambapo watu kadhaa walifariki, sala na dua ilifanyika katika msikiti wa mbuyun karibu na kiwanja cha mchezo wa mpira  wa miguu.
baada ya kumaliza jukumu hilo la ibada ya sala  na dua jumuiya ikaamua kutumia haki yao ya kimaumbile na kikatiba kuzungumza maneno machache yaliojikita katika hoja ambazo zina mashiko ya msingi ambayo ni haki ya  MZANZIBAR katika kuchanganua mambo muhimu yasio na majibu wala ufumbuzi wa hakika au wakudumu katika jamii yetu huku wakiwa katika hali ya amani kwa muda wote.
Ilipoendelea hali hiyo ghafla jeshi la polisi lilivamia na magari yapatayo sita yakiwa yamejaa askari polisi, mawili yakumwaga maji ya sumu yenye kemikali ya kuwasha  na moja iliyobeba majibwa na hatimae kuanza kutumia nguvu kubwa kuwahujumu  na kuwafanyia unyama mkubwa wananchi wasio na hatia
UNYAMA ULIOFANYIKA
1-Kuwaathiri kwa makusudi raia  wasio na hatia ndani ya majumba yao na kupelekea kuwahujumu vibaya watoto wadogo wa umri wa miaka 2,3,na 4, isitoshe wakawapiga  na kuwatishia kuwauwa wanawake na vijana wadogo wasiotambua chochote.
2-Mtoto mdogo mwenye umri wa siku kumi alihujumiwa na kuathirika vibaya uwezo wake wa kupumua kwa muda wa siku kadhaa.
3- vijana wa kiume walipigwa mateke ya nguvu na maaskari waliovalia viatu vizito, na wengine walipigwa maeneo ya kichwani kwa kutumia tako la bunduki.
4-Msikiti wa mbuyuni waliuchafua kwa kuumwagia maji ya najis,milango yalivunjwa madirisha,baskeli za raia wasio na hatia zilichukuliwa bila ya sababu ya msingi huu ni wizi na hati hawa ni askari. silaha zilipigwa kwa makusudi ndani ya majumba ya chini na ghorofa na kupelekea kuhatarisha kuwaka moto.
SHERIA  NA UHURU WA RAIA
Katiba  ya jamhuri ya muungano ibara ya 18. kila mtu
1-Anao uhuru wa kuwa na maoni  na kuelezea fakra zake.
2-Anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari habari bila ya kujali mipaka ya nchi.
3-Anao uhuru wa kufanya mawasiliano na kutoingiliwa kati mawasiliano yake.
4-Anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbali mbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.
 KATIBA YA ZANZIBAR, ibara 18.(1) bila ya kuathiri sheria za nchi kala mtu yupo  huru kuwa  na maoni yeyote na kutoa nje mawazo yake , kutafuta, kutoa habari na dhana kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia una uhuru wa mawasilano yake kutoingiliwa kati.
KWA HIYO WASHENZI HAWA WA SHEINI WAMEVUNJA KATIBA ZOTE MBILI.
MUONGOZO WA HAKI ZA BINAADAMU KWA POLISI
1-Kila mtu ana haki ya uhuru wa kufikiri na kujieleza, uhuru wa kujielezea ni muhimu kwani bila ya uhuru huo uhuru wa kufikiria hauna maaana.
2-kila mtu ana haki ya uhuru wa kufanya mikutano na watu wengine na kujumuika kwa amani.
3-Ni wajibu wa jeshi la polisi kuheshimu utu wa mtu na kusimamia na kuenzi haki za binaadamu za kila mtu.
Baada ya kuona sheria hizo na matukio yalivyotokea  ni wazi kwamba pametokea ukiukwaji mkubwa wa sheria ambapo inawezekana ulifanywa kwa makusudi kutimiza malengo fulani yalokusudiwa.
Kwa hivo waziri useyekuwa na wizara maalum Ali M Sheini unatakiwa uwe shahidi kwa wananchi mbele ya MOLA wa mbingu na ardhi dhidi ya uonevu na dhulma inayotendeka katika ardhi ZANZIBAR, inaaminika ya kwamba labda  yeye hahusiki na unyama huu ila baada ya hawa washenzi kufanya hivi si sio mara ya kwanza utawachukulia hatuwa ngani..? au utanyamaza tu kwa kuwafurahisha mabwana zako wa tanganyika.pia kuna kila dalili kwamba unyama huu unatekelezwa na Serikali ya Tanganyika.
Hivyo ni vyema ikaeleweka kwamba kwa shaka hiyo hatuna sababu kwanini
tusipate shaka ya kutokua na imani na KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR, INSPEKTA JENERAL WA POLISI na WAZIRI WA MAMBO YA NDANI.
Kwa hivo hakuna sababu ya kuiepuka tabia ya kimaumbile ya kukaribia kukosa uvumilivu na uonevu uliokithiri kwa raia wasio na hatia, hivyo jeshi la polisi lifate sheria kwani harakati za kupigania haki ya jamii hazatazimwa kwa nguvu za mabomu au maji ya muasho kwa hiyo harakati za haki zitasimama pale wanaostahiki haki kupata haki yao.
UBAGUZI WA KIDINI
Chakusikitisha ambacho kiko hadharani ni ubaguzi wa kidini ulioo ndani ya jeshi la polisi katika utendaji wake kwasababu haijawahi kutokea hatasiku moja kufanya kitendo cha kuvamia KANISA kwa kufanya hujuma kama hizo.Ajali na matukio ambayo yalisababisha kuathiri kwa makanisa Serikali ilitoa tamko kali na ilifidia uharibifu huo uliofanywa  na jeshi la Polisi na huku tukimuona Waziri mkuu  MIZENGO PINDA akitetea makanisa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
WAISLAMU wanajiuliza hivi waziri huyu anatumikia KANISA Tu..?
Ni jambo lakushtua na kushangaza jinsi unyama wa jeshi la Polisi walioufanya dhidi ya WAISLAMU katika maeneo yao ya makaazi na ibada ni kuona serikali zote mbili zimekaa kimya, hakuna tamko wala kemeo lolote dhidi ya jeshi la polisi hii inatuthibitishia sisi kuwa serekali zote mbili ni serekali za kanisa.na ndio maana serekali haikeme kupingwa mabomu misikiti na kunajisiwa na maji ya muasho na majibwa na polisi kuingia na viatu misikitini serekali zote kimya maana ni serekali za kanisa kisha munasema SEREKALI HAINA DINI WANAFIKI WAKUBWA.hata shein waziri asiyekuwa na wizara maalum alikemea na kuja kwenye TV na kurupoka mpaka anatokwa na kipovu cha mdomo ila sasa misikiti inanajisiwa kimebana kimya kama sio unafiki nini ..? Jumla ya watu zaidi ya 50 walikamatwa na wengine walitafunishwa mbwa, walipigwa na kupasuliwa vichwa, nakuathiriwa  vibaya kwa kipigo hicho, na kipigo kiliendelea mpaka ndani ya kituo cha polisi MADEMA, juu ya unyama huo uliofanyika hakuna mtu yoyote aliepatikana na hatia au kupelekwa katika vyombo vya sheria isipokua dhulma na unyanyasaji wa hali ya juu ndivo vilivotawala;;;;;
                 WAZANZIBAR WAMECHOSHWA NA MUUNGANO KWA NINI HAWAACHIWI WAPUMUE……………………………………….?
       WAZANZIBAR MNATAKA NINI?
     MNAUTAKA MUUNGANOOO?

No comments:

Post a Comment