Saturday, August 11, 2012

ASEMA YEYE NI PROFESA MBONA MANENO YAKE KAMA POJO KAMA YA BABA YAKE NYERERE


Assalam Alaykum Wazanzibari na Wazalendo wenzangu wa Nchi hii.
Binafsi nimeshawishika kuandika makala hii baada ya kuona kumeanza kuzuka kundi ambalo “LINAPOTOSHA UKWELI KWA KUTUMIA KASUMBA” na kukandamiza mawazo na maoni ya wazanzibari juu ya mustakbali wa Nchi yao na hasa wale wengi wanaodai “MFUMO MPYA WA MUUNGANO WA MKATABA”.
Binafsi pia, naamini kabisa kundi hili lililoanza kuonesha ngozi yao halisi ya kutaka daima kuiona Zanzibar inabaki ilipo sasa limeanza kupinga vikali “MFUMO WA MUUNGANO WA MKATABA” baada ya kuona asilimia kubwa ya maoni ya wazanzibari wa mikoa miwili iliyokusanywa maoni na Tume Ya Warioba; wengi wa wazanzibari wamependekeza mfumo huo, KUSINI UNGUJA ASILIMIA 47.4% na KUSINI PEMBA 75% ya watoaji maoni wamependekeza tuwe na mfumo huo wa mkataba huku Zanzibar na Tanganyika zikiwa na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa. Huku pia wakiona kwamba mikoa mitatu iliyobaki yaani KASKAZINI UNGUJA, KASKAZINI PEMBA NA MJINI MAGHRIB itakuwa na mawazo makali zaidi kudai mfumo huo pamoja na kudai mamlaka kamili ya Zanzibar kurudishwa kuzidi hata hiyo mikoa miwili ya kusini iliyomaliza kutoa maoni.
Napenda kwanza kumnukuu mmoja wa Maprofesa wa Tanzania, Profesa Shivji anasema hivi
“Nikitoa mfano nikasema kwamba kuna taarifa kwamba chama kimoja huko Zanzibar kinapandikiza pendekezo la ‘muungano wa mkataba, sio wa katiba’ bila ya kueleza waziwazi maana yake” mwisho wa kunukuu.
Hivi nimuulize Profesa Shivji ni chama gani kinapandikiza pendekezo hilo??? Hilo la kwanza maana ninavyofahamu vyama vikuu Zanzibar vina sera za serikali mbili na serikali tatu. Pili Jee kwani kuna ubaya gani ikiwa kutakua na watu wanaopendekeza mfumo huo ikiwa ni kwa ajili ya kuweka misingi bora ya Muungano na kuyajali maslahi ya mataifa yote mawili ya Muungano???
Profesa Shivji anaendelea kusema
“Ukweli ni kwamba huwezi ukawa na Muungano wa mkataba bila kwanza kuuvunja Muungano. Kwa hivyo, wanachoshawishi moja kwa moja ni kuuvunja Muungano. Basi waseme hivyo badala ya kujificha nyuma ya pazia la ‘muungano wa mkataba” mwisho wa nukuu.
Hapa ndio hasa lengo langu mana hata jana niliona makala pia kuna bwana aitwa mgaza amekuwa na mawazo hayo pia.
Prof. Shivji na wenzako wenye mawazo kama yako mimi motto mdogo sana nikuulize “HIVI KUNA UBAYA GANI WA KUVUNJA MUUNGANO NA KUEKA HUO MKATABA IKIWA HAYO NDIO MAONI YA WAZANZIBARI WENGI NA IKIWA KWELI KUNA NIA YA DHATI YA KUANDIKA KATIBA MPYA???”
Profesa Shivji anaendlea kusema hivi
“Tukianza kubaguana kati ya Watanganyika na Wazanzibari, tutaendelea kubaguana kwa msingi wa Uislamu na Ukristo, na Usukuma na Uchaga, Uarabu na Uafrika, weusi na weupe bila kikomo. Kama alivyosema Mwalimu, ukishaonja nyama ya mtu basi utaendelea kuila kila siku” mwisho wa kunukuu.
Hiyo ndio KASUMBA PANDIKIZI KUWANYAMAZISHA WAZANZIBARI WASIDAI UTAIFA WAO NA NCHI YAO,ATI ANASEMA NINI AU NA YEYE ANAJIFANYA NYERERE ILI WAZANZIBAR WASIDAI HAKI YAO NYERERE KAFA NAKILI KAZICHUKUWA NYINYI MLIOBAKI KASUMBA TU MBONA HUKUTAJA UKIRISTO NA UISLAMU UHINDU NA UPAGANI UHINDI NA URABU NA UAFRIKA..?) Mtu kama Profesa sikutarajia kumsikia anaongelea pumba kama hii ila sasa ndio tunajuwa kuwa sio wote ni profesa wengine hununuwa vyeti kisha wakajiita maprofesa haahaha kwa kweli kuna utata hata wa elimu aliyonayo au hitendei haki elimu yake kwa kutaka kuficha ukweli kwasababu nia ya wazanzibari haipo katika hilo bali wazanzibari wengi wamejikita katika kudai maslahi yao na taifa lao baada ya vurugu kubwa walizotendewa na Muungano huu uliopo chini ya mfumo wa serikali mbili (KUELEKEA MOJA).
MAPENDEKEZO YANGU BINAFSI JUU YA HAWA WANAOPINGA MKATABA NA MADAI YA WAZANZIBARI.
KWANZA: Ninawaomba wazanzibari waendelee na Umoja wao walionao pamoja na kudai maslahi ya taifa lao wazi wazi bila ya kuficha na pia kutoweka mbele kasumba zinazopikwa na itikadi za kivyama, ikiwa tutaendlea na msimamo tuliouonesha katika kipindi hiki cha miaka miwili ni imani yangu ZANZIBAR HURU itapatikana inshaallah bila wasiwasi wowote.
PILI NALIOMBA BARAZA LA WAWAKILISHI LIFANYE MAREKEBISHO YA KATIBA YETU KABLA MCHAKATO WA KATIBA MPYA KUMALIZIKA.
kwa vile katiba yetu inasema katika utangulizi:
“NA KWA KUWA tunazingatia na kuthamini kazi nzuri ya Kimapinduzi iliyofanywa na Viongozi wa Mapinduzi, wakiongozwa na Mwasisi wa Chama cha ASP na Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, ambaye fikra zake zitaendelezwa na kudumishwa daima, kizazi baada ya kizazi katika kupambana na Ukoloni, Ubepari Unyonge, Uonevu na Dharau, na badala yake kudumisha Uhuru na Umoja, Haki na Usawa, Heshima na Utu;”
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar miaka iliyopita ilimuagiza Jaji Zuru kuipitia Katiba ya Zanzibar na kupendekeza marekebisho ikibidi. Jaji Zuru amesema katika ripoti yake kuhusu kifungu cha (1) cha Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza ya Katiba ya Zanzibar kuwa:
“Mtu akisoma kwa makini Utangulizi (Preamble) na Katiba yote kwa jumla, ataelewa kwamba Zanzibar ni dola yenye mamlaka yake kamili (sovereign state) na kwamba wale waliotunga Katiba hii hawakuwa na nia ya kusalimisha na kuachia mamlaka (sovereignty) ya Zanzibar wakati wa kuundwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, ambao ulizaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Haya yanaelezwa wazi katika kifungu cha 9 cha Katiba ya Zanzibar kinachosema,
“9.-(1) Zanzibar itakuwa ni nchi ya kidemokrasia na haki za kijamii.
(2) Kwa hiyo hapa inaelezwa rasmi kwamba:-
(a) Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba utatoka kwa wananchi wenyewe.” Mwisho wa kumnukuu.
Kwavile tayari tumeshabadilisha kipengele cha sura ya mwanzo ya katiba yetu kinachoitambua Zanzibar kama ni Nchi, naomba kwa sasa pia tufate mapendekezo ya jaji Zuru, kipengele hicho cha mwanzo kisomeke hivi:
“Zanzibar ni, na itabaki dola yenye mamlaka………………………” kwa kiengereza “”Zanzibar is and shall remain a sovereign state……………………”
kwasababu bado Marekebisho ya kumi ya katiba yetu hayatambui kama Zanzibar ni Dola na hata Ibrahim Mzee katika semina za Baraza la Wawakilishi alisema kwamba Zanzibar ni Nchi lakini si Dola.
Hapo kwa mawazo yangu ndio hawa Watanganyika wametuletea Katiba Mpya kuja Kumeza Hicho ili tubaki kujigamba ni Nchi kumbe mamlaka hatuna.
Nawaomba wazalendo pia wasome makala ya NAFASI YA ZANZIBAR KATIKA MUUNGANO
Jamhuri ya Watu Wa Zanzibar Kwanza.

No comments:

Post a Comment