Saturday, October 27, 2012

KISHEIN CHATUMIKIA KANISA KWA NGUVU ZOTE KUWADHALILISHA MASHEIKH NA WAISLAMU NCHINI ZANZIBAR


WASHENZI WA SHEIN WANAENDELEA KUWASHIKILI WAKOMBOZI WA ZANZIBAR DIKTETA SHEIN ASEMA ATAWASHUGHULIKIA WALE WOTE WANAOJARIBU KUITOWA ZANZIBAR KATIKA MAKUCHA YA TANGANYIKA

Hii ndio hali inayoikabili Zanzibar kwa sasa — mpaka jana nipo msikitini kwa sala ya Ijumaa walikuwa jamaa hawa wa vikosi vya SMZ wanaimba na kuisulubu UAMSHO na viongozi wake huku wakiwataja kwa majina na kusema kuwa ‘tumewanyoa ndevu’ n.k pamoja na kugha jengine za kejeli na matusi, na idhalali.

Zanzibar tumefika hapa, angali kwa makini:
1. Tunapachua bendera za UAMSHO [zilizoandikwa lailah ila-llah] chini ya mtutu wa bunduki, badala yake zinapachikwa bendera za CCM.HONGERA SHEIN

2. Wamenyolewa ndevu masheikh wetu, viongozi wetu mamiri wetu wakombozi wetu viongozi wa dini (alama muhumi katika uislamu na sunna kubwa kuweka ndevu); lakini tumeridhia sana na kuwaacha vijana na kufuga nywele ‘rasta’. Tumefika hapa.HONGERA SHEIN

3. Tumezuia kusali hadharani [uwanjani kama zilivyo sunna] na baadhi ya misikiti kuzuiliwa kusali,HONGERA SHEIN na tumeruhusu msikiti kama ule pale Mwembeshauri, masjid mushawar wa serikali – kusali, na kutumika kama platform ya kuwatukana na kuwakashif na kuwahukumu viongozi wa UAMSHO ndani ya msikiti, mbele ya viongozi wote wa SMZ, na wa dini – akiwa Fadhil Soraga amesimama juu ya mimbar ya msikiti akitukana na kutoa hukumu dhidi ya akina Farid na wenzake.

4. Jamani eee ….. kesi hii iko mahakamani bado, lakini leo tunaona wazi wazi – Shein (MTUMWA WA WATANGANYIKA,anae jifanya anajua utawala wa sheria) anatoa hukumu dhidi ya viongozi wa UAMSHO, kwakutumia platform ya baraza la Eid, tunashuhudia Mohammed Aboud anatoa statement za kuwahujumu watuhumiwa, tunamuona Soraga anatoa hukumu dhidi ya watuhumiwa, tunamuona na kumsikia Mussa Ali Mussa, kamishna wa polisi firauni anatoa hukumu dhidi ya suspects kabla ya hata mahakama kutoa hukumu. CCM Kisiwandui kama kawaida, pia wanatoa hukumu dhidi ya akina Farid na wenzake kabla ya mahakama kuamua. Kisheria tunasema hakuna aliye juu ya sheria…..na huwezi kuamuliwa wewe ni muhalifu au laa, before the court. Hapa ibara ya habari hii ni kubwa. Lakini viongozi wetu, kama ninavyosema siku zote, kuwa wanaishi katika impunity – hawajali kufanya makosa, na wanajisifu kwa fakhari kubwa.

Kweli akina Farid na wenzake wa UAMSHO ni ‘watu wabaya sana..?’, SMZ viongozi wake, na DPP office, na Mahakama – wazuri kiasi gani ikiwa wameuwa mtoto bububu miaka 14.

Angalia — DPP Office chini ya Ibrahim Mzee (huyu mzalendo mnayemchekea sana humu ukumbini eti anaitetea Zanzibar kupitia makongamano ya BLW, na ule uchepe unaofanywa na akina Hamza, Asha Bakari na wenzake) – leo kesi kama hii inayowakabili akina Farid and others iko wazi kabisa kuwa BAILABLE/yaani inadhaminika; leo DPP inaingiliwa na mifumo ya siasa chafu za Zanzibar na kuwanyima dhamana watuhumiwa hawa.

* DPP office inakubali kupinda ethics na taratibu zake za kazi pengine kwa kuwaridhia ‘mabwana’ wakubwa. Yuko wapi Abubakar Khamis Bakari mnafiki, Waziri wa Sheria under GNU. Kweli haki hii..?

Lakini yote ya nini haya: chanzo ya switilfahamu hii ni kuelekea kupata katiba mpya. Awali, nilisema kuwa Katiba MPYA ndio chanzo cha fitna, na ndio source ya kuimaliza Zanzibar. Sasa, tusubiri SERIKALI MOJA NDIO LILILOBAKIA NA SHEIN NDIO ALIYECHANGULIWA KUTUMALIZA.

Kumbuka kuwa Mjini Magharibi ndio wataofuata kutoa maoni, na mmemuona na kumsikia jaji Warioba alivyokuja hapa kutisha watu – na wajumbe wa BLW. Na bado………..mtaona kibano.

* Nyie pigeni kofi kwa GNU, Katiba Mpya, na mambo kama hayo. Hivi sasa, SMZ inachagua vijana ‘makini’ na kwa siri kubwa “wao kwa wao” kuingia katika tume ya kubadilisha katiba mpya — kwenda kufanya kazi maalum huko. Yatafuteni mtayapata.

* Hawa wanaingizwa kwenda ‘kuchakachua’ na kuandika vile wanavyotaka wao, sio walivyosema wananchi au wanavyotaka wananchi wa Zanzibar. never be……Tume ya Warioba wakaridhia watachosema au watachotaka Wazanzibari. Hii ninasema wazi na kujiamini kuwa NEVER BE! Hii wiki hii tu, kuna vijana, the so called lawyers — wanakwenda DAR na tayari wamepangiwa kila kitu huko kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

* Unajua system ya TZ ni ‘nzuri’ sana: kuiba mali ya Umma is OK, kuuza unga (cocaine) is OK…..na uharamia unaoujua wewe fanya, lakini usipinge muungano tu;mzee karume kasema muungano n koti kenda na maji jumbe halkathalika seif sharrif kapewa funzo sasa yuko pamoja nao  hili ndio kosa la UAMSHO!! Uamsho ilikuwa wasimame katika viriri na kusema “Muungano Oyeeeeee’, JK Oyeee, Mwalimu Nyerere oyeeeee…………hapo ungeliona mambo yao yangalikuwa super.

Sympathy ziende kwa viongozi wa UAMSHO. Ni Wazanzibari pekee wanaoitetea Zanzibar lilah taaala, bila kulipwa katika vikao vya kamati kuu au vya kiwizara, wala hawana posho au mshahara. Ni viongozi pekee genuine, with a genuine heart kwa ajili ya Zanzibar.

La mwisho, zanzibar broadcasting Corporation (ZBC) imetoa barua kutaka vyombo vyooote vya habari Zanzibar visiandike au kuchapicha au kutangaza habari za UAMSHO. Mimi nafikiri kisheria hawana mandate hii, wenye mandate hii ni Idara ya habari maelezo. Mnaona tunavyotoa maamuzi kishabik shabik hivyo? Ukwereketwa mbele. Naam….! UAMSHO CHINI, VIKOSI VYA SMZ JUU. DAIMAAAAA!

No comments:

Post a Comment