Wednesday, November 28, 2012

HOSPITALI YA MNAZI MOJA IMEKUWA MTOTO WA GETI KALI KUINGIA MIA 500 HATA KAMA UNALETA MNGONJWA DUUUUUUUUH!!!!



Moja kati ya agenda kuu ya Kitumwa cha watanganyika, Dr. Kumbi Ali Mohammed Shein, ni kuikuza na kuindeleza hospital kuu ya Mnazi Mmoja — iwe ya ‘Rufaa na kimataifa’.
Bahati nzuri Dr Kumbi.Shein naweza kusema ni ‘kindaki ndaki’ wa hospital hiyo anaijua A-Z, kuanzia mazoezi, na hata kazi amefanyia hapo; mpaka ameondoka na kuingia katika siasa ametokea hapo; pia kama Kibaraka cha watanganyika, ofisi yake akichungulia anaona wodi ya watoto, laboratory aliyokuwa anaifanyia kazi n.k.
Kwa kweli yeye na Mnazi mmoja ni kama mtu na ‘mwanawe’.
Pamoja na hayo, hospital ya Mnazi Mmoja inakabaliwa na matatizo mengi, likiwemo kubwa sana na UBINAFSI.
Mfano mzuri, mpaka sasa sioni sababu kwa NINI kuingia hapo hosp, lazima ulipie sh.500/= kama ukiingia na gari hata kama gari hiyo ina mgonjwa ndani yake; kuna mnyororo pale lazima ulipe utake usitake.
Huu sio ubinadamau hata kidogo, na tunakuambia Juma Duni Haji, na bosi wako, Dr Kumbi.Shein muchukue uamuzi wa kuondosha mnyororo huu (kama kweli ni viongozi wenye mamlaka) au kama ni masheha tu, na ubabe wao ni kwa UAMSHO, tujue.
Kinachofanyika pale ni dhulma. je, pesa zile zinazokusanywa shl 500 pale, zinaingia katika mfuko gani?
Isitoshe, mara moja walisababisha msongomano pale, na msafara wake dr Kumbi.Shein unakuja speed kubwa kuingia Ikulu, hapo ilikuwa tafran kubwa. Eneo lile kiusalama si eneno linalohitajika msongamano.
Mgonjwa huyo, alipie kulipia kuingia humo hosp mumesikia wapi hata nchi zilizo endelea na hospitali zao nzuri kama hoteli basi kuingia hulipi itakuwa hapa uko viwaja vya maisara harufu ishakuva kisha ukingia ulipe thulma mpaka hospitali basi kwa gari, alipie cheti, alipie X-Ray, alipie kumuona daktari, alipie choo, akitaka kujisaidia — jamani kweli haki hiyo?
Wakati fulani, niliwahi kumueleza waziri wa Afya aliyepita, Sultan Mugheir, kadhia hii — kuna kipindi alinifahamu, na aliondosha huu mnyororo wa hosp. Sasa umerudi tena.
Maalim Juma Duni (Babu Juma), Dr Kumbi Shein, Maalim Seif, na Balozi Seif Ali Iddi wa tanganyika, msiwakamue wananchi sana kiasi hicho, give them a space please, basi hata kuingia hospital na mgonjwa watu walipie, au kuja kuangalia mgonjwa. Jamani hebu kuweni binadamu japokuwa kidogo.
Mambo muhimu kama usafi wa vyoo, huduma za chakula, huduma za matibabu n.k hizi zote hakuna hapo, ila kuchukua pesa kwa kila ‘inayoitwa huduma’ lazima ulipie hata kama hutoipata.
Utalipia X-Ray, lakini unaweza kuwa hutoipata huduma hiyo, hizo zinazoitwa city scan kadhalika.Mpaka chakula sasa hakuna pale hospital, na ukitaka ulipie. Shabash!!!!!!!
Unajua wananchi wengi wa Zanzibar walaitegemea sana GNU inaondosha uonevu kama huu, usiokuwa na maana, YES, hawakutegemea utajiri bali angalau maudhi madogo madogo yaondoke, lakini yamezidi.
Ahhhh…..sifikiri kama uongozi wa juu utanisikiliza, maana hawana utamaduni huo, wa kusikiliza wananchi wa chini, wao ni ubabe tu — SMZ-GNU kwa kweli imeoza sana, haina tija kubwa sana kwa wananchi walio wengi (ubabe dhidi ya Uislamu, na waislamu, wanafunzi wanafelishwa kwa visingizo tofauti, wafanyakazi wanachakachuliwa mishahara yao na officials wa wizara, kuna waliokufa na meli, fidia zao mpaka leo mtihani — haya yote na mengine  mtumwa wa watanganyika Shein, huyaoni, wewe msimamo wako na serikali yako ya udikteta kupitia DPP office, UAMSHO wasote rumande mpaka wafe humo humo).kiyama utasema nini kwa m/mungu wewe kibaraka wa watanganyika..?
Mimi naomba mwanasheria yeyote wa ndani na nje ya nchi, anieleze je, kuna kesi ya kujibu kwa akina Farid na wenzake..? Na mengine mengi —- na hili la hospital linatukera tena linatukera sana.
Dr Kumbi Shein ulisema kuwa wanaokwenda kujifungua kwa ‘mkasi’ wasilipie, hii mpaka leo wanalipa tena nyongeza inadaiwa pia ya kulipa zaidi.
Na ukijifanya unahoji, unaambiwa ‘kwamitwe huyo dr.shein’ aje akutibu yuko nyuma ya ukuta hapo, akupasue….au utaoza hapo hapo! hayo ndio majibu unayopewa wodi ya wazazi ……! Kweli haya hayajui huyu  Dr Kumbi Shein…….ina maana anapelekewa habari potofu za UAMSHO tu. Dr Kumbi Shein,habu isome hii au wasaidizi wako waisome hii – kuwa bado wazazi wanaokwneda kujifungua kwa mkasi ‘wanalipishwa pesa nyingi tu’. Ulisema katika baraza la Eid el Hadji ‘enough is enough’ — tunataka tuone na hili ubabe wako wa ‘enough is enough’ unalifanyia kazi.

No comments:

Post a Comment