Monday, August 6, 2012

WAZANZIBARI MULIOKOWEKO NJE,MUNASAIDIA VIPI KATIKA KUIKOMBOWA NCHI YETU YA ZANZIBAR..?



HAWA NDIO MRIMA FAMILI AU UKIPENDA UNAWEZA KUWAITA MAKABURU WEUSI
Ukombozi wa Zanzibar ni mfululizo wa mapambano yanayoendelea kwa muda mrefu sana, huku baadhi ya watu wakijitoa muhanga kwa kila hali na mali,kisiasa na pia tumeshuhudia hata wengine wakipoteza maisha yao katika mapambano haya. Lengo lao Wazalendo hawa ni kuipigania Nchi yao kwa kuweka heshima ya Taifa lao. Mwana mzalendo yeyote lazima ajitolee katika hili,na ni vyema akaelewa kwamba ama inawezekana malengo na madhumuni yake kufanikiwa au kupotea mwenyewe kwenye mapambano haya,kwani vita hii sio lele mama,inatakiwa kujitolea muhanga.
Ni vita ambayo mara kwa mara huwa kuna baadhi ya kundi au Taifa fulani linafaidika kwa njia moja au nyengine,hii hupelekea hata umwagaji wa damu na majanga mengineo, lengo ni wahusika kulinda maslahi yao binafsi.Na hichi ndicho kinachoendelea hapa Zanzibar, Serikali ya Tanganyika inajivunia maslahi yake Zanzibar, kwa kuinyima fursa za kila aina kisiasa na kiuchumi lakini pia Wahafidhina wachache ambao na wao  wamevalishwa kilemba cha ukoka pia na wao wanafaidika kwa upande wao,kwa maana hiyo ndio tunashuhudia kuona Zanzibar imeshindwa kupumua kwa muda mrefu,nguvu za ziada zinahitajika ili kuweza kujinasua na dhulma hii.
Tumeshudia akina Nelson Mandela na wengine wengi wakipigania Nchi yao kwa kujitoa muhanga nafsi zao huku Wazalendo wengine wakiweka kambi zao nje ya Nchi kuendeleza mikakati ya mapambano kwa Nchi yao.Pili tumemshudia Rais wetu wa zamani wa Visiwa vya Zanzibar Al-haji Aboud Jumbe Mwinyi akipoteza Urais wake kwa kupigania ukombozi wa Visiwa hivi na wengi wengineo. Naamini kwamba mchango wao wote unaonekana na umechangia pakubwa katika vugu vugu hili la kuleta ukombozi wa kweli katika Taifa letu.
Vile vile tumeshuhudia mengi Zanzibar tokea vuguvugu la kudai ukombozi mpaka kufikia kuundwa kwa mfumo wa vyama vingi,ukweli yametokea mengi ya kuhuzunisha na mimi binafsi sipendi kuyakumbushia kwani yanatia unyonge ingawa kwa upande mwengine yanajenga ari,hamasa na ujemedari wa kujitolea ili kuikomboa Nchi yetu.Alama za nyakati zinatofautiana na pia aina za mapambano pia zinatofautiana vile vile.Hili lazima tulikubali kwamba wale wote wenye mawazo ya kale lazima waelewe kwamba kilichobakia ni historia hivi maendeleo ya tekinolojia ya kisasa na demokrasia ndio yanayotawala dunia kwa sasa,hatuna budi kuelekea huko kama Taifa huru.
Zanzibar katika kipindi hichi cha karibuni kumetokea matukio chungu mbovu ya watu na vikundi mbali mbali lakini mpaka jumuia na asasi za kiraia kwa njia moja ama nyengine kuzungumzia suala la uhuru kamili wa Zanzibar kama Taifa huru. Ni jambo la kushukuru kwamba leo hii walio wengi wamefahamu lengo na madhumuni ya kuipata Zanzibar yetu.Ni dhahiri licha upinzani mkubwa uliopo lakini ukweli umedhiri kwa maana hiyo uongo unaanza kujitenga.Hatuna budi kwa Wazalendo wote kuunganisha nguvu zao zote ili kuona yale madhila ya muda mrefu yanafikia mwisho wake na Zanzibar inajitawala wenyewe kama ilivyokuwa hapo awali.
Suala langu linakuja kuhusiana na Wazalendo walioko nje,jee wanasaidia vipi katika ukombozi wa Zanzibar ? Hii ni kutokana na ukweli kwamba kila mzanzibar Mzalendo ana sehemu ya mchango wake katika hili. Tumekuwa mara nyingi tukitupia lawama baadhi ya viongozi hawafanyi hivi na vile lakini tujiulize sisi binafsi mchango wetu ni upi katika  Taifa letu.Tukumbuke kwamba Wazalendo walio nje wana umuhimu mkubwa sana katika ukombozi, hii ni kutokana na kuwa na kila fursa na nyezo za kuwasaidia Wazalendo wenzao walioko nyumbani.Ni vyema tukaitumia fursa hii kuliko kuwatupia mpira baadhi wa watu wengine ambao jitihada yao na juhudi zao hazina kikomo katika mapambano haya.
Matusi au lawama ambazo tunatoa katika mitandao mbali mbali ya kijamii tuelewe kwamba hazitotusaidia sana bila ya kuelewa kwamba na sisi kama Wazanzibar Wazalendo tuna sehemu yetu katika jamii yetu. Ujumbe kweli unafika lakini ni watu wachache tu ndio ambao wanafaidika nao na hasa wale walioko nje ama kwa kupata habari za kwao ua pengine kwa kujifurahisha tu lakini lile lengo la ukombozi na mapambano linakuwa halipo.Ni vyema tukashikamana kwa pamoja bila kuangalia huyu ni nani na anatoka wapi,kuna kila njia na nyendo kufanikisha mapambano,tukaeni pamoja tuwasaidie wengine kwenye kupigania ukombozi wetu.
Nchi nyingi ambazo zinafanya mapambano kama yetu basi wale wote walio nje ndio wanaokuwa waratibu wazuri wa harakati zile. Tumeshuhudia Wanaukombozi wengi wakiwa na ofisi zao nje kuratibu mapambano ya uhuru wao. Sisi kama Wazanzibar tumejaaliwa kupata bahati nzuri kwani wengi wa Wazanzibar leo hii wanaishi nchi za nje,sehemu ambazo zina fursa za kila aina,jee mchango wetu ni upi katika hili tukumbuke kwamba jazba na matusi kwenye mitandao haitosaidia chochote zaidi ya kujifurahisha tu na kuudhiana wakati mwengine.
Nitowe mfano mdogo tu kama tunavyosikia kwamba ujumbe wa Tanzania uko Marekani kudai kuongezewa kwa eneo la bahari,sote tunaelewa fika kwamba sehemu ile wenye uwezo wa kumiliki au kuomba ni sisi Wazanzibar na kule Marekani wapo Wazanzibar ambao wanalijua hili wamekaa kimya basi hata maandamano tunashindwa kuionesha Dunia kwamba Wazanzibar hawaridhishwi na hili . Hapana budi kuonesha kwa vitendo hisia zetu kwamba hichi ni chetu na tuko huru kukipigania mpaka tone la mwisho la uhai wetu,huu ndio uzalendo tusiwe na fahari kusifu vya wenzetu huku kile chetu kinaangamia na kupotea mikononi mwa walowezi na mafisadi.
Leo hii yanatokea matukio makubwa makubwa Zanzibar tumekaa kimya hivi kweli kilio chetu ni nani atatusikiliza ?Zamani miaka ile 1995 angalau kule United Kingdom vijana walikuwa na harakati za hapa na pale leo hii kimya kila mmoja anashughuli zake hivi huu uzalendo uko wapi ? mwisho tunakuwa wazuri wa kulaumu na kumuoneshea kidole mtu mmoja oh’ Maalim Seif mbona hajafanya hivi au vile,serikali ya GNU haijafanya hivi, uamsho wanapinga muungano lakini hawandamani,sasa tujiulize sisi tumechangia nini zaidi ya maneno chabwaa yenye maudhi tu.
Wazalendo walioko nje lazima na sisi tukubali kwamba ni wahusika katika hili na pia tuna michango mikubwa  katika kufanikisha ukombozi wetu.Tusihadaliwe na usiku wa kiza tukajisaidia njiani ,mchango wetu unahitajika sana. Wazanzibar walioko Visiwani wamefanya mengi na wanaendelea kudai uhuru wao,kinachohitajika ni kushirikiana nao katika mapambano,huu ni wakati pekee kutoa michango yetu kwa jamii na msaada mkubwa unahitajika,kwani hili ni la kwetu sote kama Wazanzibar Wazalendo. Ni imani kwamba wito na ujumbe huu utawafika Wazalendo wenzetu na pia wataufanyia kazi,lazima tuelewe kwamba :
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR MWAZO.
Ipo haja ya kukaa pamoja na kutafakari nini cha kufanya kuwasaidia wenzetu lengo na madhumuni ni ukombozi wa Nchi yetu,tusiwe na mawazo ya kumtukana Imam Farid au mzee Moyo,hawa wanahitaji support kutoka kwetu kwani tayari wameshajitolea na tukumbuke kwamba tulikotoka ni mbali na tunapo kwenda ni karibu.Pia kila mtu ana mchango wake katika kupigania hili,hata barua pepe kuituma kwa pale panapo husika basi ni mchango mkubwa na wenye thamani katika ukombozi,na wewe utahesabika kwamba umechangia katika mapambano haya ya ukombozi

No comments:

Post a Comment