Tuesday, October 30, 2012

KITUO CHA POLISI CHA MADEMA CHAGEUKA KUWA WANTANAMO YA WAZANZIBARI


BARUA YA MZANZIBARI NAWANDIKIA NYINYI DUNGU ZETU MULIOKUWEPO NJE

“ndugu zangu za siku nyingi, nadhani watoto wetu wote hawajambo, na mimi sina hujambo kwani Zanzibar inaumwa sana na kama ujuavyo ikiumwa zanzibar na sisi tunaumwa.
“kwa kweli ndugu zangu yanayoendelea Zanzibar ni maafa tena makubwa sijui itachukua mada gani tuweze kuaminiana tena kwani hivi sasa mimi (anajitaja kwa jina lake) nawandikia lakini allah ndie ajuae kama kesho naweza amka kutokana na hofu tulioingiziwa na CCM ndani ya nchi yetu kwa malengo wanayoyajua wao. kila muda watu hupigwa mpaka hupeteza fahamu, au kupoteza maisha, huvunjwa vunjwa viungo au hupelekwa madema wakateswa mpaka wakafa kisha wanakutupa mnazi moja hospitali na kuwapigia simu jamaa zako waje kuchukuwa maiti alumuradi mtihani mkubwa. na utaratibu ndio ule ule kwa sababu anaepigwa vita ni mzanzibari sio uamsho kama inavyo fikiriwa uamsho ni kisingizio tu sasa imefikia pahala sasa hapa Zanzibar watu hawaaminiani maana utasema huyu nikimhadithi basi atanichongea nije kufatwa na kupigwa.
“taarifa rasmi jana walizikwa watu 2 mmoja kazikwa mwera meli 6 na huyu kijana mzenji ila anaishi dar es salaam alikuja kula sikukuu tu katoka shangani ameenda bububu kuamkia jamaa zake kufika wazee wa kazi wameanza kumpiga na kumpiga kichwani damu imeingia na ubongo wakamtupa hapo hapo nje na kufa. na wa pili ni kijana mdogo sana kama miaka 26 mkazi wa magomeni round about namjua mtu mzuri wamekuja askari wakamchukua na kumuuliza tupeleke waliko ubaya ubaya akawajibu mimi siwajui na jamaa ni mtu mpole sana hafahamu chochote mambo hayo basi kweupe machana wakampiga askari ni kmkm, valantia, jku pmoja na polisi watu chungu tele walishuhudia tukio hilo wakamfunga kamba mikononi nyuma na wakampakia garini kufika madema wakampiga nakumpiga tena mpaka akafariki, halafu wakamtupa monchwari jamaa zake waligoma kuchukua maiti, jana jumaapili jioni mimi nilienda kumzika mwanakwerekwe baba ake ni polisi mstaafu kwa kweli nakwambiane dungu zetu wote muliokuwepe bara ulaya,canada,amerika,oman,yemen,arabuni na kwengineko hali ni mbaya hali ni mbaya sana tena sana ndani ya nchi yetu ya zanzibar nchi imeka kama haina raisi wala sheria watu wanauliwa tu ovyo ovyo na kupingwa na kuvunjwa vunjwa viungo mimi nimepata taarifa za kijasusi pengine nitakamatwa sijakimbia na wala sikimbii wakinichukua na wakanipiga na kuniuwa ndio mwisho wa bianaadamu maana kuna askari jana amenambia.
“kwa kweli hali mbaya na hatujui tufanye nini, jee ni uamsho tu au kuna agenda iliyojificha chini ya zulia. maana Mwanza tanganyika ameuwawa kamanda wa polisi pia lakini hatujasikia kuuliwa raia wala kupigwa mtu,wala kuvunjwa vunjwa viungo mtu yoyote na la kusikitisha vyombo vyote vya habari vinakataa kuripoti habari yoyote ya mambo haya si jumuiya za kimatiaifa, wala vyama vya upinzani, yaani gizaa totoro kwa sisi rai tumekuwa kama panya tunaosakwa na mapaka,
“leo nilikuwa na  askari mmoja nimemuuliza jeee hii piga piga itaisha lini: akanambia hii haishi lengo ni kuwakatisha tamaa wazanzibari wote ili wasiendeleee na misimamo yao ya kudai nchi yao ya zanzibar hadi itakapokuja tume ya maoni mkoa wa mjini kwani mikoa iliyopita tume ya maoni wameona ccm lengo lao halitofanikiwa sasa kazi ni mjini sasa hii wanaanza kutisha ili watu woogope waende ccm pekee yao kutowa maoni na ccm wakitowa maoni ni muungano udumu na kutoka katika serekali mbili kuelekea moja huu ndio mpango askari huyo aliniambia kisha huyo akaenda zake akiniwacha nikiduwaaaaaaaa.
“sasa ndugu zanguni hali ndio hii sisi wazalendo na wanaharakati tufanye nini....??? ndugu zetu wanauliwa,wanawake wetu na mama zetu wanavuliwa nikab zao na kupigishwa vichura chura huu ndio mwanzo mwisho najuwa watawanajisi naomba tupate njia kabla yakufikia kufanya hayo tuwe tushawathibiti pia  wanateswa watu vibaya sana madema imekuwa WATANAMO YA WAZANZIBARI, wanavunjwa vunjwa viungo kikatili na hukuna hatua yeyote inayochukuliwa na yeyote tufanye nini dungu zanguni muliokuwepo nje tufanye nini sisi hapa zanzibar..........??????????????????

No comments:

Post a Comment