Thursday, November 29, 2012

NCHINI ZANZIBAR KUBAKA SIO KOSA SIKU HIZI KUIDA ZANZIBAR NDIO KOSA-ASKARI WATATU WAMBAKA MTOTO NA KUACHIWA HURU PEMBA.MAHAKAMA YA WILAYA YA CHAKE CHAKE IMEWAPANDISHA MAHAKAMANI ASKARI WATATU KUTOKA KIKOSI CHA VALANTIA CHA KVZ KWA TUHUMA ZA UBAKAJI.
MWENDESHA MASHTAKA KATIKA MAHAKAMA HIYO MKAGUZI MSAIDIZI WA POLISI GONGO SHAABAN GONGO AMEWATAJA ASKARI HAO NI ADIBU AMABE AMEFAHAMIKA KWA JINA MOJA TU LAKINI HAKUWEPO MAHAKAMANI HAPO WENGINE NI ABDU KHAMIS NA HAFIDH YUSSUF MASOUD.
AIDHA MWENDESHA MASHTAKA HUYO AMEELEZEA MAHAKAMA CHINI YA HAKIMU MCHA HAMZA KWAMBA VIJANA HAO KWA PAMOJA WALIFANYA TUKIO HILO LA KUM’BAKA MTOTO WA MIAKA 18 SIKU YA JUMATATU YA 29-10-2012 SAA MBILI USIKU WALIPO KUWA KAZINI KATIKA ENEO LA ZSSF CHAKE CHAKE PEMBA.
WASHTAKIWA HAO HAWAKUTAKIWA KUJIBU LOLOTE KWAKUWA KUTOKANA NA MAHAKAMA HIYO KUTOKUWA NA UWEZO WA KISHERIA WA KUSIKILIZA KESI  KAMA HIZO.AIDHA AMEFAFANUA KUWA VIJANA HAO WALIFANYA KOSA HILO KINYUME NA SHERIA KWA MUJIBU WA KIFUNGU NAMBA 127{1} SHERIA NAMBA 6 MWAKA 2004  NCHINI ZANZIBAR KWA KUBAKA.
KESI HIYO IMEGHAIRISHWA HADI ITAKAPOTAJWA TENA 2-12-2012 AMBAPO YALITOLEWA MASHARTI YA DHAMANA KWA KILA MMOJA KUWA NA KIASI CHA SHILINGI LAKI TANO ZA MAANDISHI NA WADHAMINI WAWILI AMBAO KILA MMOJA AWE NA KIASI KAMA HICHO IKIWA MMOJA NI MFANYAKAZI WA SERIAKALI.JE SI VIHOJA HIVI ASKARI WATATU WANAMBAKA MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 18 NA KUPEWA THAMANA KAMA WANAKULA BATATA ZA UROJO VILE HUKU UAMSHO WANAITETEA NCHI HII ISIMEZWE NA WATANGANYIKA WANASOTA RUMANDE MPAKA LEO HAWAJEWA THAMANA WALA MAINI YA THAMANA IKO WAPI HAKI.....?WABAKAJI TENA ASKARI WAKO HURU WATETEA HAKI WANAISHIA JELA.

VIDEO-HAWA SI POLISI BALI NI MAJIZI NA MAJAMBAZI WA DR KUMBI SHEIN NA WAUWAJI WAKUBWA

POLISI GANI INAIBIYA RAI..?POLISI GANI ANAUWA..?POLISI GANI ANAMSHIKA MWANAMKE KWA GUVU NA KUMHARIBI..?POLISI GANI WANAVUNJA MILANGO YA RAI NA KUWATESA NDANI YA NYUMA YAO..?POLISI GANI HAWA SI POLISI NI MAJAMBAZI WA RAISI-SIKILIZA NA UJIONI PENI HILI LA UKWELI

MJUWEE MALKIA WA KWANZA MKAMASINI


HUYU NDIO MALKIA WA KWANZA MKAMASINI

YANAYO WAKUTA WAKINA DADA NCHINI TANGANYIKA KWA KUTAKA KUWA MATAJIRI NA MARUFUU WA BONGO MOVIE NI HAYAA.


HIVI NDIVYO WANAVYO AMINI WATU WA TANGANYIKA KUWA LAZIMA UZINDIKWE NDIO UFANIKIWE

HAYA NDIO MAMBO YANAYO WAKUTA WANA DADA WA NCHI YA TANGANYIKA NCHINI KWAO KILA SIKU WANANDANGANYWA UKITAKA UTAJIRI AU UKITAKA KUWA MARUFU AU WAZIRI MBUGE LAZIMA HAYA YAWAKUTE WANA DADA WA NCHI YA TANGANYIKA MTAZIDUKA LINI.......................? ANAE BISHA WACHA COMMENT YAKO UNIPE UKWELI KAMA HUU NI UZUSHI TU....NIGELIKUWA NASEMA TU SAWA ILA USHAHIDI HUO HAPO WA PICHA DADA ANAPIGWA PINI KISAWA SAWAA NA MGANGA WA JADI SIJUWI HATA KADANGANYWA VIPI KUWA ATAKUWA MOVIE STAR AU ATAKUWA WAZIRI HAHAHAHAHA TANGANYIKA TANGANYIKA MUTASTARABIKA LINI.......?

MSAANI MARUFU SHARO-HUSSEIN AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI-WASHENZI WATANGANYIKA WAMUIBIA KILA KITU CHAKE NA KUMUWACHA NUSU UCHI HALI YAKUWA NI MAITIBinadamu wote duniani wameumbwa na utambulisho Fulani. Ukiachilia mbali rangi, na kabila kuwa vilingo mahususi vya utambulisho wa mtu, Mila na utamaduni ni kipimo chengine kikubwa cha kuupima utu na utambulisho wa mtu au watu wa jamii Fulani. Utamaduni katika fasili yoyote ile utaingiana na mazoea yaliyoselelea kufanywa au kutendwa na watu Fulani katika jamii au jamii kwa ujumla kama sehemu ya utaratibu wao wa maisha ya kijamii. Huu huweza kuitwa utamaduni.
Ikiwa ni siku nne hivi tangu kufariki kwa ajali mbaya ya gari, msanii Chipukizi Hussein Mkeity maarufu kama Sharo Milionea, katika wilaya ya Muheza kule Tanga, matukio yaliyofanyika baada ya kifo hicho yalizidi tukio lenyewe la ajali. Kwa ufupi tu, baada ya gari la msanii huyo kupindukia na kung’oa roho yake, kilichofanyika pale ni kwa wanakijiji wa kata ile ya Muheza waliokuwepo kukimbilia kumpora maiti huyo kila kitu.
 HUSSEIN MARUFU SHARO MILLIONEA BAADA YA KUFAA NA KUPORWA KILA KITU CHAKE ALICHOKUWA NACHO KATIKA GARI  BADALA  YA KUMSAIDIA WAO WANAMPORA VITU VYAKE WASHENZI NI WASHENZI TU WATANGANYIKA NI WASHENZI WAKUBWA.
Washenzi hao walidiriki kumvua nguo maiti na kumuacha akiwa nusu uchi badala ya kumsitiri. Kitendo hichi sitaki nikitolee fatwa kuwa ni kizuri bali ni kitendo cha kinyama nasijali kusema hivyo kwani kila mtu na atakavyokichukulia kwa sasa kwa mujibu wa mila na desturi za mtu huyo. Kilichonishangaza zaidi ni wakati naperuzi kurasa za magazeti ya hapa nyumbani leo asubuhi ambapo niliona tahariri katika gazeti la ‘Nipashe’, iliyoandikwa na mwandishi maalum, yenye kichwa cha habari ‘Kupora maiti ni unyama usiopimika’. Hili lilinishangaza kwa sababu nyingi sana.
Kwanza, kwanini kupora maiti tu iwe ndio unyama usiopimika..? Kwa taswira za kimaana ya kilugha hapa tunaona kwa mbali kuwa kuna taswira kuwa mwandishi anaamini kuwa kupora si kitu cha ajabu sana kwa nchi ya Tanganyika lakini kupora maiti ndio ni unyama mkubwa zaidi. Pia Napata taswira kuwa kuna badhi ya matukio haya ya kupora ambayo mwandishi wa tahariri anayaona yanapimika au kwa kiasi hayashitui sana kwani yanastahiki kutokea hivyo. Si vibaya, ndio nikasema kila mtu na anavyouona ubaya kwa macho yake na akili yake.
Pili, hii si ajali ya kwanza mbaya kutokea maeneo ya nchi hii ya Tanganyika. Kuna ajali mbaya zaidi zilizouwa watu wengi mno na hutokezea kila mwaka si chini ya mara kumi hapa nchini Tanganyika na hasa hasa dar au mikowani. Katika matukio yote haya, jambo la kwanza baada ya ajali kutokea tu wananchi hukimbilia kuiba kilakilichopo, kiwe mwilini au kimezagaa chini, kiwe cha maiti au cha majeruhi. Huu umekuwa ndio utamaduni wa Watanganyika kila panapotokea ajali. Na kama kuna mtu anabisha ajitokeze.
GARI ALILOPINDUKA NALO HUSSEIN SHARO MILLIONEA NA KUIBIWA KILA KITU CHAKE
Kwa bahati Nzuri au mbaya, binadamu hasikii uvundo wake anaounuka mwenyewe mpaka uzidi kipimo na kuudhi mpaka masafa marefu. Hapo kwa mbali ataanza kuhisi kuwa kweli ananuka uvundo na ataanza kufikiria mbinu za kujipapatua na hili. Katika hali kama hii tunasema huwa maji yamezidi Unga. Na hichi ndicho alichokiona muandishi wa tahariri hii katika Gazeti la Nipashe.
Kuna kila sababu ya mwandishi kulaani kitendo kile kwa sasa ijapokuwa ndio mazoea ya Watanganyika katika nchi yao ya Tanganyika huko kufanya hivyo kila siku na kila mara ajali zinapotokea. Nafikiri jambo lililomsukuma mwandishi kulaani kitendo hicho labda ni kuwa aliekufa ni msanii maarufu na kwa hivyo hakustahili kuporwa na sio tu kwa sababu ni maiti. Kuna maiti kadhaa huporwa katika ajali tena huwa wengi kuliko Sharo mmoja aliyekufa akiwa pekee garini. Hatuoni maandiko yoyote ya kulaani kitendo hicho.
Sababu ya pili yawezekana na vile kuwa tukio hili la uporaji limeripotiwa wazi wazi katika vyombo vya habari sambamba na ripoti za kifo cha msanii huyo. Wachilia mbali kitendo cha kupachika picha yenye kutisha katika vyombo vya habari ya maiti ya msanii huyo kuwa ni jambo la aibu na kashfa katika mila na tamuduni za waungwana wa Kitanganyika,je tukio la kumvua maiti nguo na kumuacha hali ya nusu uchi kama ilivyoripitiwa bila kutia chenga je hili..? pia imewatia aibu watu wa Muheza,na nchi ya Tanganyika  kwa ujumla.
Na labda kwa kuchelea hili, mwandishi wa Nipashe akaamuwa kujikosha, bila kujua kuwa kukoga sio kusafika. Na kwa hili bado hatujasafika kwa kulaani kitendo cha kupora maiti, kwani huu ni utamaduni na mazoea Yawatanganyika wakiwa nchini kwao na hata wakiwa nchi za nje wanajulikana kwa umarufu wa kupora watu na kuibiya watu na kusema uwongo huwo ndio utamaduni wa Watanganyika.Ndio kwanza mkoko unaalika mauwa. Utamaduni haubadiliki siku moja, tuendelee kuulani, si kwa sharobaro tu na mabasi ya mikoani pia. Funika kombe mwanaharamu apite.

M/MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI

Wednesday, November 28, 2012

SMZ YA ZAMANI.......NA SMZ YA SASA IPI ...YENYE KULETA MAINDELEO SMZ YA SASA KAZI KUNADI MAENDELE MAENDELEO KILA LEO WALA HATUYAONI.


IBEENI NYIEE WEEE LAKINI MUJUWA MUTAVIWACHA HAPA HAPA NA MUTAINGIA HUMO KABURI KAMA MZEE KARUME ALIVYO INGIA KISHA HAPO NDIO UTAJUWA UTAMU WA UWONGOZI WAHAFIDHINA WAKUBWA NYIE NA MATHALIM WAKUBWA


Siku moja aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya watanganyika, ambae pia huitwa baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa akitembelea kisiwa cha Pemba, kikazi. Katika safari yake hiyo ya mzunguko wa kikazi ilisadifu kupitia barabara ya mkoani kwendea Chake chake. Karibu na kichunjuu, hivi kuna krosi moja kubwa sana iliyokuwa na muundo wa herufi ‘S’.
Wakati wakipita pale na msafara wa magari na jinsi njia ilivyokuwa mbovu, na makarama ya krosi ile ilivyochongeka, Nyerere hakuamini kama anapelekwa Chake chake. Akauliza;‘Tunakwenda, tunarudi?’ Akaambiwa tunakwenda, il’hali gari ikiwa limeelekeza uso kule linakotoka na likiendelea na mwendo ule ule katika msafara. Nyerere akasubiri ajionee kioja, akatulia.
Miaka zaidi ya 30 tangu Nyerere aulize suali hili, na sasa ni karibu miaka 13 tangu Nyerere afariki, hakuna mmoja wetu aliepata kufikiria falsafa ya maneno haya, yaliyochukuliwa kama mzaha wa Nyerere tu wakati hule na hadi sasa. Kusema ukweli maneno haya hayakustahili kutiwa kapuni na kama kuna aliyefanya hivyo amekosea. Ndio maana mimi nilie yaweka hakiba leo nayavongonyowa na kuwatunukia. As’aa huenda mukazinduka.
Zanzibar, nchi kinyonga, mara nchi, mara si nchi, vyovyote tukavyoiita, itaitika. Hadi sasa Visiwa hivi vinapata umri wa miaka isiyopungua 48 tangu kuachwa na mkoloni mweupe na kuvamiwa na mkoloni mweusi. Miaka hii si kidogo hasa kwa kuyatathmini maenddeleo yetu na ya nchi kwa ujumla. Naamini huu ni wakati muafaka wa kujiuliza, ikiwa SMZ ndie mtawala mkuu wa visiwa hivi tangu miaka hio, na anaehubiri maendeleo kila uchao, tuiulize Serikali yetu ya SMZ suali lile lile, ‘TUNAKWENDA, TUNARUDI?’
Nchi hii ilikuwa ina maendeleo makubwa na ilikuwa na hakiba isiyomithilika katika mahakibizo ya fedha duniani mpaka zama za miaka ya mwisho ya 70. Serikali zetu za SMZ zilizopita zilikuwa zimetawaliwa kimabavu kweli kweli lakini mengi tuliyaona sasa hatuyoni tena. Ndani ya miaka minane ya Abeid Karume, tulipata majumba makubwa nchi nzima. Tukajengewa hosipitali na vituo vya afya.
Ndani ya miaka ya Karume, Jumbe hadi karibu ya Ali Hassan Mwinyi, wazee wakipewa pesa za matumizi zikiitwa ‘ulufea’ (Welfare benefits) na zikiwasaidia sana. Wakati wa tawala za SMZ za siku hizo sio sasa mukumbuke, hosipitali zilikuwa zimejaa madawa, usafi na huduma za kila aina. Skuli zetu zilijengwa hatua kwa hatua, hakuna alielipia mchango wa skuli, hakuna alienunua daftari, kalamu wala penseli. Hakuna mwanafunzi aliekosa huduma za afya za kichocho, vipimo kila muda Fulani.
Ilifika wakati kwa jinsi Serikali ilivyo kuwa ikiwajali wanafunzi, Waziri wetu wa Elimu wa mwanzo hapa Zanzibar, aliwahi kupendekeza kuwa vichwa vya Ng’ombe vyote vinavyochinjwa nchi nzima vipelekwe mashuleni wanafunzi wapikiwe supu, ili wapate wanywe wakati wa mapumziko (recess) nikichikesho ikisikia sasa. Bahati mbaya mpango huu ulivunjwa na Sheikh Karume, pale alipomwambia Waziri wa Elimu kuwa asijefanya hivyo mpaka ahakikishe kila mwanafunzi ameshapata kijiko na kibakuli cha kunywea supu. Mapango huu ukafa hapo, lakini ulikuwa na nia njema.
Enzi za SMZ ya wakati huo sio ya sasa vurugu mechi na wizi, kulikuwa na huduma za dakhalia (boarding). Ukipasi ukipelekwa huko kupatiwa mafunzo ya kuwa mtu utakaejitegemea. Tukipewa kula asubuhi mchana na jioni. Japo tukiita bondo, lakini tukipewa tena bure na kwa wakati bila kuchangishwa gharama. Wanafunzi wakiletewa meli bure kupanda au wakifanyiwa tiketi kabisa wakifika huchukuwa na kusafiri tu kwenda Unguja na Pemba. Tuache huko.
Hospitali, kula kunywa na huduma masaa ishirini na nne. leo kula ishaondolewa hospitali ya mnazi moja maendeleo hayo. Mgonjwa akipembejewa na madaktari wa kikwetu na wa kigeni wakati huo leo matusi mpaka utarudi kwenu na maradhi yako. Serikali haikuwa na meli zilizoenda kwa kasi wala madege, lakini watu wakisafiria meli za Serikali za uhakika na unafuu wa bei. Huo ndio wakati ambao tunaweza kuusema kuwa nchi yetu ilikuwa changa, na ilikuwa na matongo ya ukoloni mweupe kabla ya kutiwa matungoo ya mkoloni mweusi tanganyika, haikuwa na uoni wa mbali wala uwezo wa kutuletea maendeleo.
Tupige dira ya SMZ leo. Serikali yahubiri na kutangaza kila siku kuwa nchi hii imepiga hatua kubwa kimaendeleo ukilinganisha na Zamani hahahah nacheka kwenza ahahahahaha. Sikatai. Maendeleo wakati mwengine hupimwa kwa miwani ya macho, ambayo kigari kidogo huwa TATA, au FUSO. Maendeleo siku hizi hupimwa kwa kutazama ndege zipitazo juu ya anga letu, tivii pana majumbani, au kila mtu ana simu ya kiganjani. Maendeleo yetu hupimwa kwa viongozi kuwa katika magari makubwa ambayo wakiwa ndani ya magari hayo hawasikii ule uvundo unaonuka pale Darajani kituo cha dala dala wala hawawasiki wanachi walio waomba kura kabla hawajapata hayo magari makubwa.
Maendeleo hupimwa wakiwa katika magari ambayo pia yakipita njia mbovu hawahisi wala hawapati vumbi mle ndani. Na pia licha ya kuwa nchi ina joto la tanuri ya mbata siku hizi kwa uchafuzi wa mazingira, viongozi wetu wa SMZ hawalihisi joto hili na vuke kali, katika magari na majumba yao yaliyo ‘full kipupwe, full kiyoyozi, full kujiachia’. ahahahaha nacheka kwanza maana nikilia nitaumiya moyo bora nicheke. Raha zote hizi zilizowazunguka viongozi wetu unawategemea kuwa siku moja watasema kuwa nchi hii inarudi nyuma badala ya kwenda mbele..? Ungekuwa wewe ungetia ulimi wako puani ukasema ukweli huu wakati yote hayo huyaoni kwa maraha yaliyokuzunguka...?
Hebu linganisha hayo machache niliyoyasema yalifanywa, enzi za Karume, Jumbe na kidogo Mwinyi na uone. Sasa tudurusu kwa pamoja. Nitawauliza maswali munijibu mpaka nimalize, sawa...? Bismillah! Ule ‘ulefea’ bado upo..?, Skuli zetu zina vifaa...? madafatri na kalamu bure..? Dkahalia zipo...? Elimu bado ni bure..? Ndio ni bure maana haina maana yoyote, lakini inalipiwa. Samahani hili nimejijibu mwenyewe. Haya tuendelee.
Kule spitali dawa ziko...? Ndio lakini kwa pesa duuh nimejibu mwenyewe tena. Kile chakula vipi bado wanapatiwa wagonjwa...? Ahh! Bajeti ya Wizara ya afya ndogo..?, kimefutwa Chakula. Lakini Waziri wa Afya ana prado la milioni 70, na mafuta yake ya laki moja kwa wiki pengine. Hawasemi kuwa mawaziri waendeshe gari ndogo kama Starlet, na Vizt kujenga taifa. Heri wafe wagonjwa wao waendeshe magari mazuri. Ndio sisi bwana, wakoloni weusi. Nani anajali kama wagonjwa wanakufa kwa kutukanwa tu kule Spitali, kwa kukosa dawa tu na hata kula sasa..? Hawa ndio viongozi wetu bwana, ni zaidi ya majoka ya mdimu.
Madakatri jee wanashuhulikia wagonjwa...? Hapana, wanawatukana wala hakuna anejali serikalini kwani wao hawatibiwi hapa hata wakiumwa na tambazi (uvimbe) huenda nje ya nchi. Kwanini..? Tumeendelea hivyo. Tuendelee, au mshachoka...? Mmeona wapi Serikali kujenga tena majumba ya watu na makazi...? Hapana. Ule usafiri wa meli dhamana za Serikali ukalipo..? Hapana zilizopo ni za matajiri na hata tukizama SMZ husema, haina la kufanya. Tumezama, tunazama, na tutaendelea kuzama. Ndio maendeleo!!!!
Ya kale hayako tena, kweli. Lakini pia ya sasa hayapo na wala tusiyatarajie. Nchi hii kama ingekuwa gari, mmoja kati ya madereva hawa saba tuliojaaliwa na Chimwaga kutuongoza, lazima bila shaka alizitowa gia zote na kuibakishia gia ya kurudi nyuma tu (reverse gear). Na ndio hivi tunapelekwa msobe msobe. SMZ wakisimama majukwaani, huhubiri chuki, na uhasama na uongo mwingi kisha wakikutana katika vyombo vya habari husema wameleta maendeleo. Hivi ni kweli jamani. Sikupata nafasi ya kuchambuwa sana lakini mpaka hapa tu jiulize ndugu yangu.
‘TUNAKWENDA, TUNARUDI?’

HOSPITALI YA MNAZI MOJA IMEKUWA MTOTO WA GETI KALI KUINGIA MIA 500 HATA KAMA UNALETA MNGONJWA DUUUUUUUUH!!!!Moja kati ya agenda kuu ya Kitumwa cha watanganyika, Dr. Kumbi Ali Mohammed Shein, ni kuikuza na kuindeleza hospital kuu ya Mnazi Mmoja — iwe ya ‘Rufaa na kimataifa’.
Bahati nzuri Dr Kumbi.Shein naweza kusema ni ‘kindaki ndaki’ wa hospital hiyo anaijua A-Z, kuanzia mazoezi, na hata kazi amefanyia hapo; mpaka ameondoka na kuingia katika siasa ametokea hapo; pia kama Kibaraka cha watanganyika, ofisi yake akichungulia anaona wodi ya watoto, laboratory aliyokuwa anaifanyia kazi n.k.
Kwa kweli yeye na Mnazi mmoja ni kama mtu na ‘mwanawe’.
Pamoja na hayo, hospital ya Mnazi Mmoja inakabaliwa na matatizo mengi, likiwemo kubwa sana na UBINAFSI.
Mfano mzuri, mpaka sasa sioni sababu kwa NINI kuingia hapo hosp, lazima ulipie sh.500/= kama ukiingia na gari hata kama gari hiyo ina mgonjwa ndani yake; kuna mnyororo pale lazima ulipe utake usitake.
Huu sio ubinadamau hata kidogo, na tunakuambia Juma Duni Haji, na bosi wako, Dr Kumbi.Shein muchukue uamuzi wa kuondosha mnyororo huu (kama kweli ni viongozi wenye mamlaka) au kama ni masheha tu, na ubabe wao ni kwa UAMSHO, tujue.
Kinachofanyika pale ni dhulma. je, pesa zile zinazokusanywa shl 500 pale, zinaingia katika mfuko gani?
Isitoshe, mara moja walisababisha msongomano pale, na msafara wake dr Kumbi.Shein unakuja speed kubwa kuingia Ikulu, hapo ilikuwa tafran kubwa. Eneo lile kiusalama si eneno linalohitajika msongamano.
Mgonjwa huyo, alipie kulipia kuingia humo hosp mumesikia wapi hata nchi zilizo endelea na hospitali zao nzuri kama hoteli basi kuingia hulipi itakuwa hapa uko viwaja vya maisara harufu ishakuva kisha ukingia ulipe thulma mpaka hospitali basi kwa gari, alipie cheti, alipie X-Ray, alipie kumuona daktari, alipie choo, akitaka kujisaidia — jamani kweli haki hiyo?
Wakati fulani, niliwahi kumueleza waziri wa Afya aliyepita, Sultan Mugheir, kadhia hii — kuna kipindi alinifahamu, na aliondosha huu mnyororo wa hosp. Sasa umerudi tena.
Maalim Juma Duni (Babu Juma), Dr Kumbi Shein, Maalim Seif, na Balozi Seif Ali Iddi wa tanganyika, msiwakamue wananchi sana kiasi hicho, give them a space please, basi hata kuingia hospital na mgonjwa watu walipie, au kuja kuangalia mgonjwa. Jamani hebu kuweni binadamu japokuwa kidogo.
Mambo muhimu kama usafi wa vyoo, huduma za chakula, huduma za matibabu n.k hizi zote hakuna hapo, ila kuchukua pesa kwa kila ‘inayoitwa huduma’ lazima ulipie hata kama hutoipata.
Utalipia X-Ray, lakini unaweza kuwa hutoipata huduma hiyo, hizo zinazoitwa city scan kadhalika.Mpaka chakula sasa hakuna pale hospital, na ukitaka ulipie. Shabash!!!!!!!
Unajua wananchi wengi wa Zanzibar walaitegemea sana GNU inaondosha uonevu kama huu, usiokuwa na maana, YES, hawakutegemea utajiri bali angalau maudhi madogo madogo yaondoke, lakini yamezidi.
Ahhhh…..sifikiri kama uongozi wa juu utanisikiliza, maana hawana utamaduni huo, wa kusikiliza wananchi wa chini, wao ni ubabe tu — SMZ-GNU kwa kweli imeoza sana, haina tija kubwa sana kwa wananchi walio wengi (ubabe dhidi ya Uislamu, na waislamu, wanafunzi wanafelishwa kwa visingizo tofauti, wafanyakazi wanachakachuliwa mishahara yao na officials wa wizara, kuna waliokufa na meli, fidia zao mpaka leo mtihani — haya yote na mengine  mtumwa wa watanganyika Shein, huyaoni, wewe msimamo wako na serikali yako ya udikteta kupitia DPP office, UAMSHO wasote rumande mpaka wafe humo humo).kiyama utasema nini kwa m/mungu wewe kibaraka wa watanganyika..?
Mimi naomba mwanasheria yeyote wa ndani na nje ya nchi, anieleze je, kuna kesi ya kujibu kwa akina Farid na wenzake..? Na mengine mengi —- na hili la hospital linatukera tena linatukera sana.
Dr Kumbi Shein ulisema kuwa wanaokwenda kujifungua kwa ‘mkasi’ wasilipie, hii mpaka leo wanalipa tena nyongeza inadaiwa pia ya kulipa zaidi.
Na ukijifanya unahoji, unaambiwa ‘kwamitwe huyo dr.shein’ aje akutibu yuko nyuma ya ukuta hapo, akupasue….au utaoza hapo hapo! hayo ndio majibu unayopewa wodi ya wazazi ……! Kweli haya hayajui huyu  Dr Kumbi Shein…….ina maana anapelekewa habari potofu za UAMSHO tu. Dr Kumbi Shein,habu isome hii au wasaidizi wako waisome hii – kuwa bado wazazi wanaokwneda kujifungua kwa mkasi ‘wanalipishwa pesa nyingi tu’. Ulisema katika baraza la Eid el Hadji ‘enough is enough’ — tunataka tuone na hili ubabe wako wa ‘enough is enough’ unalifanyia kazi.

SEREKALI YA GNU-SUK-YA ZANZIBAR SASA SIO SEREKALI YA DEMOKRASI TENA BALI IMEKUWA SEREKALI YA HITLER KUWAFUGA WATU JELA,KUWA WATU,BILA YA SABABU YOYOTE.TUNAAMBIWA kuwa hapa nyumbani na nje katika mfumo wa utawala bora wa haki na sheria dhamana kwa mshitakiwa ni haki, japokuwa mahakama ndiyo yenye uamuzi wa mwisho juu ya suala hili.
Nchi nyingi zenye utawala wa demokrasia zimeweka utaratibu unaojaribu kwa kiasi fulani kuhakikisha mahakama hazitumii vibaya mamlaka yake katika suala la dhamana.
Hii ni kwa sababu ipo dhana yenye nguvu inayosema kumuwekea mshitakiwa masharti magumu ya dhamana yanatoa tafsiri ya kuwa sawa na kumnyima dhamana au kuanza kumuadhibu mtu hata kabla hajatiwa hatiani.
Katika baadhi ya kesi zinazoendelea Zanzibar hivi, hasa zile zenye harufu ya kisiasa, kuchimba almasi au dhahabu ni rahisi kuliko kupata dhamana. Hali hii imesababisha baadhi ya watu,Visiwani na nje, kuuliza kwa kiasi gani mahakama za Zanzibar zipo huru? Mimi ukiniuliza jibu langu ni kwamba nasikia kuwa zipo huru, lakini sizioni kuwa huru.
Baadhi ya watu Visiwani, hasa wanasheria, wanasema panapokuwepo kesi zenye mashiko ya kisiasa ya aina moja au nyingine mahakama za Zanzibar huwa zinendeshwa kwa kitufe cha mbali (remote control).
Maelezo haya yamepata nguvu kutokana na mahakimu na majaji kueleza mara nyingi kuwa wamekuwa wakipewa amri na wakubwa, baadhi ya wakati kwa kutumiwa vikaratasi, juu ya namna wanavyotakiwa kuendesha kesi.
Unapokuwa na mtindo wa aina hii, hata ikiwa kwa kesi chache sana, basi majumuisho unayopata ni kuwa mahakama hazipo huru na kwamba zimegeuzwa kuwa sehemu ya utawala badala ya kuwa eneo lililo huru na linalotoa na kulinda haki.
Mahakama za Zanzibar hivi sasa zimekuwa zikitoa masharti ya dhamana ambayo unaweza kusema magumu sana au hayatekelezeki na hali hii imezusha wasi wasi juu ya huo uhuru wa mahakama unazungumzwa.
Zanzibar imekuwa na sifa ya kuweka masharti magumu ya mtuhumiwa kupewa dhamana na baadhi ya masharti haya ni ya aina yake na ya kipekee ambayo husikii kuwekwa Tanzania Bara au katika nchi yoyote ile inayojinadi kuwa na mazingira ya utawala wa haki na sheria.
Baadhi ya masharti haya, kama nilivyoeleza siku za nyuma, yana sura chafu ya kuwabagua raia na kuwaweka katika madaraja mawili, moja la watukufu na lingine ni la watu ambao mahakama haitaki kuwaamini.
Hawa watukufu ni wale wanaofanya kazi serikalini na wasiostahiki kuaminiwa na kuheshimiwa ni wale ambao sio wafanyakazi wa serikali.
Siku hizi imekuwa kawaida kusikia mshitakiwa anaambiwa kwamba wadhamini wake lazima wawe watumishi wa serikali wakati inajulikana wazi kuwa mtumishi wa serikali hawezi kuhatarisha ajira yake kwa kukubali kuwa mdhamini katika kesi ambayo watuhumiwa wake wamekuwa wakizungumzwa na viongozi wakuu wa nchi.
Mfano mmoja ni wa kesi inayowakabili viongozi wa jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho. Hivi mfanyakazi gani wa serikali atajitokeza kuwawekea dhamana? Tusidanganyane, huu sio mchezo mzuri na ndio maana wananchi wengi na hata hao tunaowaita washirika wetu wa maendeleo wanauona hauonyeshi haki kutendeka.
Au vipi kijana ambaye hana hata kiwanja utamtaka aweke dhamana waraka wa nyumba wakati hata hivyo viwanja hugawiana wakubwa na watu wanaohusika na ugawaji hujigawia wao, watoto, wake zao na hata wajukuu? (angalia ripoti ya tume ya uchunguzi juu ya ugawaji wa viwanja). Kama majina ya kweli na sio ya bandia ya watu waliopewa viwanja yatawekwa hadharani utaona watu hoe hae kama akina Salim Said Salim ambao hawapo tayari kuwaabudu viongozi kwa ajili ya kutaka vyeo au kulinda urafiki hutayaona.
Majina ya waliopewa viwanja yatawekwa hadharani. Sasa vipi mtu masikini utamtaka aweke kaburi la mzee wake. Jamani zama za kuifanya Zanzibar kuwa na haki ya kufanya tutakalo, licha ya kutia saini mikataba ya kimataifa ya kuheshimu haki za binaadamu, ikiwa pamoja na za washitakiwa, zimepita. Siku hizi nchi haziruhusiwi na hzivumiliwi ukiukaji wa haki za binaadamu au za washitakiwa.
Mtindo huu wa kuwabagua watu wa Zanzibar kwa mafungu ni wa hatari na utaiathiri Zanzibar.
Fikiria serikali itahisi vipi kama watatokea watu na kusema wanaoruhusiwa kuingia katika hoteli au maduka wanayoyamiliki ni wale tu ambao sio watumishi wa serikali? Kama serikali kupitia mahakama, ina wabagua watu kwanini na wananchi nao wasiwe na haki ya kuendeleza sera hii ya ubaguzi kwa kutumia mali zao?
Lakini kama serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar inataka kurejea tulikotoka ambapo kulikuwepo mahakama za wananchi (mahakimu wazee wanaosinzia hovyo) na kutojali uhuru wa mtu na hata kutoa hukumu kabla ya kesi kusikilizwa basi serikali isione aibu kutamka hivyo.
Kinachosikitisha ni kuona haya yanafanyika wakati Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ile ya Mkurugenzi wa Mashitaka inaongozwa na watu wenye kuheshimika katika fani ya sheria, lakini wamekaa kimya kama vile kutoa masharti magumu au kumnyima mshitakiwa dhamana ni jambo zuri na linalofaa kupongezwa.
Nilitegemea wanasheria wenye kuheshimika kama hawa wawili wanaoongoza taasisi hizi muhimu za serikali, wangejitokeza kupinga mwenendo huu wa kibaguzi, lakini inaonekana wameweka maslahi yao mbele kuliko yale ya kulinda haki na sheria.
Wazanzibari waache utamaduni wa kulindana kwa maovu. Watu anaojiita waungwana hulindana kwa mambo mazuri na sio mabaya, hasa yale yanayoitia nchi dosari. Lakini hata jumuiya za kiraia zimekaa kimya, labda kwa kuhofia msajili kuzifuta, lakini ukweli lazima usemwe, potelea mbali liwalo na liwe.
Wazanzibari wanataka kuwa na utawala wa haki na sheria za kweli na sio bandia kama inavyojitokeza sasa. Wazanzibari wengi walikuwa na imani na matumaini makubwa na serikali ya umoja wa kitaifa katika kusimamia haki na sheria, lakini kinachoonekana hivi sasa ni kwamba ndoto yao haikuwa ya asubuhi, mchana wala usiku.
Hakuna kitu kibaya katika nchi inayojigamba kuwa na utawala wa kidemokrasia, halafu zikaweopo dalili za vyombo vya dola na mahakama kutumika vibaya na hasa kuridhia kile kinachoonekana kama utashi wa kisiasa.
Mpaka sasa viongozi wa Uamsho hawana kosa mpaka pale itapothibitishwa bila ya wasi wasi wowote na mahakamani kuwa shutuma zinazowakabili ni za kweli na sio za kusingiziwa au kubunia.
Watu waliokabiliwa na mashitaka ya kuingiza dawa za kulevya ambazo zinaathiri maisha ya mamia ya watu, waliodaiwa kuiba mabilioni ya fedha, waliodaiwa kufanya uzemba wa meli kuzama na watu wengi kufa na wanaosemekana wameajiri wafanyakazi hewa na kuitia hasara serikali wamepata dhamana.
Ni muhimu kuelewa kwamba dunia ina tuangalia na kutucheka. Tufanye mambo mezani na kutumia hekima na busara. Vile vile tuelewe kwamba dunia inatuangalia na hapo tutakapolaumiwa kwamba tuliziendesha mahakama zetu hovyo tusije tukasema tunaonewa. Tujuwe kuwa hatimaye tutapanda tunachovuna, lakini historia itatukumbuka baadhi yetu kuwa tulikataa kupalilia mbegu mbaya.

Monday, November 26, 2012

HUMAN RIGHT ABUSE IN ZANZIBAR ISLAND

  

REF: HUMAN RIGHTS ABUSE IN ZANZIBAR ISLAND
Recent developments in Zanzibar show that the authorities there have taken a big step backwards in terms of human rights.   Rampant and deplorable human rights abuses came to light during a series of events which led to confrontations between the police and followers of an Islamic organisation called UAMSHO (Awakening).
UAMSHO, a registered NGO, has been active in Zanzibar for a number of years now.  In addition to its religious activities, it has taken part in observing elections, has produced well-researched reports on past elections and has provided civic education to the populace.  The organisation has a wide grass root support within the community. Recently it has been actively championing for the restoration of Zanzibar’s sovereignty.
The government has accused it for inciting its followers to commit unlawful activities. UAMSHO denies it and has on its part accused government security apparatuses of inflicting harm on its followers during their peaceful demonstrations.  This pattern of accusations and counter accusations culminated last month with the three day mysterious ‘disappearance’ of a charismatic leader of UAMSHO, Sheikh Farid Ahmed Hadi.  UAMSHO maintained that the Sheikh was abducted by the security forces, a charge which the government denied.
However, when Sheikh Farid resurfaced he too intimated that he had been abducted by the security organs.  The government’s response was to promptly arrest him together with his fellow leaders and to charge with several criminal offences.  This came as no surprise as for weeks rumours were rife that the government was under pressure by diehards of the Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania’s ruling party, to ban UAMSHO. It is not our intention to judge the merit or demerit of the case as it is sub-judice.

What is troubling us is the well prepared measures to humiliate all the detainees connected with UAMSHO. By their actions the state organs have shown that they are bent on humiliating and dehumanizing the UAMSHO detainees.  For example, despite knowing very well how Muslims sheikhs cherish their beards the sadist jailers have found it proper to forcefully shorn them of their beards.  They did it even before the accused were brought to court for the first time.  Defence lawyers have publicly complained of other forms of mistreatment meted out to the detainees.  These include, denying them the opportunity to offer their obligatory prayers, denying them a change of clothes since their arrest and inhuman prison conditions. No doubt the jailers what they do to satisfy their primitive sense of power, to show Zanzibaris that they are capable of doing whatever they want to do and nobody can question them.
It is sad to note that the government has remained silent to all these injustices. The detainees constitutional rights are denied. The protests of their lawyers have fallen on deaf ears. In the meantime, indiscriminate harassment of ordinary citizens continues unabated. All those suspected of being sympathetic to UAMSHO are publicly brutalized. It reminds us of the dark days of Zanzibar when there was no respect for human rights.
We, therefore, appeal to all human rights activists to urge the Tanzanian and Zanzibar governments to impress upon their state organs the urgent need of according each and every citizen their human rights.


Tuesday, November 20, 2012

MUUNAUTAKA AU HAMUTAKI-JIBU HATUTAKI HIVYO NDIVYO ALIVYO ULIZA SHEIKH FARID ALIPOKUWA AKITOKA MAHAKAMA YA VUGA LEO NA KURUNDISHWA RUMANDE NA MAMIRI WENZAKEViongozi wa jumuiya ya uamsho wanaodaiwa kusababisha vitendo vya uvunjifu wa amani Visiwani zanzibar wamefikishwa kwa mara nyengine katika mahakama kuu ya vuga kwa ajili ya kutolewa ufafanuzi juu ya malalamiko yaliyotolewa na mawakili wao dhidi ya vitendo wanavyofanyiwa wateja wao wanapokuwepo gerezani. Ikiwa ni pamoja na kukosa uhuru kitu ambacho ni kinyume na haki za binaadamu.
Viongozi hao walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tatu kamili barabara asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa gari nne za askari wa kutuliza ghasia {ffu}, huku wakiwa wamevalia kikazi zaidi.
Mapema baada ya viongozi hao kushushwa katika gari lilokuwa limewabeba alisikika Sheikh Mussa Juma, ambaye ni mmoja wa washtakiwa hao, akiwaambia waandishi wa habari “Nyinyi waandishi wa habari njooni gerezani kuchukua habari jinsi tunavyonyanyaswa sio mnachukua hapa tu”
Kabla ya kuingizwa washtikiwa hao katika chumba cha kesi askari polisi walianza kuwatawanya wananchi waliofika mahakamani hapo pamoja na waandishi kwa njia za amani ili kuweza kuondoa usumbufu katika chumba hicho. Lakini wakati huo huo wakamchukuwa kijana mmoja ambae alikua akipiga picha matukio hayo kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Nae mwendesha mashtaka wa kesi hiyo george kazi ametoa ufafanuzi juu ya malamiko ya washtakiwa hao na kusema mahakama haina haki ya kuvilazimisha vyombo vya ulinzi kutenda haki kwa washtakiwa hao, hivyo amewaomba mawakili wa viongozi hao kufungua kesi katika mahakama kuu ya vuga kwa lengo la kudai haki hizo.
Aidha amesema bado upelelezi wa kesi yao bado unaendelea hivyo ameamuru washtakiwa hao kurejeshwa tena rumande hadi tarehe 29 mwezi huu.
Wakati washtakiwa hao walipokua wakiingizwa katika gari kwa ajili ya kurudishwa rumande sheikh mussa alirudia tena maneno yake aliyoyasema mwanzo huku akiungwa mkono na sheikh farid kwa kusema zanzibar itapatikana, na baaadae kuwauliza wananchi “mnautaka muungano” na wao kujibu huku wakipiga takbiri katika mlango wa mahakama “hatuutaki”
Wakati huo huo wakili wa washtakiwa hao bwana Salum Tawfiq ameziomba familia za washtakiwa hao kuendelea kupeleka baadhi ya huduma kama vile chakula ingawa hawaruhusiwi

Sunday, November 18, 2012

KUMBI SHEIN UWONGOZI UNA MWISHO WAKE WEWE KICHWA CHA SAMAKI


HUYU NI KUMBI SHEIN ALIPORUDI KUTOKA DODOMA
Binaadam yeyote ambae ana akili timamu mara zote huwa ni kiumbe chenye kufikiri sana hatma yake,lakini la msingi kabisa ni fikra inayo muunganisha baina yake na Mola wake na kujua nini hasa lengo la kuumbwa kwako kama Binaadam kamili .
Licha ya Mola wetu kutupa hidaya hii muhimu,hakutosheka na hilo bali pia katupa utukufu na daraja kubwa sana pale alipotupa hidaya nyengine baada ya kwisha kutuumba yaani akili kwa Mwanaadamu,lengo ni kufikiri na kuelewa majukumu yetu kama binaadamu na tupo hapa Ulimwenguni kwa misingi gani.
Mola wetu ametuekea bayana kwa Mafundisho sahihi kwa kumleta Mtume wake na Kitabu chake kitukufu ili tupambanue mustakabali wetu kati ya mabaya na mema. Vile vile hakuishia hapo kwa kutuweka njia panda lahasha ! bali tumebashiriwa pepo kwa watenda wema na pia moto kwa watenda maovu.
Kutokana na mantiki hiyo ni kuonesha kwamba kila lenye mwanzo basi halikosi kuwa na mwisho. Hata hii dunia tunayoringia basi nayo pia ina mwisho wake,hatuna budi kwa Waumini kukumbushana katika hili.
Ikiwa hivyo ndivyo basi ni vyema kwa Kumbi Shein na Kaumu yako mukaelewa kwamba uongozi ni dhamana na Urais una mwisho wake.Yeye kama kiongozi aliejitwisha joho hilo ana dhamana kubwa amebeba na masuala makubwa ya kwenda kujibu kesho yaumu -likyama yanamngojea hili halina mush-keli kwa wenye kuamini.
Mabeni ya wafuasi wako lakini pia na Washauri wako wa karibu Kumbi Shein haitokuwa kinga ya siku hiyo itakayo kufanya uwachwe hivi hivi tu usiulizwe masuala kutokana na jinsi gani ulivyo upata ufalme wako na jinsi gani ulivyowatumikia Wazanzibar. Siku hiyo hapatakuwa na Kizota wala Dodoma bali ni wewe kutoa majibu sahihi mbele ya haki ili kila Mzanzibar apate haki yake.
Kumbi Shein inaonesha dhahiri kwamba Ufalme unakutia kibri na jeuri na kuona kana kwamba utadumu kwenye Ufalme huo milele,hilo haliwezekani.Chini ya uongozi wako Wazanzibar wanazidi kudhulumiwa na wewe hilo unalifurahia na kulishadidia kwa vile wewe uko Madarakani. Kuna watu wanakushauri vibaya ili uzidi kuwanyima haki Wazanzibar unaowatawala huku wao wanafaidika na hilo.
Kumbi Shein uifikirie pia nafsi yako na hatma yako kesho mbele Muumba umeshajindaa na majibu mazuri ? Lengu langu ni kukumbusha tu kwani wakati mwengine sisi ni Binaadamu tunajisahau na kuona huo ulwa umeupata kwa akili zako na usomi wako wa kichwa cha samaki usiye juwa hata muungano wa mkataba. Wako viumbe wengine hawakuwa Madokta lakini waliongoza kwa Ik-lass hilo ulijue.
Kumbi Shein Wazanzibar wanadai haki zao za msingi kama alivyo amrisha Mola wetu,lakini kutokana na wewe na Kaumu yako kuona matamanio ya kidunia ni bora zaidi, haki hizi unazifumbia macho,matokeo yake unakuja na kibri na kejeli kwa Wahusika,huoni kwamba mwisho wa yote hayo Urais una mwisho wake ? Unajua dhahiri kwamba Wazanzibar wanadhulumiwa lakini wewe na Wapambe wako maslahi yenu yanawaendea,kumbuka hayo yana mwisho.
Nakupa mfano mdogo tu Kumbi Shein tokea Mapinduzi ya 1964 ni Marais wangapi wameshapita kukalia kiti hicho ulicho nacho na hii leo wako wapi ? Kumbi Shein jawabu wewe utakuwa unalo,lakini kumbuka leo hii hawatajwi tena katika ulwa huo,kilichobakia ni majuto na huzuni tu, kumbuka na wewe utakuwa miongoni mwao. Mali na majumba utayawacha hapa hapa,ila haki za msingi za wale mulio wadhulumu hizi hazitokufa abadan.mfano mwengine mzee karuma kalala pale kisiwa nduwi na majumba yake kayawacha hapa hapa basi na wewe ndio hivyo hivyo utaviwacha hapa hapa.
Kumbi Shein muda unao  uyafikirie hayo,kuwalaani baadhi ya Wazanzibar na kuwaseka ndani sio suluhisho la Wazanzibar kutokudai haki zao za msingi bali unazidi kuwasha moto kwa kizazi kipya kilichopo na kinachokuja hapo baadae. Kumbi Shein kumbuka kwamba chuki hizo munazozipanda mizizi yake haitaishia hapo tu bali matunda yake yatachanua.
Kifungo kile ulichowatia wale unaowaita wavunjaji wa Amani elewa si chochote bali ogopa kifungo cha Mola wetu hakuna anaekiweza. Iko siku madhila ya Watu wale utakuja kuyaona pekee yako bila Washauri wako au Chama chako.

HII NDIO CCM NAKILA ANAYE IFUATA AJUWE NDANI YA KICHWA CHAKE HIVI NDIVYO KILIVYO,MKITAKA MSITAKI MABADILIKO YATAKUJA TUUNyerere laana ya m/mungu imfikie huko huko aliko alithubutu kumwita Kolimba na Malecela kama ni wahuni, kwahiyo Uhuni umejaa CCM na kwa kweli kama tutaendelea kuwa ndani ya utawala wao tujuwe nikuzama na wahuni hao wapo tayari kufanya lolote lile almuradi kupata maslahi yao, ikiwa kuuwa, kuiba, kufitini liwe lolote lile baya, muhimu wanaweza kulifikia lengo lao.
Ikiwa wana CCM kama kweli wanamthamini Abied Amani Karume kwa mila na tamaduni zetu za Kizanzibari mtoto wake na familia yake siku zote zitakuwa zinatukuzwa, lakini kinyume chake ndio hiki leo kumtukana Amani ni sawa kumtukana Baba Karume, tabu nikuwa mhuni hajui alifanyalo ndio tabu yake.
Hawa ni watu hatari sana na lazima kutafutwe suluhisho la mara moja la kuwadhibiti. Mwanamume huwa hana matusi ila awe baradhuli, hakika waandishi hawa wa Kisonge wengi wao ni kaumi hiyo wakiongozwa na Borafya, kutokana na malezi mema ya Kiislamu niliyopewa siwezi kutukana kama wao, lakini ni aibu kwa Borafya huko nyuma alivyowahi kuwa na mambo aliyoyafanya na kwa kweli kile ni chombo kilichokuwa kinakwenda mperampera karibu kitagonga mwamba, subra ni muhimu, ingawa mwenye kasema kala nyama ya mbwa dua hazimpati.
CCM Kisonge wajuwe dunia haibaki kama wanvyofikiria mabadiliko hutokea bila ya mtu kuelewa, wapi Iran na Shah, wapi DDR na Honicker, wapi Yugoslavia na Tito, wapi Romania na Sacisko, wapi Somalia na Said Bare wapi zitakuwa ni nyingi na kutoweka kwake hakuna aliofikiria. Karibuni tumeona tawala kuporomoka kama Misri, Tunisia, Libya ambako hakuna mmoja alitarajia ipo siku yatakuwa hayo, tunajuwa waliofungika kiakili wanaamini CCM na Zanzibar ya kisonge kubakia milele, kwasababu hawajasoma na kutegemea fitna na ubaradhuli kuweza kuwafanya maisha yao yaweze kwenda. Wakati utawasuta watu na watake kujinyonga na kuiona dunia sio.
Amani hawezi kushtakiwa na madhalimu, kwani kumshtaki Amani ni kukishtaki chama cha CCM, Zanzibar na Bara. CCM imejaa dhulma, walimdhulumu Bilali wakampa Amani, sasa leo wanasema nini? Frankenstein amemtengeneza kiumbe kaanza kuleta mashaka, sasa huku hawa wapumbavu wameshindwa kuelewa leo wanatukana nini?
Kumtukana Bibi Fatma Karume nikujiuliza ni kweli huyu alikuwa mke wa muasisi wa Mapinduzi? Hapa ndipo ninapofahamu Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru, kuwa waliofanya Mapinduzi sio sisi wenyewe Wazanzibari, matokeo kile kizazi kichafu cha kina Injini na Mfaranyaki ndicho hadi leo kinaisumbua Zanzibar. Hakuna marefu yasio na mapana na hakuna Kiza kisichopambanukiwa. Mapinduzi sio daima lakini haki ndio daima.

PIMBI SHEIN-HAJUWI HATA MUUNGANO WA MKATABA HAHAHA HUYU KUMBI HUYU SIO DR NI KUMBI-VITISHO KWA RAIA WA ZANZIBARRAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amesema licha ya serikali kutokuwa na msimamo juu ya suala la mfumo gani wa serikali, lakini Chama Cha Mapinduzi msimamo wake ni kutetea serikali mbili kueleke moja kama zilivyo huku akiukataa mfumo wa muungano wa mkataba.
Dk Shein ameyasema hayo katika mkutano wa CCM uliofanyika jana katika viwanja vya Kibanda Maiti Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni sherehe za kumkabirisha baada ya kumaliza mchakato wa uchaguzi wa chama hicho uliofanyika huko uchawini Dodoma wiki hii.
Katika mkutano huo Dk Shein alizungumzia jumla ya mambo sita ikiwemo suala la kutetea Muungano ambao asema muungano wa serikali mbili hauna budi kudumishwa kwa kuwa ndio muungano sahihi.                                                     
Kwa hivyo muungano huu utadumu ni muungano imara na muungazo wa kidugu na ni muungano wa kihistoria na zipo nchi nyingi zenye muungano kama huu sitaki nizitaje,na kuna faida nyingi sana katika muungano huu katika mambo mbali mbali, mambo ya afya, kilimo katika huduma za bahari kuu tunashirikiana na tunafaidika sote, muungano huu una faida kubwa kwetu sisi tuna faida kubwa sana katika serikali hizi mbili, soko la bara ni kubwa tulikuwa tukiagiza vyakula kutoka nje lakini leo hii tunaagiza bara, wengi wetu wanaishi bara wamejenga majumba makubwa ya fakhari, alisema Dk Shein(KALEWA NA MADARAKA MPAKA HAJUWI ANACHOKISEMA MASIKINI PIMBI)
Dk Shein aliongeza kwamba Muungano huu ni bora kuliko muungano yote duniani kwanza huo wa Muungano wa mkataba sisi hatuujui.ukiwa na kitu ulichokizowea lazima wende na kitu ulichokizowea sisi tumezowea muungano wa serikali mbili…..alisema.(UTAUJUWAJE NA WEWE NI MSHAMBA WA MWISHO KIBUSHUTI ATI NI BORA KULIKO MIUNGANO YOTE DUNIANI HAHAHAHAAH UMEKWENDA UTURUKI NA UK BASI NDIO UNAONA USHATEMBEA KTK ULIMWENGU KUMBE NDIO KWANZA)WAZANZIBARI ANGALIENI KUMBI HILO TULILO EKEWA.
Aidha Dk Shein awali waliposhauriana na Rais Kikwete kuhusu suala la kufanyika kwa katiba mpya waliamua kwamba lengo ni kuendeleza na kuimarisha muungano na sio kuuvunja.
Licha ya kuwa na msimamo huo lakini alisema wananchi wapo huru kutoa maoni yao na hawalazimiki kufungika katika sera za vyama vyao na kila mmoja ajisikie yupo huru kutoa maoni yake huku akisiitiza kwamba CCM ina sera zake za serikali mbili na wengine wenye sera zao za vyama pia wanapaswa kutoa maoni yao.
Alisema Tume ya katiba imepewa mamlaka ya kupokea maoni wache watu wakatoe sio lazima sote tuwe na maoni ya aina moja wao wana yao na sisi tuna yetu sio lazima tuwafuate nyie,alisema Dk Shein na kushangiriwa.
Aidha Dk Shein aliwaambia wanachama wa chama hicho kwamba mchakato huu bado unaendelea hatua kwa hatua ingawa msimamo wa serikali bado hatujautoa kwa sababu tunawaachia wananchi wenyewe, hii ni hatua ya kwanza tu zahma za nini na fujo wakati mchakato huu bado, nilisema mchakato unakuja tume itateuliwa na wenye wajumbe wa pande mbili za muungano na nikasema katoeni maoni yenu na Kikwete hivyo hivyo tumesema hivyo kila pahala wananchi mkatoe maoni yenu vyama vina sera zake alihoji.
Akizungumzia suala la kuwepo kwa muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa Dk Shein alisema muundo huo utaendelea kuwepo na hakuna haja ya kuuvunja kwa kuwa lengo la ni kuleta umoja na mshikamano jambo ambalo ndio miongoni mwa malengo ya mapinduzi.
Serikali ya mapinduzi zanzibar ina muundo wa kitaifa nataka nikuhakikishie kwamba serikali hii tutaiendeleza kwa mustakabali wa wanzanzibari wakiwa wamoja na hili ndio lengo la mapinduzi yetu na hili la umoja, mapenzi na mshikamano alilianzisha Mzee Karume yeye alisaini mkataba watu kuishi kwa umoja na mshikamano kwa hivyo hili sio jambo jipya madhumuni ni kuleta maendeleo katika nchi yetu tukiwa pamoja na mashikamano, vyama vya siasa vinafanya siasa lakini sio kutukanana sio kugombana sio kushutumiana alisema Dk Shein.
Rais Shein alisema Serikali ya umoja wa kitaifa imetimiza miaka miwili na wamefanya kazi kubwa sana katika kipindi cha miaka miwili ingawa changamoto kadhaa alisema.
Alisema yeye ndio rais wa serikali na anaongozwa kwa misingi ya sheria na kanuni na hivyo anasaidiwa kazi na wasaidizi wake wawili ambao ni makamo wa kwanza na makamo wa pili na amekuwa akipokea ushauri ambao anaona unafaa na kwa ushauri ambao anaona haufai anaupuuza na halazimiki kupokea ushauri na hapaswi kuulizwa kwa nini anapuuuza kwa kuwa katiba imempa mamlaka hiyo.(USIULIZWE KWA M/MUNGU WEWE KIBUSHUTI..?)
Dk Shein akizungumzia suala la kulinda na kuyaenzi mapinduzi alisema hakuna mtu atakayethubutu kuyachezea na hivyo kila mmoja anapaswa kuyaheshimu na kuyathamini kwa kuwa ndio misingi ya uendeshaji wa nchi.(YA KUUWA WATU NA KUTHULUMU WATU SIO KISHA ATI ALLAH HUU AKBARI MSIKITI YAGUJUUU)
Suala la kuyalinda na kuyatukuza mapinduzi matukufu(ASTAHAFIRU ALLAH) hilo halina mjadala nitaendelea katika maisha yangu yote kuyatunza mapinduzi tutayalinda tutayatunza na kuyaendeleza ya kuwatumikia wazanzibari wote bila ya ubaguzi, kuondosha ubaguzi wa rangi na jinsia na kadhalika, kuleta maendeleo bila ya ubaguzi lengo lile lile lililotangazwa mwaka 1964 hili ni jambo la msingi hakuna wa kuyaondosha wala kuyabeza madhumuni ya mapinduzi tutahakikisha yale ambayo tumeahidi katika ilani yetu,alieleza.
Alisema suala la kuheshimiana katika vyama ni muhimu kwa kuwa lengo la kuendeleza umoja na kuwashughulikia wote ambao watatumia fursa ya kuharibu umoja huo na mshikamano na kusisitiza kuendeleza siasa za kistarabu bila ya kutukanana na kukashifiana.
Kila mmoja ana sera za chama chake tutashindana kwa sera bila ya kutukanana bila ya kupigana na wakati wa uchaguzi mkuu tutashindana kwa sera na CCM itashinda tuna sababu nyingi za kushinda sio kwa hila wala sio kwa jambo jengine lolote kwa sababu CCM ina mambo mengi na ina watu wengi,aliongeza.(WATU WENGI MACHOGO MULIOWALETE KUTOKA BARA KISHA MKAWAPA VITAMBULISHO VYA KIZANZIBARI SIO AU KUINGILIA WATU MAJUMBANI MUKIWAPIGA NA KUWAUWA NA VITISHO HAA LAZIMA MUSHINDE KIBUSHUTI SHEIN)
Aliwaambia wana CCM suala la kulinda na kutunza amani katika ni muhimu na kamwe hatuwachia watu wachache kuvuruga amani iliyopo kwa visingizio vya dini na kuhatarisha amani iliyopo nchini.
Suala la kutunza amani hatutawavumilia na mimi sitamvumilia yeyote yule ambaye atatuharibia amani yetu, nasema hatutamvulia mtu yeyote kwa anayetumia siasa au anayefanya siasa kwa kutumia mwamvuli wa dini Alisema.(SIASI NI KIPANDE KIDUGU TU KTK DINI MZUKA WEWE UMESOMA WAPI..?)AMA KWELI KUMBI NI KUMBI TU
MAENDELEO YA KIBUSHUTI SHEIN HAYOOO YANA INGIA NCHINI ZANZIBAR KAMA YA SALMIN AMOUR NGOMA WEE WAKIRUDI NYUMBA HATA CHA KUKILA HAMUNA MUNAISHI MIHOGO NA MASHELISHELI WAPUMBAVU WAKUMBWA
Aidha alisema msimamo wa serikali sio kuwazuwia watu kuendeleza dini zao lakini lazima wafuate sheria za nchi na kuacha kutumia dini kwa kufanya hujuma katika nyumba za ibada au kuwavunjia watu mali zao na kuharibu miondombinu.(JE WASHENZI WAKO SIO WALIOKWENDA KUPIGA MABOMU MISIKITINI..? JE WASHENZI WAKO SIO WANAINGIA MAJUMBANI WAKIPIGA WATU NA KUWAIBIA..?JE WASHENZI WAKO SHEIN SIO WALIO VUNJA MILANGO YA WATU NA KUIBA VESPA NA BASKILI ZA WATU UNASEMA NINI WEWE KIBUSHUTI)

Saturday, November 17, 2012

IF 9-11 DESERVES A MOMENT OF SILENCE....THEN PALESTINE DESERVES US TO NEVER SPEAK AGAIN

M/MUNGU AMLEZE PEMA PEPONI
M/MUNGU AWAPE MOYO WA SUBIRA KWA MTUHANI HUU WAZAZI WA MTOTO HUYU
M/MUNGU AWAPE MOYO WA SUBIRA WAZAZI WA WATOTO HAWA
WHERE IS U.N.....................?
WHAT IF WAS UR KID.....?
WHERE IS HUMAN RIGHT WHERE IS THE U.N........?

WHERE IS U.N...? WHERE IS HUMAN RIGHT..? EVERY BODY TURNING BLINDE EYES


BARUA YA WANA FAMILIA YA UAMSHO(SHEIN AVUNJA HAKI ZA BINADAMU,SHERIA NA KUENDESHA NCHI KIUBABE)


HATA MANDELA WALIMFUGA MWISHO NCHI ALICHUKUWA SHEIN NI KITUMWA CHA MAKABURU WEUSI TANGANYIKA NDIO MAANA ANAFANYA HAYA KUFURAHISHA MABWANA ZAKE WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA.

Waungwana naomba ingizeni haya malalamiko ya ndugu zetu masheikh wetu wa jumuia ya uamsho wanayo lalamika zidi ya uonevu wanaofanyiwa na serekali ya Smz chini ya mwevuli wa Muungano.
Barua ya wana Uamsho kwa Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar
WANAFAMILIYA ZA WATUHUMIWA
ZANZIBAR
11 NOVEMBA 2012.
KWA:
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA
ZANZIBAR,
MKURUGENZI
ZANZIBAR LEGAL SERVICES CENTRE
ZANZIBAR,
TANZANIA LEGAL AND HUMAN RIGHTS CENTRE
DAR ES SALAAM,
AMNESTY INTERNATIONAL
DAR ES SALAAM OFFICE,
DIPLOMATIC MISSIONS
DAR ES SALAAM.
YAH: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINAADAMU
Unaombwa uhusike na mada ya hapo juu.
Sisi ni wana familiya wa mashekhe na baadhi ya watu wengine ambao kwa sasa wanatuhumiwa kwa makosa ya uchochezi kupitia Kesi, 9/2012 iliopo Mahakamani Kuu na Kesi namba 380/2012 Mahakama ya Mwanakwerekwe.
Kwa vile suala lao kwa sasa lipo chini ya mahakama, wao bado ni watuhumiwa tu na wala sio wafungwa, kwa bahati mbaya kwa sasa wanachukuliwa kuwa zaidi ya wafungwa.
Watuhumiwa wote hao wanavunjiwa haki zao za msingi za kibinaadamu ambazo taifa lenyewe linadai kuziamini na kuzisimamia kama inavyoelezwa katika Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na kama ambavyo Tanzania ilivyoridhia mikataba mbali mbali ya ulimwengu.
Ikumbukwe pia Tanzania imesaini mikataba ya kuheshimu uhuru wa kuabudu na kutoa haki za wafungwa na wajibu wa kutekeleza mikataba hiyo hauwezi kuepukwa na Serikali ya Zanzibar kwa kuwa Tanzania imeridhia mikataba hiyo.
Kama mahabusu ambao hawajahukumiwa na mahakama pekee ndio yenye haki ya kuthibitisha kuwa washtakiwa ni wakosa au laa. Miongoni mwa haki zao wanazonyiwa ni pamoja na:
1. kuzuiliwa kubadili nguo kwa muda wa zaidi ya wiki tatu na wala hawaruhusiwi kuletewa kutoka nyumbani
2. kuzuiliwa kupatiwa chakula kutoka nyumbani ambapo wengine miongoni mwao ni wagonjwa wa vidonda vya tumbo na hawataweza kula kinachoenda kinyume na miiko ya kitabibu.
3. kuzuiliwa kuonana na familia zao
4. kuzuiliwa kuwaona kwa uhuru mawakili wao
5. kuzuiliwa kwa wanafamilia kusikiliza kesi zao
6. masharti magumu na yasiotekelezeka kama vile kuwataka washtakiwa wapate dhamana ya watu ambao wanafanya kazi Serikalini
7. mahabusu hao kutengwa kila mtu chumba chake (solitary confinement) jambo ambalo ni kinyume na vigezo vya kuweka mahabusu au wafungwa.
Na kama hayo hayatoshi wamezuiliwa hata haki zao za kuabudu kwa kuzuiliwa kupatiwa nakala za Qur-ani ili waweze kusoma na kujumuika pamoja na wenzao katika sala ya pamoja wakati mahabusu wengine wakiruhusiwa kwa hayo. Huu ni udhalilishaji unaopita mipaka ya kibinaadamu na ni kinyume na sheria za nchi yetu inayodai kuwa ni ya kidemokrasia na ni kinyume cha sheria za kimataifa kwazo Tanzania imezikubali.
Tunahitimisha barua yetu hii kwa kutoa wito maalum kwenu kulisimamia suala hili la uvunjwaji wa haki za kibinaadamu ili kuhakikisha haki inapatikana kwa watuhumiwa na familia zao bila ya kudhulumiwa mtu yeyote. Tukumbuke kuwa hakuna mtu ama kiongozi yeyote aliye juu ya sheria bali kila mmoja anawajibika kufuata sheria ipasavyo.
WANAFAMILIYA WA WATUHUMIWA
……………………
FAMILIYA YA SH. FARID HAD
……………………
FAMILIYA YA SH. MSELLEM ALI
……………………
FAMILIYA YA SH. AZZAN KHALID
……………………
FAMILIYA YA SH. MUSSA JUMA
……………………
FAMILIYA YA SH. SULEIMAN JUMA
……………………
FAMILIYA YA SH. KHAMIS ALI
……………………
FAMILIYA YA SH. HASSAN BAKAAR
……………………
FAMILIYA YA SH. GHALIB AHMAD
NAKLA:
MWANASHERIA MKUU, ZANZIBAR
KAMISHNA CHUO CHA MAFUNZO, ZANZIBAR
WAANDISHI WA HABARI TANZANIA
WAISLAMU WOTE TANZANIA
MKURUGENZI WA MASHTAKA DPP, ZANZIBAR

WAZANZIBARI WASEMA NCHI YAO KWANZA KIBUSHUTI SHEIN ASEMA CHAMA KWANZA NDIO KILICHO MUWEKA MADARAKANIMakamo Mwenyekiti wa Chama CHa Mapibnduzi Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein amesema sasa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaondoka na gia mpya katika kuimarisha na kuendeleza Chama katika ngazi zote ili kuona kinaleta mafanikio na kupata ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Amesema baada ya kumalizika uchaguzi wa ngazi za juu na kupata viongozi wapya kazi iliobaki ni kuimarisha chama kuanzia shina hadi taifa.
Amesema vikao vya chama ndivyo vinavyoimarisha na kuhuwisha chama kwani katika vikao hivyo ndimo mnamojadiliwa na kupangwa mambo yote ya kuendeleza chama.(SIO NCHI)
Dk Shein alitoa kauli hiyo leo jioni huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui alipokuwa akizungumza na wazee wa chama hicho mara baada ya kuwasili Zanzibar kutoka Dodoma kuhudhuria Mkutano Mkuu wa chama ambako alichaguliwa kuwa makamo wa Mwenyekiti wa CCM upande wa Zanzibar.
Amesema chama kitaendelea kuwaenzi wazee na kutumia busara zao katika kujenga uimara wa chama hicho na pia kupata hekima katika kukiendeleza na kukiimarisha ili kiendelee kuwa chama chenye misingi imara na kisichoyumba katika utekelezaji wa majukumu yake.(MAJUKUMU YA FITNA NA KUWABAGUWA NA KUWAGAWA WAZANZIBARI TUNARUDI KUULE TULIKO TOKA)
Hivyo aliwashukuru kwa jitihada zao za kukilinda na kukienzi chama hicho na pia kumchagua yeye kukiongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Ameahidi kufanya kazi bega kwa bega na wazee hao katika kukiendeleza chama cha mapinduzi.
Akizungumzia suala la utoaji maoni juu ya katiba mpya , Dk Ali Mohammed Shein amefahamisha kuwa nia ya kuwepo kura ya maoni ni kuimarisha muungano na sio kuvunja, hiyo ndio sera ya chama cha mapinduzi.(TUPENA BASI HIYO KURA YA MAONI)
Ameongeza kuwa katika mapendekezo hayo hapana pahali palipoandikwa au kusema kwamba Muungano uvunjwe. CCM ina sera yake ya kuimarisha muundo wa serikali mbili na sio vyenginevyo. Sera ya ccm iko wazi maelezo yake yapo wazi alisisitiza Dk Shein.(SEREKALI MBILI KUELEKE MOJA AU SIO KIBUSHUTI SHEIN..?)
Amesema watu wamekuwa wakitia chumvi juu ya suala hili hivyo si vyema kuwafuata kwani sisi tunasera yetu (CCM) na wao wanasera zao, sisi tuna chama chetu na wao wana vyao.(SERA YAO NI KUTAKA NCHI YAO CHAMA CHAO NI ZANZIBAR KWANZA WEWE SHEIN BADO NI KIBARAKA WA WATANGANYIKA UNAE TAKA SISI KUENDELEA KUWA WATUMWA NA KOLONI LA WATANGANYIKA.)
Alifahamsha kwamba chama ndio kiwe mbele na hakuna wa kuwababaisha wana ccm, kwani chama ndio kilichodhibiti nchi ibakie katika mikono ya wazalendo wa Tanzania si vyenginevyo.(NCHI NDIO IWE MBELE WEWE KIBUSHUTI)
Alitahadharisha kwamba wapo watu bado wanaitaka Zanzibar na kama wana ccm hatukuwa makini na tukafanya mchezo watu wataichukuwa nchi.(FITNA HIZOO SHEIN KIBUSHUTI ANAZILETA ILI AWAGAWE WAZANZIBARI)
Kuhusu amani na utulivu wanchi, Makamo mwenyekiti huyo alisema bado wako watu wanaichezea amani iliopo jambo ambalo ni hatari sana.Serikali haitavumilia kuona amani inachezewa.(ILI YAKUWAINGELIA WATU MAJUMBANI NA MISIKITINI MUKINAJISI KWA MAMBWA NA MABOMU NDIO AMANI SIO..?)
Alivipongeza vikosi vya ulinzi na usalama kwa kurejesha utulivu na kuendelea kulinda maisha namaliza raia.(YA LAZIMA UWAPONGEZA WANA DHULMA KAMA WEWE MWENYEWE ULIVYO THULUMU KURA UKAJIWEKA KTK URAISI HUKUSHINDA ILA DHULMA DHULMA NDIO LAZIMA UWAPONGEZE)
Amerejea kauli yake kwamba serikali haiwezi kuvumilia tena vitendo vinavyofanywa na Muwamsho na kusema kwamba serikali itaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa kikundi chochote ambacho kitaashiria uvunjifu wa amani hapa nchini.na kamwe serikali haitovumilia kuchezewa.Haturudi nyuma katika kulinda amani ya zanzibar ili sifa nzuri ya visiwa hivi isiondolewe.(IMEONDOKA ZAMNI SANA NA WEWE NDIO UNACHAFUWA ZAIDI KIBUSHUTI WEWE)
Nao wazee wa CCM wa Mikoa mitatu ya Unguja walitoa pongezi zao kwa Mkutano Mkuu wa Taifa na Ushindi wa asilimia mia moja (100%)kwa Dk shein na kusema kwamba hivi sasa chama kimeingia katika muelekeo wa uhakika zaidi wa kukipatia ushindi wa kishindo chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao. Kwani kutokana na sababu za kiitikadi kilichojitokeza ni kuzorota kwa utendaji katika chama hasa ngazi za chini katika kipindi kilichopita cha uongozi.
Wamesema sikweli maneno yaliosemwa na kiongozi mmoja wa kisiasa kamba doria zinazofanywa na askari kwa lengo la kudumisha amani vinafanya doria katika maeneo yenye wafuasi wa chama hicho na eti kwamba kinawabughudhi.(UKWELI NIUPI BASI SIMUSEME..?)
Waliwataka viongozi wa juu kukumbushana umuhimu wa kujikinga na fitna na kuziepuka taarifa za kubuniwa.