Wednesday, August 1, 2012

UAMSHO YA TANZANIA BARA YAWATIA MIKWAJU MACHANGU NDOWAA KATIKA JIJI LA DAR-ES-SALAAM-KWA KUTO UHISHIMU MWENZI MTUKUFU WA RAMADHANI



Stori:
Machangu wamekiona cha mtemakuni! Wakati Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ukiwa katika kiendele, akina dada wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili maarufu kama Machangudoa au Chipsi Funga au Wauza Sukari Tamu,kula uwondoke,wamekulaviboko laivu baada ya kutuhumiwa kuwatega Waislamu.
Tukio hilo liliajiri katikati ya wiki hii ambapo vijana wa Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho cha Tanzania Bara walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia bakora za nguvu machangu duwa hao ambao kwa sasa wametapakaa kila kona jijini.
WATUMIA BAJAJ
waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba baana ya serekali kushindwa kabiasa kuondosha uchafuu katika mji na haswa ukiangalia kuwa raisi wa nchi hii ya tanganyika kuwa ni muslim na hajali wala hata kufikiri yakuwa huu ni mwenzi mtukufu na kuana rai wangu wanafanya machafu habu niwakataze kimya ikulu.
BARABARA YA SHEKILANGOVijana hao waliolenga kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo walianzia kwenye Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viungo vya Sinza, Dar ambapo kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi kwenye mataa ya Shekilango waliwakuta machangu na kuwatandika viboko kabla ya kutua mitaa ya Mwenge
KINONDONIBaada ya kufagiafagia Sinza kwa kuwaadabisha wanawake hao ndipo zoezi likahamia mitaa ya Kinondoni ambapo nao walipokea bakora na mikwaju ya nguvu.
KISA KUHARIBIWA SWAUMU
Kwa mujibu wa vijana hao, walifikia hatua ya kufanya zoezi hilo baada ya muumini mmoja wa kiume kukatiza maeneo ya Corner Bar, Afrika Sana na kuvutwa kisha kuchezewa nyeti na makahaba na kusabisha kuharibika kwa swaumu yake.
Ilieleza kuwa baada ya kukutwa na kimbembe hicho, ilibidi muumini huyo kukatiza safari yake ya kwenda kuswali msikikini mishale ya saa 2:00 usiku.
Ilisemekana kuwa aliporudi nyumbani alitawadha na kufunga safari nyingine ya msikitini na alipofika kwenye msikitini ndipo akawasimulia waumini wenzake ambao nao walikasirishwa na kitendo hicho hivyo wakapanga kuvamia maeneo yote ya biashara hiyo ili kuwashikisha adabu na kuondowa uchafu huu.
Waandishi wetu, wakiwa kwenye mishemishe zao za kutafuta habari mishale ya saa 5 usiku waliwashuhudia waumini hao wapatao saba wakishuka kwenye Bajaj nyeusi maeneo ya Sinza wakiwa na bakora mikononi kisha kuwavaa machangu hao na kuwatandika.
Wakati wakitekeleza zoezi hilo, jamaa hao walisikika wakiwaambia: “Sisi tupo kwenye swaumu nyiye mnatutega, ala!”bakora na mikwaju ikiendelea na machangu wengine kuanza kutoka nduki
HAWAHESHIMU MWEZI MTUKUFU?
Waumini hao waliongeza kusema kuwa makahaba hao wamekuwa hawana heshimu na mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan ndiyo maana wanaendeleza biashara yao hiyo ya aibu na uchafu
.

No comments:

Post a Comment