Sunday, August 26, 2012

KILEMBWE CHA FIRAUNI AKUBALI KUHISABIWA KATIKA SENSA


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameendelea kuinasihi Jamii Nchini kujiandikisha katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza usiku wa kuamkia leo ili kupata Takwimu sahihi zitakazoliwezesha Taifa kupanga Mipango bora ya Maendeleo.
Nasaha hizo alizitoa mara baada ya kuandikishwa katika dododso la Sensa ya Watu na Makazi akiwa mkuu wa kaya yake wakati akizungumza na Waandishi wa Habari hapo kwenye makaazi yake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif akiwa pia Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na makazi Tanzania ya mwaka 2012 alisema Serikali lazima iwe na Takwimu za uhakika na ndio maana suala la kuhesabiwa likawa la lazima kwa mujibu wa sheria za Takwimu.
Alisisitiza kwamba tabia ya baadhi ya watu au vikundi kutumbukiza kila kitu katika siasa inaweza kuathiri maendeleo ya jumla ya Taifa na matokeo yake kuipelekea Jamii katika maangamizi.
“ Kama hatutafanikiwa katika zoezi la sensa ni kusema kwamba tumeathirika vibaya Kimaendeleo na kamwe tusidhani kuwa Maendeleo yanayozungumzwa kila mara yanalengwa kwa watu au kikundi maalum”. Alifafanua Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikemea kitendo cha Baadhi ya makarani kutoandika katika madodoso waliyokabidhiwa na badala yake wameanzisha vitendo vya kuandika kwenye vikaratasi.
Alisema tabia hiyo inakwenda kinyume na utaratibu waliopangiwa na waelewe kwamba wanajibebesha dhima kwa vile tayari wamekubali kula kiapo cha uaminifu katika kufanya uadilifu kwenye jukumu walilokabidhiwa.
“ Inasikitisha kuona Makarani hao wamekubali kufanya kazi hizo kwa uadilifu baada ya kula kiapo lakini matokeo yake wanakwenda kinyume na taratibu za kazi”. Balozi Seif alielezea mshangao wake kutokana na vitendo hivyo.
Akizungumzia baadhi ya Vikundi vya Kidini vilivyokuwa vikipinga zoezi hilo Balozi Seif alitahadharisha kwamba hata vitabu vya dini zenyewe vimeamuru na kusisitiza umuhimu wa kuhesabiwa.
Alisema wana dini wanaokataa kuhesabiwa waelewe kwamba wanakwenda kinyume na maamrisho ya dini yenyewe.
“ Sababu za kidini katika masuala haya yanayopigiwa kelelele na baadhi ya vikundi vya kidini zinaonekana ni za juu juu, lakini liko suala la ndani lililojificha ambalo linalooneka kuwa zaidi la Kisiasa ”. Alitanabahisha Balozi Seif.
Mwenyekiti huyo mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania alisema huduma zitakazotolewa na Taifa katika kuwapatia Wananchi na Jamii yote baada ya kuwa na Takwimu haitachaguwa watu au Vikundi vya Dini.
“ Taifa litakapojiandaa kusambaza huduma za Kijamii ndani ya maeneo itaelewaje idadi ya watu na maeneo hayo kama hakukuwa na Takwimu sahihi za watu na ukubwa wa eneo husika?”. Alihoji Balozi Seif.
Alielezea faraja yake kuona zoezi la uandikishaji wa sensa ya watu na makazi katika maeneo kadhaa Nchini linaendelea kwa amani na utulivu na kuiomba Jamii kuiendeleza hali hii kwa faida ya Wananchi wote.
Akitoa shukrani kwa Niaba ya Uongozi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mratibu msaidizi wa Sensa Mkoa Mjini Magharibi Bibi Sabina Raphael Daima alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa mashirikiano yake aliyoyatowa kwa makarani wa Sensa wakati wa kuandikishwa kwenye dodoso la Sensa.
Bibi Sabina aliomba kitendo cha ushirikiano wanachoendelea kukishuhudia kwa Viongozi mbali mbali wa ngazi za juu wa Serikali na hata wa Vyama vya Siasa kwa makarani wao wa Sensa kinafaa kuwa changa moto kwa Wananchi wote Nchini.
NYINYI LAZIMA MUKUBALI KUHISABIWA ILI KUHIFADHI TONGE ZENU TUNAWAJUWA NI WANAFI WAKUBWA.

No comments:

Post a Comment