Monday, October 29, 2012

SHEIN NA WASHENZI WAKE WAENDELEA KUWAUWA WAZANZIBARI


mola amlaze mahali pema peponi

mola amlaze pahali pema peponi

mola amlaze pahali pema peponi

Baba wa marehemu anasimulia mtoto wake alikamatwa siku ya sikukuu mosi akipeleka ng’ombe wake malishoni na akiwa na pesa shilingi elfu 80 ambazo shilingi elfu 30 alichangiwa na baba yake. Pesa hizo alikusudia kwenda kununua godoro baada ya kumaliza kufunga ng’ombe wake. Baba mtu alipomuona mtoto wake nje ameshikwa na polisi wasiopungua 20 alikwenda kusikiliza kumezidi nini? La haula baba mtu nae pia  alipigwa na kutakiwa aondoke mara moja. Baba mtu baada ya kushuhudia mtoto wake akipata kipigo hakua na cha kufanya aliondoka na kumwacha mtoto wake mikononi mwa askari hao. Baada ya kufika jioni na kuona mtoto wake hajarejea, baba mtu alikwenda kituo cha polisi Mwanakwerekwe kumtafuta mtoto wake lakini alimkosa ndipo alipokwenda kito kikuu cha polisi Madema na kumkosa pia. Ndipo baadae akapokea simu kuwa mtoto wake ameshafariki na yupo chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mnazi mmoja na kumkuta akiwa katika hali kama hii hapa unayo iyona ktk picha 

No comments:

Post a Comment