Wednesday, August 1, 2012

VIDEO-BAADA YA MABOMU SASA SHEINI AFTARISHA NA KUKITUMA KIBARAKA CHAKE KUHIMIZA SENSA


Na FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSIWAZIRI ASIYE KUWA NA WIZARA MAALUM wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Shein jana aliungana na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika futari maalum aliyowatayarishia wananchi hao.
Hafla hiyo ilifanyika huko katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Chake na kuhudhuriwa na wananchi mbali mbali wa Mkoa huo pamoja na viongozi wa dini, Serikali na vyama vya siasa.
Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Juma Kasim Tindwa, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Mwinyihaji Makame, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih na viongozi wengine.
Akitoa neno la shukurani kwa wananchi waliohudhuria futari hiyo kwa niaba ya Rais Dk. Shein, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Juma Kasim Tindwa alieleza kuwa Dk. Shein amefarajika kwa ushiriki wa wananchi hao katika futari hiyo maalum aliyowaandalia na anawatakia kila la kheri wananchi hao.
Mhe. Tindwa aliwaeleza wananchi hao kuwa Dk. Shein hana cha kuwalipa kwa mahudhurio yao hayo ila MwenyeziMungu ndio atakaowalipa na kusisitiza kuwa upendo katika nchi ndio uliochangia kuwepo mkusanyiko huo sanjari na amani na utulivu iliyopo.
HII NDIO RAMADHANI ALIO WAPA SHEIN WAZANZIBARI ACHENI UNAFIKI WENU WAKUPAKA MAFUTA MAZURI NA KUMWAGIA ASUMINI NA VILUWA.
Nae Sheikh Mohammed Suleiman, akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba walieleza shukurani zao kwa waziri huyo isiyekuwa na wizara maalum na kusisitiza kuwa hatua yake hiyo inaonesha upendo mkubwa kwa wananchi wake.
Alisema kuwa.Shein ana kila sababu ya kusifiwa na kupongezwa katika juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar pamoja na kuimarisha amani, utulivu na upendo miongoni mwa wananchi.
Katika maelezo yake Sheikh Mohammed Suleiman na UNAFIKI WAKE NA KUJIPENDEKEZA KWA SHEIN aliitaka jamii ya Kizanzibari kutokuja mlaumu Shein kuwa hajawaletea maendeleo kama watakataa zoezi la kuhesabiwa yaani Sensa.
Sheikh Suleiman Aliendele kusa na UNAFIKI WAKE,kuwa maendeleo yoyote hayawezi kupatikana iwapo hapatakuwa na Sensa na kusisitiza kuwa mtu asije ilaumu serikali ama kiongozi wa nchi kuwa hajaletewa maendeleo kama atakata yeye mwenyewe kuhesabiwa.
Alieleza kuwa jambo hilo katika Uislamu sio geni kwani Mtume Mohammad (S.A.W) alikwisha waeleza Waislamu kuwa hataingizwa mtu peponi ama motoni bila ya kuwepo Sensa akiwa na maana ya kuhesabiwa.astahafiru allah  sheikh tubu kwa mola wako.
Pamoja na hayo, alieleza kuwa zoezi hilo la Sensa litaweza kusaidia kujua idadi ya mayatima, walemavu wa aina zote na watu wengineo ambao pia nao ni muhimu katika jamii na wamekuwa wakihitajia mahitaji muhimu lakini baadhi yao wamekuwa hawayapati kutokana na kutojulikana idadi yao.hawakujuwa idadi ya watu waliozama katika meli ya MV.SPEICA na MV SKAGIT watajuwa ya watu waliokuwa majumbani wacheni unafiki semani kweli mnataka yanu yawe mupate pesa mulizo ahidiwa mnajuwa wazi kama hamukufanya hiyo sensa hamuzipati hizo pesa.
Katika futari hiyo, Mama Mwanamwema Shein nae alishiriki akiungana na akina mama wenzake kutoka sehemu mbali mbali katika Mkoa huo pamoja na viongozi wa dini, serikali na vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla.
Leo Shein anatarajiwa kufutari pamoja na wananchi wa Mkanyageni Chokocho huko Chokocho.
Wakati huo huo salamu za rambirambi kufuati kuzama kwa meli ya MV Skagit hivi karibuni zinaendelea kutolewa kwa waziri huyu asayekuwa na wizara maalum wa Zanzibar na pamoja na wananchi wa Zanzibar ambapo Jumuiya ya African Public Administration anda Management (AAPAM) imetoa mkono wa pole kutokana na ajali hiyo.
Nayo Jumuiya ya Wawekezaji katika sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI) imetoa mkono wa pole kwa waziri huyo asiyekuwa na wizara maalum,familia na wananchi wote wa Zanzibar kufuatia ajali hiyo vichekesho walio fiwa hawapewi pole anapewa waziri asiyekuwa na wizara maalum sheini pole.

No comments:

Post a Comment