Saturday, October 27, 2012

SHEIN-WENYE DEVU ZINYOLEWA KWA NGUVU WANAWAKE WENYE NIKAB WAVULIWE NA KUPIGISHWA VICHURA


Haya, tumeshuhudia kunyolewa ndevu kwa Mamiri wetu wakombozi wa zanzibar na wazanzibari akina Ustadh Farid na wenzake wa UAMSHO.
Kinachoendelea sasa ni kuwa vikosi vya washenzi wa shein na vile ulinzi na Usalama vya Bara,vinapita mitaani na kufanya yafuatayo:
1. Kuwanyoa ndevu wanaume wanaowakuta njiani (wameyafanya haya juzi, na jana maeneo mjini, ikiwemo pale Vuga maeneno kwa ‘ally mpemba’.
2. Kuwavua nikab wanawake, kuwagaragiza chini, na kuwaendesha kichura wanawake. Haya yanafanyika mbele za kadamnasi.
3. Kufunga baadhi ya misikiti isilaliwe, na jana walimwaga maji ya kuwasha msikiti mmoja Bububu, na kuuchafua vibaya sana.
* Ukiachalia zile taarifa za kuuliwa kijana mmoja maeneo ya Magomeni, na mwengine kupigwa mahtuti baadhi ya vijana kule Daraja bovu, kuna hali ya kutisha zaidi na zaidi ya kuwapora watu mali zao, kuwanajisi watoto, na kufanya ujahil kama huo.
* Mambo kama haya, kuvua nikab, au kuwanyoa ndevu wanaume – ilikuwa sana anafanya mambo haya ni ben Ali wa Tunisia alipokuwa madarakani kama alivyo sasa kishein.
Yeye Ben Ali alikuwa pia haruhusu vijana kuwa masheikh au kusali, alikuwa anaamini kusali/kutoa mawaidha — ni kazi ya wazee tu.
What next? Nadhani SMZ itapiga marufuku hata kusali, na kufanya ibada yeyote ile, na itakuwa marufuku kusali msikitini (Ben Ali pia aliwahi kutoa fatwa kama hizo). Usiseme haiwezekani, everything is possible chini ya utawala wa waislamu wenzetu (Kikwete, Kishein, Mwinyi, na wenzake wooote).
Naomba tukumbuke kuwa wiki mbili zilizopita, RPC wa Mwanza, Barlow — aliuliwa kikatili sana, na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi – lakini mpaka sasa, hakuna msako wala kupigwa watu wa mitaa ya Mwanza ikiwemo eneo alipouwawa kamanad huyo wa Mkoa — eneo la Kitangiri.
* Huo ni mfano tu. Sasa kinachofanyika Zanzibar dhahir bila kujificha ni visasi [revenge] vya zama na zama vilivyobaki katika nyoyo za watu wa Wazanzibar dhidi ya wenzao.
* Kwa muhtasari — kila kiongozi wa Zanzibar lazima afanye ujahil wa kupindukia ndio aonekane kuwa kiongozi aliyekamilika bila hivyo anakuwa hajakamilika kama ni rais ‘halali’. Lazima kila Rais akamilishe na kumegua sehemu ya Zanzibar na kuisalimisha kwa Tanganyika.

No comments:

Post a Comment