Thursday, October 11, 2012

WALIO ZOE VYA KUNYONGA VIKUCHINJA HAWAVIWEZI BABA YAKE ALIUWA WAZANZIBARI WENGI 1964 MWANAWE APEWA UWAZIRI HARAMU JUU YA HARAMU

ccm20
Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nikithubutu kujinasibu na kujivunia sana mulhaka nilionao na chama changu mama ‘Efuru’ (Afro Shirazi).Kwamba kilikuwa chama ambacho kilitulea na kilimlea kula Mzanzibari na bila shaka kilikuwa chama cha kizanzibari kwa ajili ya wazazibari na Zanzibar yake.mpaka mwaka 1964 kikaharibu vibaya sana baada ya kukubali kuwaulisha wazanzibari na kuwapora malizao na kuwanajisi wanawake wa kizanzibari na kuwalazimisha kuolewa na mwatwana ya kibara.na kuanzia mwaka huo wa 1964 ASP hajaka na kutafakari waliyo yafanya yalikuwa ni makosa makubwa hapa duniani na kesho akhera wao wamendele kula kharamu na kuthulumu mpaka leo bado wanaendele kula vya kunyonga sio vya kuchinja maana hawaviwezi vya kuchinja washazowea vya kunyonga. Kwa hayo machache yatosha kwangu kukikata chama hicho na kuto kukipa voti yangu.
Mwaka 1977, vilipounganishwa vyama, niliona makengeza zaidi maana nilijuwa kuwa sasa ASP haramu walio ifanya haita ishaa hapo bali itazidi mpaka wazanzibari wajute kuzaliwa katika nchi hii na ni kweli sasa naam hakuna hata mzanzibari moja asiyejuta hata hao walioju wanaokula uluwa wa haramu pia wanajuta ila wanajikaza kisabuni tu. Nikaona baba (ASP) anaunganishwa na baba mwenziwe wa upande wa pili (TANU), na huku nikitambuwa kuwa mafahari wawili hawakai zizi moja, nilipata ishara kwa mbali ya kupotea kwa muelekeo wa Zanzibar moja kwa moja na pia ikanijia hisia kuwa misho kutakuwa hakuna nchi inayo itwa zanzibar naam yote yamesadikika na tayari sasa nchi ya zanzibar hii yooo inatuwaagaa.
Tukaletewa CCM, tukawamo, makobe na kasa. Kilichotokea kwa Zanzibar baada ya kuunganisha vyama hakuna haja ya kuandikwa tena hapa hata kwa sentensi moja. Mambo yote hadharani. Ila kwa ufupi tu nitie kaditama ya mukaddimati wangu wa tahariri hii kwa kusema kuwa Efuru iliondoka na mashina yake na kuiacha Zanzibar pakavu.
Porojo yote hii unafikiri imekuja kwa kitu gani? Hewalaaaaa! Nikiwa kwa sasa si muumini wa CCM wala CUF kwa sababu zangu za kwamba naamini kwamba vyama vyote hivyo aidha havina uwezo au hata nia ya kuisaidia Zanzibar na watu wake isipokuwa wao wanauwezo wa kujaza matumbo yao na familia zao hatakama zanzibar itapotea au kufa sawa alimuradi wao wanajaza matumbo yao basi kila kitu kwa soksi kilakitu kwa soksi. Si CUF wala si CCM kwa sasa labda sasa hiyo UAMSHO.
Lengo langu si kuijadili CUF kwani kwa ukweli ni chama ambacho hakina hatamu ya uongozi na walahakitakuwa na hatamu maana kishashida mara chungunzima nakisha kipokipo tu kama popo usingizi.  maamuzi makubwa ya nchi hii kwa sasa japo kuwa kwa upande mmoja ni sehemu ya Serikali kwa huku Zanzibar. Lengo langu hasa ni kuupambanua wahaka na mshangao ulionipata kuoona kuwa chama ambacho wananchi wengi wa zanzibar wamekitegemea sana, CCM, kuwa hakina nia wala malengo ya kuikwamua na kuitetea Zanzibar katika Muungano.
Nafahamu kuwa lengo la CUF si kuvunja Muungano. Pia mimi si muumini wa kuleya muungano bali ni muumini mkubwa wa kupambana na uonevu na unyonyaji unaofanywa na muungano dhidi ya Zanzibar kama vile walivyo uamsho kwa sasa. Mimi na wenzangu hatuhitaji kuvunja muungano maana hakuna huwo muungano kuna ukoloni. lakini kwa nguvu moja tunataka chama cha CCM Zanzibar kishikamane na CUF na UAMSHO kwa kuitetea Zanzibar tu. Kwani vyombo vyote hivyo vitatu ni watoto wa mama mmoja, Zanzibar tukitaka tusitaki ndio mungu ashatumba kuwa mama moja baba kila mtu wake ndio kidogo tukahitalifiana ila isiwe sababu ya kumuangamiza mama yetu zanzibar kisa tuna baba tafauti laaa laaa laa.
Kinachonishangaza leo hii na kuona na kuamini kuwa CCM haina lengo kuitetea Zanzibar badala yake ni kuinakamaisha zaidi na kusaidia kuifuta katika ramani ya dunia, ni pale tunaposikia kuwa wana CCM wote wanapinga muungano ‘wakatwe vichwa’ sio angalau kuvuliwa magamba tu.
Taarifa kutoka makao makuu ya CCM Zanzibar yathibitisha wazi kuwa viongozi kadhaa wa juu wa CCM watavuliwa vyeo na dhamana walizonazo hata wakiachwa na kadi watabaki kama mafuvu au mabupuru yasiyo kitu wala heshima katika chama ili kuwakomoa. Hali kama hii ilimfika mzee wetu Aboud Jumbe, ambae haonekani wala hasikiki katika CCM pamoja na kuwa alifanya mengi ya kuunufaisha huo Muungano na kuikandamiza Zanzibar. Mchawi hana huruma, imani wala ihsani.
Kuna taarifa za kuaminika hapo jumba la uchawi kubwa Kisiwanduwi kuwa Amani Karume atadamirishwa kwa kila hali muda si mrefu sitistajabu yakimkuta ya kumkuta maana ndio thulma inavyo kwenda utathulumu wee kisha na wewe utathulumiwa tu kama hutaki ya kukute basi bora urudishe ulicho thulumu haraka. Wengine ni Mansour Yussuf Himid, Mzee Moyo, na kambi yote ya Amani Karume iliyoshadidia mardhiano na inayounga mkono ukombozi na utetezi wa haki za Zanzibar ndani ya Muungano. Kama hayo hayajafanyika basi bado masaa na dakika tu ili yafanyike.
Lakini iwapo haya yatatekelezwa na kuwaondoa viongozi hao na mtandao wao katika chama kwa sababu tu wamedai haki za Zanzibar katika Muungano ambao kwa sasa kila mwananchi wa hapa Zanzibar , awe anautaka au hautaki, anauona kuwa hauna manufaa ya kweli kwa Zanzibar, hasa ukichukulia kuwa Muungano wenyewe umebadili sura ya umoja na kuwa ukoloni wa ndani.
Iwapo viongozi hao wa CCM watakatwa vichwa, taswira inayojengwa na CCM kwa wananchi ni ipi..? Na kisha ifikapo wakati wa kampeni CCM itawaambia vipi wananchi ambao kwa sasa wanaamini umasikini walionao ni matokeo ya unyonyaji inaofanyiwa Zanzibar na Muungano..? Hivi CCM haijui kuwa kufanya hivyo itakuwa inajikashifu...? Je CCM Ipo kwa jili ya mzanzibari au kwa WAKOLONI TANGANYIKA kuendele kunyonyo na kumaliza mama yetu Mzanzibari ili afee kabisa..?
Naamini yawezekana haya yasiwakere ya wapi watapata kura za kuitawala tena Zanzibar kwani njia ya kupitia kwenda ikulu ina tundu nyingi kwao wao na ina njia moja tu kwa wapinzani wao CUF.CCM na ikulu damu damu, ikichaguliwa isichaguliwe itaingia tu ikulu kwa nini kwasababu bado wanaendeleza haramu ile ile ya mwaka 1964 tuwauwe ili tu kae ikulu. lakini pia itazame na kusoma alama za nyakati. Kuna siku wananchi watachoka na washachoka maana tunaona vuguvugu lenavyo wiva kila kukicha.pia hao ambao bado wana imana na CCM wakibaini kuwa CCM inatumika kama kibaraka wa MUUNGANO wa kuinyonya na kuikandamiza  nchi yao ya Zanzibar basi patakuwa hapatoshi. CCM hala hala ujiti na macho, na ncha ina hoho!

No comments:

Post a Comment