Wednesday, August 8, 2012

TANGANYIKA IKO TAYARI KWENDA KUWAULISHA VIJANA WA KIZANZIBARI NCHINI MALAWI KAMA WALIVYO WAULISHA UGANDA


Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi“Mambo yamewiva. Jee Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SUK-GNU MUKO TAYARI KWENDA KUWAULISHA TENA VIJA WA KIZANZIBARI KAMA MULIVYO WAULISHA KATIKA VITA VYA UGANDA..?wazazi wa vijana wa kizanzibari munamsimamo gani juu ya jungu hili linalopikwa na watanganyika kwenda kuwaulisha watoto wenu.mkae mkijuwa hakuna hata mtoto moja wa waziri wala mbunge wala maraisi hawa watatu atakae pelekwa malawi kuliwa. 
Tuesday, 07 August 2012 20:40
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI, Dodoma
KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imesema Tanganyika (Tanzania) imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.Akizungumza mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Lowassa alisema kamati yake imeridhishwa na maandalizi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanganyika (Tanzania) (JWT) (JWZ).
“Tumepewa maelezo na jeshi letu na tumeridhika kuwa ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na limejipanga vizuri sana kwa uhakika, kiakili na kivifaa,” alisema Lowassa.
Kabla ya Lowassa kuzungumza na waandishi wa habari, alifanya kikao cha faragha kilichohusisha pia wajumbe wa kamati hiyo na makamanda wa (JWT) (JWZ) walipofika bungeni kutoa taarifa kwa kamati hiyo.
Hata hivyo, katika tamko hilo Lowassa alisema Tanganyika (Tanzania) inatarajia mgogoro huo utamalizika kwa njia za kidiplomasia kwa sababu Watanganyika na Wamalawi ni ndugu wa muda mrefu.
“Ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na kama ilivyo ahadi yao (JWT) (JWZ), wako tayari kulinda mipaka ya nchi yetu hadi tone la mwisho. Tunasali sana tusifike hapo,” alisema Lowassa na kuongeza: “Tunategemea hatutafika huko, lakini kwa heshima ya nchi yetu kama ikibidi kufika huko (vitani) tutafika kulinda mipaka yetu”.
Mwenyekiti huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu, alisema kama Tanganyika (Tanzania) itafikishwa mahali itabidi damu ya Watanganyika imwagike, nchi iko tayari kulinda mipaka yake kwa nguvu.Alisema kama itabidi kuingia vitani, itatumia umoja na mshikamano wa Watanganyika na wazanzibari wa mwaka 1978 wakati wa Vita na Uganda kulinda mipaka ili kulinda heshima ya nchi ya Tanganyika.
Alisema mwaka 1978 wakati Rais wa Uganda, Idd Amin na majeshi yake walipochukua sehemu ya Tanganyika na kujitangazia ni mali yake, ilichukua hatua kumfukuza Amin.
“Alijitangazia sehemu ile ni mali ya Uganda hutegemei nchi ikae kimya, hutegemei Watanganyika wanyamaze wakati nchi yao imetekwa, tulichukua hatua tukamfukuza hadi nchini kwake.”
Lowassa alisema Kamati ya Bunge inajua madhara ya kiuchumi yaliyotokana na Vita ya Idd Amin na kwamba vita yoyote ikipiganwa lazima kunakuwa na madhara ya kiuchumi.
Hata hivyo, alisema anaamini mgogoro huo hautafika huko na kusisitiza kuwa, lakini ikibidi (JWT) (JWZ) ni moja kati ya majeshi bora duniani na ni jeshi lililojiandaa vizuri kwa lolote.
“Wako tayari sisi ni moja kati ya jeshi lililojiandaa vizuri na jeshi bora duniani na la kujivunia. Tuko imara kiakili na kivifaa tena vya kisasa,” alisema Lowassa.
Alisema kamati yake inaunga mkono msimamo ulitolewa bungeni juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuhusu mgogoro huo na kwamba ndiyo kauli rasmi ya Serikali.
Juzi, Waziri Membe alizionya kampuni za kigeni za Malawi zilizoingia katika ardhi ya Tanganyika eneo la Ziwa Nyasa kutafiti mafuta na gesi kusitisha mara moja.
Akiwasilisha makadirio ya wizara yake, Membe alisema upo ushahidi kuwa ndege tano za utafiti za Malawi ziliruka anga la Tanganyika na kutua katika Ziwa Nyasa upande wa Tanganyika.Membe alisema pamoja (JWT) (JWZ) kutoruhusu ndege hizo za Malawi kuingia na kutua eneo hilo la Ziwa Nyasa, bado ziliingia na kutua kinyume kabisa cha sheria za kimataifa.
“Wenzetu wa Malawi wanadai Ziwa Nyasa lote lipo Malawi na msingi wa madai yao ni mkataba wa Heligoland wa mwaka 1890 na sisi tunasema mpaka uko katikati ya Ziwa.”
Membe alisema hata mgogoro wa mpaka kati ya Cameroon na Nigeria ulitatuliwa na Mahakama Kuu ya Dunia kuwa mpaka baina ya nchi hizo mbili upite katikati ya Ziwa Chad.
Juzi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Patrick Kabambe alikaririwa na Redio Sauti ya Ujerumani akisema wataendelea na utafutaji mafuta licha ya onyo hilo la Tanganyika.
Waziri huyo alisema ziwa hilo linaitwa Malawi na siyo Ziwa Nyasa na kwamba utafutaji wa mafuta na gesi utaendelea na hakuna wa kuwasimamisha. Alihoji, iweje Tanganyika ishtuke sasa..???
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI
HAYA KISHEIN UTAKUJA KUOMBWA SASA HIVI VIJANA WA KIZANZIBARI UKAWAULISHE MALAWI.KAMA WALIVYO FANYA KATIKA VITA VYA UGANDA NA VITA HIVI NDIO HIVYO VINAPIKWA. MAANA TOKA UAMSHO IVUME WAZAZI WA VIJANA WINGI WAMELALAMIKA KUWA VIJANA HAWANA KAZI.  HATA JESHI WANAKATALIWA SASA TANGANYIKA IMEKA IKAFIKIRI IMEONA OK WANATAKA KAZI SIO TUTAWAPA.  WANAKWENDA KUICHOKONOWA MALAWI ILI VITA VIANZE KISHA MACHONGO HAWA WAONGA KAMA NINI KUFAA NINI KITAKACHOTOKEA NIKUWA ZANZIBAR PIA NI TANZANIA KWA HIYO TUPENI VIJANA. WATAKUJA KUBEBWA WATU MAJUMBANI ILI WAKAISADIYE TANGANYIKA KUPIGANA NA MALAWI WATAWEKWA FRONT LINE ILI WAULIWE WAO KWANZA MCHEZO HUWO UNACHEZWA DODOMA.  WAZANZIBARI VUNJENI MUUNGANO HARAKA HARAKA TENA HARAKA AU SOTE TUTAKWENDA ULISHWA MALAWI WANAUME KISHA WANAWAKE WETU WAJE WATESEKA NA WATOTO AMKENI WAZANZIBARI AMKENI.KAMA NI VITA BASI BORA TUPIGANE NA WAO WATANGANYIKA,WAKOLONI WEUSI,MAKABURU WEUSI WASIYOTAKA KUTUPA UHURU WA NCHI YETU YA ZANZIBAR KULIKO KUPIGANA NA WAMALAWI KWA FAIDA YA TANGANYIKA SISI ZANZIBAR ZIWA NYASA HALITUHUSU KABISA TUNA BAHARI SIO MCHEZO NAYO PIA TANGNYIKA ANATAKA KUICHUKUWA WAZANZIBARI  HII NI NJAMAA YA KUTAKA KWENDA KUWAULISHA VIJANA WA KIZANZIBARI NA KAMA HAMUAMINI NGOJENI MUONE VITA VIANZE TU WATAKUJA KUCHUKULIWA VIJANA NYUMBA HADI NYUMBA KUANZIA UNGUJA MPAKA PEMBA WALAZIMWISHWE KWENDA KUPINGANA VITA HIVYO NA WAMALAWI.

No comments:

Post a Comment