Sunday, August 26, 2012

MNAFIKI WAKWANZA AKUBALI KUHISABIWA-SENSA- KAMA KANISA LINGESEMA USIKUBALI KUHISABIWA USINGELIKUBALI KUHISABIWA ILA MSIKITI UMESEMA UNAUTHARAU SIO MAALIM..?


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad leo amekuwa miongoni mwa viongozi  walioanza kuhesabiwa katika zoezi linaloendelea la sensa ya watu na makaazi.
Makarani wa sensa wakiongozwa na msimamizi wa makarani bibi Asha Iddi Aslan walifika nyumbani kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mbweni mnamo majira ya saa nne asubuhi kwa ajili ya kuwasilisha dodoso la sense.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif  Sharif  Hamad amesema zoezi hilo limeenda vizuri, na kuwataka makarani wa sensa kuendelea kuwa waadilifu na wavumilivu katika kufanikisha kazi hiyo.
Amesema inawezekana kuwa baadhi ya watu hawakupata elimu ya kutosha kuhusu sensa, lakini kwa wale walioelimishwa na kuendelea na msimamo wao wa kukataa kuhesabiwa huenda wakawa na malengo yao binafsi.
“Wanaokataa kuhesabiwa inawezekana wana malengo yao ambayo hawajataka kuyaweka wazi”, alisema Maalim Seif.
Amesema msimamo wa Serikali pamoja na Chama chake cha CUF ni kutaka watu wote wahesabiwe katika zoezi hili linaloendelea, ili kuisaidia serikali kupanga mipango yake ya maendeleo.
Amefahamisha kuwa zoezi la sensa ni jambo la kawaida katika nchi mbali mbali duniani zikiwemo nchi za kiislam, na kutoa wito kwa wananchi kutokubali kuyumbishwa na badala yake waitikie wito wa Serikali wa kukubali kuhesabiwa kwa maslahi yao na taifa kwa jumla.
NYINYI LAZIMA MUKUBALI KUHISABIWA ILI KUHIFADHI TONGE ZENU TUNAWAJUWA NI WANAFI WAKUBWA.

No comments:

Post a Comment