Monday, October 29, 2012

MARAISI WOTE WA ZANZIBAR NI WAUWAJI WA RAI WAO.


MUWAJI MPYA ALIYE LETWA KUWAUWA KUWAKANDAMIZA NA KUIMALIZA Z,BAR
Hakuna ambae anaweza kuiongoza zanzibar isipokuwa raisi muwaji kwa sasa na hapo nyuma ilikuwa pia na waliobakia wote wanajaribu kutaka kuingia madarakani kwa njia mbali mbali lakini nathubutu kusema hakuna hata mmoja ambae anaweza kuiongoza nchi hii kwa amani na utulivu zaidi ya raisi hawa wauwaji.
Kwanini nikasema hivi ,wengine watanishangaa ni kwa nini wasiweze kuiongoza zanzibar,zanzibar ina meno kuiongoza kwake sio sawa na kucheza msewe au lele mama au sunsu mia,zanzibar inaunguza.
Viongozi wote waliowahi kukaa madarakani wameondoka na roho za watu,tusitafune maneno ,wameua na baada ya kuua wamewapongeza wauwaji,ukitia kipande cha neno katika mauaji kwa kuyapa baraka na ikiwa wewe ni kiongozi basi inakuwa wewe mas-ul na ndio muuaji.
mzee Karume ameondoka na watu kadhaa wa kadhaa hawana idadi maalum na mpaka leo haikupatikana takwimu sahihi ya waliotangulia mbele ya haki katika utawala wake ambao aliwauwa.
Aboud Jumbe amewatanguliza makundi kwa makundi kuna kundi la waliohukumiwa miaka 10 ya kuchunga ngombe,akina salum ahmed na wenzake hawa walipata watu 20 kwa pamoja hawakuonekana tena mpaka leo.
Mheshimiwa Abdullwakil ameondoka na raia mmoja wa maandamano ya sofia kawawa na amewafunga wengine katika kesi za kubabikiziwa ,wengine wamepoteza macho katika kuona baada ya kuachiliwa.
Salmin ametanguliza watu kadhaa huko pemba nakubambikiza watu kadhaa kesi zisizo kichwa wala miguu hatimae wamepoteza macho kwa kuvunda rumande.
Karume mtoto amewatanguliza watu kadhaa pemba na unguja bila sababu zozote za msingi .
Mheshimiwa Ali Mhamed Shein tayari ameshatanguliza wawili na bado anataraji kuongeza idadi kutokana na mawaidha yake aliyoyatanguliza bwawani pia tukumbuke kuwa sasa analinda muungano kwa nguvu zote kwa hiyo tutarajie kuwa ataendelea kuwa na uchanguzi wa 2015 atataka kuka kwa nguvu kwa hiyo atauwa tena.
Sasa kweli ikiwa si CCM ambae anacho kibali cha kutanguliza wananchi wake mbele ya haki nani mwengine anaweza kujitokeza kumpinga CCM katika kutanguliza wananchi hao bila sababu za kimsingi na ikiwa hakuna ambae anaweza kuwatanguliza raia zake ina maana hawezi kupata uongozi wa nchi hii abadan.
Kila siku CCM wanasema nchi tumepata kwa mapinduzi na hatutoi kwa kalamu kama mnaweza mfanye mapinduzi ndio mpate nchi ,Suali yupo wa kufanya mapinduzi ? ikiwa yupo basi ataweza kupata kuiongoza nchi hii bila ya hivyo ,allahu aalam.
Hawa ndio wale waliosema(I appreciate to be honoured in hell ,rather than be dishonoured in heaven).
Sasa tuombeni dua kwani dua ni msingi wa ibada ,lakini kupata madaraka ya kuiongoza nchi inayonukia damu za wananchi halali wa nchi hii na wakaburuzwa kama kwamba si wananchi halali wa nchi hii na wakahalalishwa waliokuwa si halali na kuengwa engwa kwamba wao ni wananchi halali wa nchi hii ni habari tosha kwamba haki haipatikani,kama utaipinga CCM utakuwa huna mpya lakini ukiitukuza na wewe utatukuzwa.
Kipimo cha kiongozi wa nchi hii ni lazima uwe muuaji,mtesaji,myanyasaji na usiye na huruma na wananchi wako bila ya hivyo kaa upande na ikiwa huna sifa na uwezo wa kuwatanguliza wenzio mbele ya haki,hutaweza kudumu katika uongozi wako.
Ule uongozi wa busara,hekima ,mapenzi,uislamu
umeshapitwa na wakati toke alfu miatisa na hamsini,ulibakia ni wa manyanganya l-manyungunyu na
nipige kibao nikukate kichwa.

No comments:

Post a Comment