Tuesday, August 28, 2012

Z,BAR NA SENSA-ATI MAENDELEO-YATAKUJA VIPI NA SISI TUNATAWALIWA NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA..?

Nimekuwa nikifuatilia taarifa mbali mbali kuhusiana na suala zima la sensa na pia kusikiliza hoja nyingi za viongozi wetu wa kitaifa kuhusu suala na umuhimu wa kujiandikisha kwa kupata idadi ya watu wanaoishi Nchini kwa lengo la kupata takwimu halisi kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi. Naamini ya kwamba wahusika wanaopigia kelele suala hili kama vili kishein,balozi na maalim seif wana malengo yao maalumu kinyume na kauli mbiu yao ya kutaka kuleta maendeleo.Suala la maendeleo hivi sasa Zanzibar nisawa na kumpigia mbuzi gitaa ukifikiria atacheza,kumbe unajidanganya.Maendeleo huletwa na Nchi ambayo inajitegemea na kujiongoza wenyewe kimamlaka,tofauti na Wazanzibar ambao hii ni nusu karne wanatawaliwa na wakoloni weusi tanganyika.


Napenda kutoa kauli hii kwamba sensa haina umuhimu wowote kwa Wazanzibar hasa kwa kipindi hichi tulichonacho.Kinachofanyika hapa Zanzibar ni serikali yetu ya kufuata mkumbo tu wa wakoloni wetu wa tanganyika kwa vile Tanganyika wanataka wajue idadi ya Raia wake ili waweze kutimiza ile adhima na malengo yao waliokusudia, na sio mengine bali kuwadhalilisha Waislam ambao inaonekana ni tishio kwa Serikali ya Tanganyika hivi sasa.Waislam wa Tanganyika wamechachamaa kudai haki zao za msingi kutokana na kuelewa kwamba Serikali ya Tanganyika inajiendesha kidini zaidi na kuwapa kipau mbele watu wa dini nyenginezo na hasa Wakristo,lengo la sensa hii nikujua idadi yao na kubuni njia za kuwadhibiti Waislamu si vyenginevyo.Hizi ni mbinu chafu zinazotumika kuwadhibiti baadhi ya Raia ambao wanaonekana kama vile ni kero katika medani ya utawala na mrengo wa dunia kwa ujumla.

Ipo haja ya kujiuliza hivi hii sensa faida yake ni ipi kwa Wazanzibar hata viongozi wetu wakawa wanakemea na kuwahamasisha Wananchi lazima wajiandikishe ? Ikiwa ni kwa ajili ya maendeleo sawa, lakini hayo maendeleo hivi sasa Wazanzibar wapi na wapi! kila mtu hoi bin taabani hajui hatma yake kuhusu nchi yake ni ipi ,hivi sasa kwa Wazanzibar sio wakati muwafaka wa kufikiria sensa badala yake ni kuja na mawazo ni mikakati gani itumike ili tupate Nchi yetu,lakini ndio hivyo tena vingozi wetu wanazidi kutuchuuza. Mimi kimawazo yangu ni kwamba sensa kwa Wazanzibar haina maana hasa kwa wakati huu, nilifikiria kwamba Viongozi wetu watasimama kidete kuwaelimisha Wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba ambayo yataamua kuhusu hatima ya Nchi yetu lakini viongozi kimya matokeo yake wamelivalia njuga suala la sensa kama vile tukiishahisabiwa ndio matatizo ya Wazanzibar yatakuwa yameisha.

Hoja zinazotelewa kwamba sensa ni kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi hazina mashiko yeyote, hivi tujiulize hapa tulipofikia sisi Wazanzibar ni nani utamdanganya kwa kumwambia kwamba ukiisabiwa ndio utapata maendeleo.Ikiwa serikali inashindwa hata kujiamulia mambo yake binafsi kama Serikali lazima wapangiwe kutoka Tanganyika hayo maendeleo yanaozungumziwa na sensa yako wapi,hii ni danganya toto lakini sensa haina ukweli wowote wala maendeleo ya aina yeyote kwa Wazanzibar.Viongozi  wasijitutumue tu kwenye sensa bali watafute mbinu za kuwatatulia Wazanzibar kero na matatizo yao na moja wapo ikiwa ni suala la Wazanzibar kupata Nchi yao na kujiamulia mambo yao wenyewena kulivua hili jinamizi la Muungano na ukoloni wa kitanganyika kuwambiya bye bye.

Ikiwa ni kuhusu kuyakata majimbo na kuyapunguza kutokana na idadi ya watu, hii si sababu ya msingi kwani C.C.M chochote wao watakachoamua hakuna wa kuwazuia. Ikiwa leo baadhi ya Viongozi wanamkemea na kumkejeli muasisi na Mwanaukombozi kama Mzee wetu Moyo watashindwaje kukata majimbo ya Wapinzani . Sensa haitowafanya C.C.M kushindwa kuyagawa majimbo kwa faida yao kwani wao ndio wanao endesha Serikali ikiwa wameshaamua kufanya hivyo,basi sensa ikifanyika isifanyike hilo kwao sio kikwazo, ,kigezo wala hoja ya msingi.Cha msingi ni Serikali kuwasikiliza kwa makini ni kitu gani Wazanzibar wanahitaji hivi sasa.Na hili naamini liko wazi halihitaji mzungu kutoka nje,kwamba kilio cha Wazanzibar ni NCHI YAO KWANZA, upuuzi wa sensa baadae.

Nahisi ipo haja kwa Serikali yetu kuelewa kwamba sisi Wazanzibar sensa haina faida kwetu,sisi tunachohitaji ni nchi yetu sio sensa na hili ukilizungumzia wengine wananuna.Wananchi wa Zanzibar wameshachoka kuburuzwa kila siku.leo hii wamejitokeza baadhi ya watu wanaitetea Zanzibar ili ijikwamue,Wazalendo hawa leo ndio wanaonekana eti ni wasaliti hawana ”support” yeyote isipokuwa matusi na kebehi lakini unakuja upuuzi huu wa sensa Viongozi wote na vyombo vya habari na magazeti imekuwa ”issue”,mbona hamsemi kwamba Wazanzibar wanataka Nchi yao wameshachoshwa kutawaliwa NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MBONA HAMUSEMI..? ,mbona kimya !.Tuwe wa kweli kuzungumzia matatizo yanayo wakabili Wazanzibar na tuyape kipau mbele lakini hivi sasa Wazanzibar kuzungumzia sensa ni kizungu mkuti,haingii akilini.

Kama kweli nyinyi lengo lenu ni kujua idadi ya watu au sio ? Nyinyi kama Serikali munashindwa nini kuwapa Raia wenu vitambulisho vya Uraia, kama vile pasipoti,vyetu vya kuzaliwa na ID nyenginezo,hii ni njia nyepesi na wala haina harama kwa Serikali kujua idadi ya Raia zake,hili dogo linawashinda sasa hayo maendeleo munayo yazungumzia yatakuwaje na tuwaelewe vipi. Ndio maana nikaja na hoja kwamba Wazanzibar hawahitaji sensa,ikiwa mtu ni raia wa kizanzibar Baba na Mama ananyimwa haki ya kujiandikisha na kuitumia haki yake hiyo ya kupiga kura na kumchagua anaetaka ndani ya nchi yake,yeye kama yeye sensa ina faida gani kwake kama si kumdhalilisha na kumfanya mjinga na mtu asie na thamani yeyote kwenye taifa lake kama raia.

Nchi ambazo zinafanya sensa ni zile nchi zinazowajali Raia zake na kuwathamini lakini leo hii Mzanzibari ni bora mnyama Nchi za nje(mbwa) anathamani na anathaminiwa kuliko yeye kwenye Nchi yake, sasa sensa inafaida gani kwake ? Nikupotezeana muda na kuwafurahisha wengine wenye malengo yao.KINA KISHEIN,SEIF SHARRIF NA BALOZI ili wazidi kuiba vizuri na kujitajirisha. Natoa mwito kwa Viongozi wetu kushughulikia Utaifa wetu na kupata Nchi yetu kwanza kutoka katika makucha ya Tanganyika halafu hili suala la sensa litakuja baada ya Wazanzibar kupata nchi yao, lakini leo hii kufanya sensa ni sawa na kutia maji pakachani ukidhani ni mtungi kumbe yote yako chini,tukiambiwa na sisi tujiambie tusikurupuke tu watu wakatutoa kwenye malengo yetu ya kudai NCHI YETU.

No comments:

Post a Comment