Monday, August 20, 2012

KISHEIN CHATUMIA AYAA ZA QURAAN KWA MANUFA YAKE

  ATAKUWA RAISI WA ZANZIBAR AKIVUNJA MUUNGANO NA ZANZIBAR KUWA NA MAMLAKA KAMILI KAMA SIO HIVYO YEYE ATABAKI KUWA WAZIRI ASIYEKUWA NA WIZARA MAALUM NDIVYO WATANGANYIKA WALIVYO MFANYA NA YEYE KAKUBALI SASA RAISI RAISI RAISI NGANI HATA HAWEZI KUNUNUWA VISHETI KENYA MPAKA APEWE RUHUSA NA DODOMA

HOTUBA YA WAZIRI ASIYEKUWA NA WIZARA MAALUM WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI,
MHESHIMIWA DK. ALI MOHAMED SHEIN, KATIKA BARAZA LA IDD EL FITRI MWEZI MOSI MFUNGUO MOSI, 1433 HIJRIYA, AGOSTI, 2012
Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad,
Makamu wa Kwanza wa Rais;
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi,
Makamu wa Pili wa Rais;
Mheshimiwa Dk. Amani Abeid Karume,
Rais Mstaafu wa Zanzibar;
Mheshimiwa Sheikh Saleh Omar Kabhi,
Mufti wa Zanzibar;
Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho,
Spika wa Baraza la Wawakilishi;
Mheshimiwa Omar Othman Makungu,
Jaji Mkuu;
Mheshimiwa Sheikh Khamis Haji Khamis,
Kadhi Mkuu;
Waheshimiwa Mawaziri,
Waheshimiwa Mabalozi,
Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Ndugu Wageni Waalikwa,
Ndugu Wananchi,
Mabibi na Mabwana.
Assalam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh
IDD MUBARAK WA KULLU AAM WAANTUM BIKHEIR
Nakupeni mkono wa Idd na natanguliza shukurani kwa kukariri kwamba “sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake vyote vilivyomo Mbinguni na Ardhini. Na Akhera, sifa njema ni zake pia; Naye ni Mwenye Hekima na Mwenye Ujuzi wa kila jambo”.
Katika Aya ya pili ya Surat Saba’ai, Mwenyezi Mungu amesema: “Anajua yaingiayo katika ardhi na yatokayo humo; Naye ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu”.
Nimetanguliza aya hii kwa makusudi wakati ambapo tumo katika sherehe za Idd baada ya kumaliza Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mwezi unaoitwa Mwezi wa Mwenyezi Mungu. Huo ni mwezi ambao tumetekeleza amri ya Mola wetu ya kufunga kama ilivyoelezwa katika Surat Al-Baqarah, katika aya maarufu kwetu sote. Tunatarajia Msamaha na Rehma zake.(HUSAMEHEWI MPAKA URUDISHE ULICHOKITHULUMU SHEIN)
Katika kutekeleza amri hii ya kufunga sisi walengwa wa amri hiyo, yaani Waumini wa Uislamu tumepita katika kipindi ambacho kinaweza kufananishwa na kipindi cha mafunzo na utoaji huduma katika Uislamu ambacho kinakuja mara moja katika mwaka. Matokeo ya mafunzo hayo ni kuibuka kwa umma wa Waislamu ambao wanamjali Mola wa Walimwengu wote, viumbe wenye utaratibu katika maisha yao na wenye nidhamu ya hali ya juu.
Ndugu Wananchi,
Bila ya shaka yo yote, mwanafunzi huwa na haki ya kusherehekea baada ya kumaliza mtihani na kutegemea kufaulu. Kwa hivyo, sisi tukiwa tumekamilisha kuufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, tuna kila sababu ya kusherehekea. Kwa hivyo, kwa ukarimu na rehma zake Mwenyezi Mungu nasi tunataraji kuwa tutafaulu, kama ilivyosema ile aya niliyoitaja. Lakini mjuzi wa yote haya ni Mwenyezi Mungu. Katika kusherehekea sikukuu hii, tuzingatie mafunzo tuliyoyapata kwenye mwezi wa Ramadhan; kwa kutofanya vitendo vya maasi. Tuwe watiifu na tuwe waadilifu na tuzingatie sheria za nchi.(SIO SHERIA ZA NCHI SHERIA ZA M/MUNGU SHEIN)
Sherehe zetu kubwa ni sikukuu mbili za Idd ambazo ni Idd el Fitr na Idd el Hajj. Kwa mnasaba wa Idd hii ya kwanza nitazungumzia kidogo juu ya mafunzo tuliyopata na baadae kugusia maana ya kusherehekea lakini kabla ya hapo natoa pongezi kwa waumini wote kwa kumaliza Mwezi Mtukufu kwa staha ifaayo. Nchi yetu ilifurahia amani na utulivu na hata wageni waliokuwepo wakati huo wamesikika wakitoa sifa. Wote waliotunza amani ya nchi yetu wanastahiki pongezi. Aidha, natoa salamu zangu za Idd kwenu na kwa wananchi wote, Zanzibar na Tanganyika (Tanzania Bara.) Huu ni wakati wetu wa kufurahi na kushereheka baada ya Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Lakini wakati huo huo tupitie mafunzo tuliyopata katika mwezi huo Mtukufu wa Ramadhan na tuwe tunafaidika nayo.
Ndugu Wananchi,
Mafunzo makubwa kutokana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, baada ya ibada ya saumu na kuwania ucha Mungu kwa njia mbali mbali, ni yale ya kuwa watu wenye utaratibu mzuri na wenye nidhamu ya hali ya juu. Binaadamu mwenye sifa hizi ni mtu aliyekamilika kiutu.(SHEIN WEWE HUNA NITHAMU WAKWANZA BAADA YA KUTOWA AMRI WAISLAMU WAPINGWE MABOMU MSIKITI WA MBUYUNI)
Utaratibu na nidhamu tuliyojifunza ulitokana na utiifu. Sote tulitii amri za Mola wetu. Utiifu ni jambo ambalo limetajwa katika Quran tukufu mara 13. Kwanza limetajwa katika Surat Al Imran, Aya ya 132; “Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa”. Tena limetajwa katika Surat An Nisaa Aya ya 59:”Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu, walio katika nyinyi. Na kama mtakhitilafiana juu ya jambo lo lote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Hiyo ndiyo kheri, nayo ina matokeo bora kabisa”.(MBONA WEWE HUKUTAKA KURUDI KWA MWENZI MUNGU NA KUZUNGUMZA NA UAMSHO..? )
Ndugu Wananchi,
Kuamrishwa kuwa na utiifu kuna sababu zake. Kutokana na hilo tunafikia zile sifa za kuwa watu wenye utaratibu wa mambo na pia kuwa na nidhamu ya hali juu kabisa na kutuwezesha kufanikiwa katika maendeleo ya maisha yetu. Sifa hizo zinatupelekea katika maisha bora kabisa.
Ndugu Wananchi,
Katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan, wengi wetu tulikuwa watiifu wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu na matokeo yake tulikuwa na mshikamano, umoja, unyenyekevu, ukweli, wenye upendo na kusaidiana. Tulikuwa na utulivu wa nafsi na hatukuwa waropokaji wa mambo bila ya kufikiri na kuzingatia.
Ndugu Wananchi,
Jambo la kwanza ni kukumbushana na kusisitiza suala zima la umuhimu wa kulinda na kuendeleza amani, utulivu na mshikamano wetu ambao ndio siri kubwa ya mafanikio tunayoendelea kuyapata. Nimeamua kutumia fursa hii kwa kuzingatia uzito wa siku ya leo kwa Waislamu wote na wananchi kwa jumla na kwa kuzingatia amri ya Mwenyezi Mungu katika Quran aya ya 55 ya Suratul Adh-Dhaariyat aliposema:
“Na endelea kuwakumbusha; maana ukumbusho huwafaa walioamini”.
Jamii yetu ni ya watu waliochanganyika sana, iwe kwa ndoa, kusoma pamoja, kufanya kazi pamoja, kusali pamoja au hata kukutana mara kwa mara katika shughuli mbali mbali za kijamii na za kimaisha. Katika hali kama hii tunapaswa kuihisi hali ya umoja tulionao ambao ndio utakaotuwezesha kupanga mipango mbali mbali na kuitekeleza kwa kushirikiana na Serikali kwa manufaa yetu na nchi nzima kwa jumla. Ni dhahiri kuwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, vikundi na maendeleo yanayoletwa na Serikali kwa ajili ya watu wake hayawezi kupatikana bila ya kuwepo hali ya amani na utulivu nchini. Haya yote yanatokana na utiifu, utaratibu na nidhamu katika maisha.
Ndugu Wananchi,
Katika siku za hivi karibuni, nchi yetu imekabiliwa na viashirio vya kuondoka kwa amani, utulivu na mshikamano. Katika kipindi hiki tumeshuhudia matukio mawili makubwa lile la tarehe 26, 27 na 28 Mei na la tarehe 20 Julai, 2012. Matukio haya yameitia doa jamii yetu na nchi yetu ambayo imejijengea sifa nzuri ya amani na utulivu. Wahenga walisema “Thamani ya amani anaeijuwa Yule iliyemponyoka”. Kuvuruga amani ni jambo la muda mfupi sana lakini kuirudisha inachukuwa muda mrefu. Aidha, kuvunjika kwa amani husababisha athari ya vitu na watu wasio na hatia. Natoa wito kwa wananchi wote kuepuka vitendo vya uvunjaji wa amani na vinavyopelekea kuathiri watu na mali zao.(TOA WITO PIA KWA WASHENZI WAKO MAPOLISI WANAO NYANYASA WATU BILA YA HATIA)
Tunapaswa kuelewa kwamba vitendo kama hivi vinaathiri sana jitihada za nchi yetu katika shughuli za maendeleo na ukuaji wa uchumi hasa katika kuimarisha sekta ya utalii ambayo tumeamua kuiimarisha kwa kauli mbiu ya “utalii kwa wote” inayoambatana na mipango madhubuti. Matukio kama haya yanasababisha kuwakimbiza wageni wanaopenda kututembelea. Sote tunaelewa kwamba uchumi wa nchi yetu unategemea sana utalii ambao kwa sasa unatupatia karibu asilimia 80 ya pato letu la fedha za kigeni.(PESA ZA KIGENI AU PESA ZA KHARAMU SHEIN) Baadhi ya nchi zinazojulikana katika utalii kama vile Seychelles na Mauritius zinaendelea kupiga hatua na kutuacha nyuma. Tufanye kila jitihada kwa lengo la kuimarisha sekta ya utalii ili tusiachwe nyuma zaidi katika uchumi wetu na maisha ya watu wetu.
Ndugu Wananchi,
Napenda kutumia fursa hii kuwatanabahisha wanaopanga na kushabikia vitendo vya uvunjaji sheria, amani na utulivu kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa itaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa wale wanaosababisha vurugu na kukiuka taratibu za kisheria.(SHEIN SHEIN UNAMTISHA NANI HAKUWA GADDAF NA MAPESA NA JESHI NA WAMEMNGOWA ITAKUWA WEWE KIBARAKA CHA TANGANYIKA) Hata hivyo, napenda kuwanasihi wananchi wasijiingize kwenye vitendo vinavyopelekea kuvunjika kwa amani na badala yake wafanye mambo ya uadilifu yanayozingatia sheria ziliopo na maadili yetu.
Serikali ina wajibu wa kulinda haki na uhuru wa wananchi wake na mali zao. Kwa mara nyengine tena nalipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri walioifanya ya kutuliza fujo zilizotokea.(KAZI NZURI YA KUPIGA MABOMU MISIKITI NA KUCHOMA MAZULIA,KAZI NZURI KUPIGA WANAWAKE WA KISLAMU NA KUWAVUWA HIJABU,KAZI NZURI KUWATAFUNISHA WASLAMU WENZAKO KWA MAJIBWA NA KUWANAJISI,KAZI NZURI POLISI WAKO KUIBA VYOMBO VYA RAI WASIO NA HATI KAZI NZURI KISHEIN.
Ndugu Wananchi,
Tafauti ya mawazo na mtazamo baina yetu, isiwe chanzo cha vitendo vya kuvunja amani na kutofuata sheria. Nchi yetu inaongozwa na Katiba na sheria zinazozingatia misingi ya utawala bora,(BASI WEWE SHEIN MWENYEWE HUZINGATI KATIBA INASEMA UNAWEZA UKAITISHA KURA YA MAONI MBONA HUITISHI..? KATIBA INASEMA SEREKALI ITAENDESHWA NA WANANCHI NA WANANCHI HAO NDIO WALIOPIGA KELELE UVUNJWE MUUNGANO MBONA HUVUNJI..?WEWE HUFUATI KATIBA UNAFUATA DODOMA ASYEJUWA NANI KISHA UNAHIMIZA WATU KUFUATA KATIBA KISHEIN.) utamaduni, mila na silka tulizoachiwa na wazee wetu za kustahamiliana na kuvumiliana kwa maslahi ya nchi yetu. Misingi hii ndiyo iliyotuwezesha kufika hapa tulipo na kusifiwa na marafiki zetu mbali mbali wa nchi za nje, majirani zetu na watalii wanaokuja kututembelea. Kwa hivyo, ni vyema tuuendeleze ustaarabu huo. Tutumie busara katika kuyatatua matatizo yetu yanapotokea, kwa njia ya mazungumzo.(KISHEIN WEWE HUKUTUMIA BUSARA BALI ULITUMIA WASHENZI WAKO WA KIKURIA NA ASKARI WAKIZENJI WAKIHAFIDHINA KUWASULUBU WAZENJI) Hii ndio njia peke yake itakayoleta maelewano pale yanapokosekana. Mambo yote yanazungumzika. Hapana lisilozungumzika. Zanzibar tunao uzoefu mkubwa katika kuutekeleza utaratibu huu. Kila mmoja wetu ana wajibu wa kuzingatia utekelezaji wa haya ninayoyaeleza. Hili ni jukumu letu sote, viongozi na tunaowaongoza; tuliopo Serikalini na waliopo kwenye taasisi na asasi zisizokuwa za Kiserikali.
Lazima tushirikiane katika kuiendeleza amani na utulivu nchini ili iwe chachu ya kusukuma mbele maendeleo ya nchi yetu kwa haraka. Hapana njia yoyote ya mkato itakayotusaidia katika kuijenga na kuiendeleza nchi yetu kwa haraka sana isipokuwa kufanya kazi kwa bidii, kushirikiana, kupendana, kuendeleza amani na kuendeleza umoja wenye nguvu.(KAZI SHEIN ZIKO WAPI BANDARINI MACHOGO,AIRPORT MACHOGO,POLISI MACHOGO,JESHI MACHOGO) Tukumbuke usemi maarufu usemao umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu(SHEIN UNGANA NA UAMSHO ZANZIBAR IJITAWALE YENYEWE BASI MBONA UNAWATENGA NA KILA  KUKICHA WANAKUHISHIMU NA KUSEMA WEWE NI RAISI MZURI ILA WEWE UNAWAPIGA MABOMU UNGANA NAO BASI KAMA UMOJA NI NGUVU..?). Mwenyezi Mungu analitilia mkazo suala la umoja, mshikamano na kustahamiliana katika aya mbali mbali katika Quran ikiwemo aya ya 46 ya Suratul Al Anfal aliposema.
“Na Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake wala msizozane (msigombane); msije mkaharibikiwa na kupotea nguvu zenu, na vumilianeni (mstahamiliane). Bila shaka Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaovumiliana”
Hizi ni sifa ambazo leo tunapokuwa tunasherehekea Idd el Fitr tunapaswa kuzizingatia na kuamua kuziendeleza katika maisha yetu ya baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Huu ni ufunguo wa maendeleo ya binaadamu.
Ndugu Wananchi,
Ni dhahiri kwamba katika kipindi kifupi tangu muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Umoja wa Kitaifa ulipoanza, nchi yetu imeweza kupiga hatua kubwa katika nyanja mbali mbali za kijamii na kiuchumi. Mafanikio hayo yamepatikana kutokana na viongozi na wananchi kuishi kwa kushirikiana na kuvumiliana kisiasa. Kwa upande wa Serikali, viongozi tumekuwa na ushirikiano wa karibu ambapo tunafanya kazi kwa kuzingatia misingi ya katiba, sheria na kuheshimiana kwa manufaa ya nchi yetu. Maendeleo katika sekta ya miundombinu, elimu, afya, kilimo na kadhalika yameimarika ni kwa sababu tumeanza vizuri na jitihada zinaonekana. Aidha, misingi ya demokrasia na uwajibikaji imezidi kuimarika. Natoa wito kwa wananchi wote muendelee kushirikiana na Serikali yetu katika kuyaendeleza mafanikio hayo.
Ndugu Wananchi,
Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata mafunzo mazuri katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kwa hivyo, hatuna budi kutekeleza kwa dhati a suala la mani, utulivu na utiifu wa sheria ambazo zinaendana na utaratibu na nidhamu katika mambo yetu ndani ya jamii na nchi nzima kwa jumla.
Utaratibu ni ustaarabu ambao unaanzia kwa mtu binafsi na kwenda mbele hadi kufikia katika familia yake, jamii na hatimaye nchi nzima. Kama tunavyojua, miongoni mwa utekelezaji wa sifa ya utaratibu ni kuwa na mipango. Kila mmoja wetu anajipangia nafsi yake, familia yake na anapaswa kushiriki kupanga katika jamii na nchi nzima kwa jumla. Kuchangia katika maendeleo ya nchi ni wito ambao unatokana na ile aya ya utiifu niliyoitaja kabla na ni jukumu letu sote, kwani Wahenga wamesema, “Kidole kimoja hakivunji chawa”.
Nachukua fursa hii kuligusia jambo la pili muhimu ambalo linalotukabili katika kutekeleza sifa za utaratibu wa maendeleo ya nchi. Katika kipindi cha wiki moja ijayo, nchi yetu itakuwa na zoezi la kuhesabu watu, yaani sensa, zoezi ambalo ni miongoni mwa utaratibu wa kupanga maendeleo ya wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yo yote. Kushiriki katika sensa ni jambo la sheria na ni zoezi ambalo nchi zote duniani zinalifanya kila baada ya miaka kumi (10) isipokuwa kama itatokezea sababu isiyoweza kuepukika. Matokeo ya sensa yanazipa Serikali taarifa halisi juu ya idadi ya watu na mambo mengine muhimu katika kutayarisha mipango ya maendeleo.(UMESEMA UMOJA NI NGUVU SASA ZANZIBAR WANAUNGANA NA WAISLAMU WENZAO WA BARA KUTO KUSHIRIKI SENSA WEWE BADO UNAIPIGIA DEBE KWA NINI NA WEWE HUWAUNGI MKONO NDIO UMOJA HUO AU WEWE SIO MUISLAMU.)
Kwa hakika inasikitisha kusikia kuwa kuna baadhi ya watu wanaowashawishi wenzao wasikubali kuhesabiwa kwa visingizio visivyokuwa na msingi.(ASTAHAFIRU SHEIN RUDI KWA MOLA WAKO KISINGIZIO HAPA NI CHA DINI WEWE SIO MUSLAMU NINI..?) Tutakumbuka kuwa nchi yetu imeshafanya zoezi la sensa kwa vipindi mbali mbali huko nyuma kwa ufanisi mkubwa bila ya kuwepo kisingizio chochote katika suala hili.(NATOKA TUFANYE HIZO SENSA MIAKA YA NYUMA NIMENDELEO NGANI SISI WATU WA CHINI TULIYO PATA KISHEIN ZAIDI YA UMASIKINI NA NYINYI MAJAMBAZI WAKUBWA MUNAZIDI KUTAJIRIKA NA KUZA MAJUMBA MAKONGWA KWA WAZUNGU ILI WAJENGO HOTELI ZA LANA NA ULANISI) Mafundisho ya dini zote hayapingi suala la kuhesabiwa kwa nia ya kupanga na kuleta maendeleo ya wananchi.(MAWE HAKUNA MAENDELEO YOYOTE ZAIDI YA KURAHISISHA NYINYI VIPI MUTAIBA VIZURI PESA ZA SEREKALI)
Kwa hivyo, natoa wito kwa wananchi wote kutekeleza wajibu wao kwa kushiriki kikamilifu na kuhakikisha kuwa wanahesabiwa siku ya tarehe 26 Agosti, 2012. (HATUHISABIWI KWANI SISI KUKU WA GREDI AU NGOMBE WA WAMASAI HATUISABIWA MPAKA TUPATE NCHI YETU KISHA TUTAJIHISABU WENYEWE JIHISABUNI NYINYI VIONGOZI MUNAO IBAA PESA ZA SEREKALI)Tukiwa Wazanzibari tuwajibike kufanikisha zoezi hili muhimu la kisheria kwetu na tusiwape nafasi wasiotutakia mema katika mafanikio ya nchi yetu.
Ndugu Wananchi,
Leo ni siku ya Idd. Hii ni siku ya kwanza ambapo Muislam humrejea ruhusa yake ya kula na kunywa baada ya kujizuia navyo mchana kutwa katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan, akiwa amejitolea kwa ajili ya kupata radhi na msamaha wa Mwenyezi Mungu.
Kadhalika, leo ni siku ya kwanza baada ya Ramadhan, ambayo Muislam anahisi furaha mbili kubwa; furaha ya kutekeleza wajibu wa kutii maamrisho ya Mola wake na furaha ya kupata malipo mema kutoka kwa Mola wake.
Mtume wa Mwenyezi Mungu, Sayyidna Muhammad (SAW) alisema:
“Mwenye kufunga ana furaha mbili: Furaha anapofungua na furaha anapokutana na Mola wake – ama kwa ibada au kwa kupata malipo ya saumu yake”.
Miongoni mwa baraka za Idd ni kudhihirisha umoja na mshikamano wa waislamu wa udugu, upendo, msamaha na mahaba baina yetu . Nyoyo zinakutana katika mapenzi ya kumpenda Mwenyezi Mungu na kupendana kwetu kama ulivyo mkusanyiko huu katika Baraza la Idd na kabla ya hapo katika jamaa za sala ya Idd asubuhi yake na pia katika sala za taraweh. Natoa pongezi kwenu nyote kwa kudhihirisha maneno ya Quran, Aya ya 10 Surat Al Hujurat “Kwa hakika waislamu wote ni ndugu”.(MBONA ULITOWA AMRI WAPINGWE MABOMU MSIKITI WA MBUYUNI BASI KAMA SOTE NI DUNGU..?)
Wakati huo huo, nawapongeza wananchi wote kwa jumla, wakiwemo wasiokuwa waislamu kwa kushirikiana pamoja na kuupa mwezi wa Ramadhan heshima yake. Huu ni ustaarabu wa kujivunia. Pia, nawashukuru wakulima, wavuvi na wafanyabiashara kwa kuhakikisha upatikanaji wa vyakula, nguo na mahitaji mengine, wakati wa mwezi wa Ramadhan.
Masheikh wetu wanastahiki pongezi na shukurani za pekee kwa kuendesha darsa za dini katika sehemu mbali mbali. Mwenyezi Mungu awalipe aliyowaahidi – Amin.
Ndugu Wananchi,
Wakati tunasherehekea Idd el Fitr na Inshaallah baada ya miezi mitatu tutasherehekea Idd el Hajj, inafaa tuwe na hadhari juu ya mambo yasiyo mazuri katika jamii. Wakati huu wa Idd, wazazi tunapaswa kuwa makini zaidi na waangalifu ili tuwaepushe watoto wetu wasipate madhara yo yote yakiwemo ya ajali na mengineyo. Tuwe waangalifu zaidi ili tuwawezeshe washerehekee Idd kwa furaha.
Kabla ya kumaliza, ingawa leo tunafurahikia Idd, lakini pia tuna wajibu wa kuwakumbuka wale walioathirika na maafa ya kuzama kwa meli ya MV Skagit, tarehe 18 Julai. Leo tuna mayatima, vizuka, wazazi waliopoteza watoto, wagonjwa na waathiriwa mbali mbali. Tuwasaidie ipasavyo na tumuombe Mola wetu awape ndugu zetu hawa na sisi subira na imani zaidi. Mwenyezi Mungu awalaze peponi wote waliopoteza maisha katika msiba huo. Serikali imeshachukua hatua mbali mbali kuhusu maafa haya. Katika kupunguza tatizo la usafiri wa baharini nimekwishaipa maagizo Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kuhakikisha kwamba katika kipindi cha miezi miwili ijayo wanakamilisha taratibu za kuagiza meli yetu wenyewe mpya, kubwa, kwa ajili ya abiria na mizigo. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu katika kipindi cha miezi kumi na tano (15) ijayo tunatarajia meli hiyo kufika nchini ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,000 na mizigo tani 200 itafika hapa Zanzibar – Inshalla. Nina furaha kupata taarifa kutoka Ofisi yangu inayohusika na Fedha, Uchumi na Maendeleo kuwa fedha kwa ajili ya meli hiyo zitapatikana wakati wowote kuanzia sasa. Pamoja na uamuzi huu, tutalifanyia mabadiliko makubwa Shirika la Meli la Zanzibar, ili lijiendeshe kwa kufanya biashara kwa faida.(SIO MELI TU NA COAST GUARD PIA MAANA HATA HIO IKIZAMA KAMA HAKUNA COAST GUARD NDIO YALE YALE HATUOMBI HIVYO ILA FIKIRI MV SKAGIT INAZAMA COAST GUARD WANASEMA HAWANA MAFUTA KATIKA BOTI ZAO UPO SHEIN)
Ndugu Wananchi,
Leo si siku ya kutoa hotuba ndefu kwa kuwa kila mmoja wetu anataka kwenda kwenye shughuli za sherehe za Idd. Basi, tunaposherehekea tuwajali wenzetu ambao hawana uwezo wa kufanya sherehe kutokana na umasikini, afya na maradhi. Tujitahidi kuwapa msaada watu wa aina hii, pamoja na kuwatembelea wagonjwa na kuwapelekea zawadi. Pia, tuwafurahishe watoto wetu ili wawe na sikukuu nzuri na tuwalinde na maovu. Waendeshaji wa vyombo vya barabarani wachukue hadhari kubwa zaidi katika kipindi hiki cha sherehe na maafisa wa polisi wafanye kazi ya ziada ili kuhakikisha kuwa usalama barabarani na mitaani unakuwepo. Tusherehekee Idd yetu kwa amani na utulivu. Kadhalika, tuwaombee taufiki na Hijja ya kukubaliwa wenzetu walioazimia kwenda Hijja mwaka huu na Mwenyezi Mungu akiwajaalia kufika huko waiombee salama, amani, baraka na kheri nchi yetu na wananchi wote kwa jumla.
Mwenyezi Mungu atuzidishie baraka na mapenzi miongoni mwetu. Atuongoze katika njia iliyonyooka na atuepushe na kila shari. Atupe uwezo wa kuendeleza umoja, uvumilivu na mshikamano nchini mwetu.
Kwa niaba yenu nimetuma salamu za Idd kwa viongozi na waislamu katika nchi mbali mbali za kiislamu. Vile vile mimi na familia yangu nakupeni mkono wa furaha ya Idd wananchi nyote.(WAMBIYE MAWAZIRI WAKO WALIOIBA WEE MPAKA WAKAJISAHAU SASA WAWASAIDIE HAO MASIKINI)
IDD MUBARAK WA KULLU AAM WAANTUM BIKHEIR.

No comments:

Post a Comment