Tuesday, August 7, 2012

ALI AMEIR NA AKILI ZAKE ZA MGANDO NIMEFAIDIKA NA MUUNGANO.JE ZANZIBAR IMEFAIDIKA NA NINI KATIKA MUUNGANO ALI AMEIR..?


Ali Ameir azushiwa kifo
KADA wa Chama cha Mapinduzi, Ali Ameir Mohamed, alikuwa kama mbogo baada ya kuzushiwa taarifa za kifo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi kuu ya CCM Zanzibar, Kisiwandui mwanasiasa huyo alielezea kukasirishwa kwake na taarifa na kusema kuwa ni za uongo.
Taarifa za kifo chake zimesambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (SMS).
Ali Ameir ambae katika siku za hivi karibuni amekuwa gumzo katika siasa za Zanzibar baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, alisema taarifa hizo zinazosambazwa na watu asiowafahamu ni za kipuuzi.
“Kufa anaeamua ni Mwenyezi Mungu, naweza kufa sasa au hata kesho na hizi si habari za kwanza kuvumishiwa, nilivumishiwa kifo wakati nilipokwenda matibabuni, lakini nilipogundua kuwa habari za sasa zimesambazwa hata kwa wanangu na jamaa zangu, nilishtuka sana,” alisema.
Mwanasiasa huyo mkongwe ambae aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, alisema habari za kifo chake pia zimetumwa kwa mtoto wake ambae yuko matibabuni, pamoja na ndugu yake anaemuuguza ambao zimewashutua sana.
“Mimi sijafa, ni hai, na kwa uzima nilionao siku hizi ni mzima kweli kwa sababu hata gari naweza kuendesha, nimekuja hapa mjini nikiwa najiendesha mwenyewe, mimi nipo kwetu Donge,” aliongeza Ali Ameir.
Alisema ujumbe huo huenda unasambazwa watu wenye siasa chafu, lakini akasisitiza kuwa hilo halitamzuia kutoa maoni yake kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hadi hapo atakapoondoka Duniani.
“Kama mtu anakasirika na ninachokieleza aniambie mie, wasiwabugudhi wanangu, watu ninao pingana nao kisiasa na wao wana watoto wao lakini siwaingilii na nawaheshimu kabisa, wawaachie wanangu waeandeshe shughuli zao, msiwabugudhi, hizi ni siasa za kijinga” alisema.FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI TUNAKULIZA JE WATOTO MULIO WAULIA WAZAZI WAO NA KUWANAJISI MAMA ZAO NA DADA ZAO WAKATI WA MAPINDUZI 1964 UTAWAMBIYA NINI ALI AMEIR..?KUMBE MTOTO ANAUMA EYEE ALI AMEIR..?
“Kama wanafanya hivi ili ninyamaze basi sitanyamaza, nitaendelea kutoa msimamo wangu na nitajihidi nisikiuke msimamo na sera za chama changu, lakini nitakapokiuka misimamo ya chama nina hakika chama changu kitaniita,” alisema.
Akizungumzia kuhusu muungano alisema, yeye angependa muungano uwe imara zaidi na uwe katika mfumo ambao umeasisiwa na viongozi wake.
“Mimi ni mmoja wa watu niliefaidika na muungano na nitasema wazi kweupe mchana,” alisema.
Hata hivyo, alisema wapo watu wanaojaribu kuvuruga chama na Muungano kwa kuwa semea wananchi kwa maslahi yao binafsi.

No comments:

Post a Comment