Sunday, November 18, 2012

KUMBI SHEIN UWONGOZI UNA MWISHO WAKE WEWE KICHWA CHA SAMAKI


HUYU NI KUMBI SHEIN ALIPORUDI KUTOKA DODOMA
Binaadam yeyote ambae ana akili timamu mara zote huwa ni kiumbe chenye kufikiri sana hatma yake,lakini la msingi kabisa ni fikra inayo muunganisha baina yake na Mola wake na kujua nini hasa lengo la kuumbwa kwako kama Binaadam kamili .
Licha ya Mola wetu kutupa hidaya hii muhimu,hakutosheka na hilo bali pia katupa utukufu na daraja kubwa sana pale alipotupa hidaya nyengine baada ya kwisha kutuumba yaani akili kwa Mwanaadamu,lengo ni kufikiri na kuelewa majukumu yetu kama binaadamu na tupo hapa Ulimwenguni kwa misingi gani.
Mola wetu ametuekea bayana kwa Mafundisho sahihi kwa kumleta Mtume wake na Kitabu chake kitukufu ili tupambanue mustakabali wetu kati ya mabaya na mema. Vile vile hakuishia hapo kwa kutuweka njia panda lahasha ! bali tumebashiriwa pepo kwa watenda wema na pia moto kwa watenda maovu.
Kutokana na mantiki hiyo ni kuonesha kwamba kila lenye mwanzo basi halikosi kuwa na mwisho. Hata hii dunia tunayoringia basi nayo pia ina mwisho wake,hatuna budi kwa Waumini kukumbushana katika hili.
Ikiwa hivyo ndivyo basi ni vyema kwa Kumbi Shein na Kaumu yako mukaelewa kwamba uongozi ni dhamana na Urais una mwisho wake.Yeye kama kiongozi aliejitwisha joho hilo ana dhamana kubwa amebeba na masuala makubwa ya kwenda kujibu kesho yaumu -likyama yanamngojea hili halina mush-keli kwa wenye kuamini.
Mabeni ya wafuasi wako lakini pia na Washauri wako wa karibu Kumbi Shein haitokuwa kinga ya siku hiyo itakayo kufanya uwachwe hivi hivi tu usiulizwe masuala kutokana na jinsi gani ulivyo upata ufalme wako na jinsi gani ulivyowatumikia Wazanzibar. Siku hiyo hapatakuwa na Kizota wala Dodoma bali ni wewe kutoa majibu sahihi mbele ya haki ili kila Mzanzibar apate haki yake.
Kumbi Shein inaonesha dhahiri kwamba Ufalme unakutia kibri na jeuri na kuona kana kwamba utadumu kwenye Ufalme huo milele,hilo haliwezekani.Chini ya uongozi wako Wazanzibar wanazidi kudhulumiwa na wewe hilo unalifurahia na kulishadidia kwa vile wewe uko Madarakani. Kuna watu wanakushauri vibaya ili uzidi kuwanyima haki Wazanzibar unaowatawala huku wao wanafaidika na hilo.
Kumbi Shein uifikirie pia nafsi yako na hatma yako kesho mbele Muumba umeshajindaa na majibu mazuri ? Lengu langu ni kukumbusha tu kwani wakati mwengine sisi ni Binaadamu tunajisahau na kuona huo ulwa umeupata kwa akili zako na usomi wako wa kichwa cha samaki usiye juwa hata muungano wa mkataba. Wako viumbe wengine hawakuwa Madokta lakini waliongoza kwa Ik-lass hilo ulijue.
Kumbi Shein Wazanzibar wanadai haki zao za msingi kama alivyo amrisha Mola wetu,lakini kutokana na wewe na Kaumu yako kuona matamanio ya kidunia ni bora zaidi, haki hizi unazifumbia macho,matokeo yake unakuja na kibri na kejeli kwa Wahusika,huoni kwamba mwisho wa yote hayo Urais una mwisho wake ? Unajua dhahiri kwamba Wazanzibar wanadhulumiwa lakini wewe na Wapambe wako maslahi yenu yanawaendea,kumbuka hayo yana mwisho.
Nakupa mfano mdogo tu Kumbi Shein tokea Mapinduzi ya 1964 ni Marais wangapi wameshapita kukalia kiti hicho ulicho nacho na hii leo wako wapi ? Kumbi Shein jawabu wewe utakuwa unalo,lakini kumbuka leo hii hawatajwi tena katika ulwa huo,kilichobakia ni majuto na huzuni tu, kumbuka na wewe utakuwa miongoni mwao. Mali na majumba utayawacha hapa hapa,ila haki za msingi za wale mulio wadhulumu hizi hazitokufa abadan.mfano mwengine mzee karuma kalala pale kisiwa nduwi na majumba yake kayawacha hapa hapa basi na wewe ndio hivyo hivyo utaviwacha hapa hapa.
Kumbi Shein muda unao  uyafikirie hayo,kuwalaani baadhi ya Wazanzibar na kuwaseka ndani sio suluhisho la Wazanzibar kutokudai haki zao za msingi bali unazidi kuwasha moto kwa kizazi kipya kilichopo na kinachokuja hapo baadae. Kumbi Shein kumbuka kwamba chuki hizo munazozipanda mizizi yake haitaishia hapo tu bali matunda yake yatachanua.
Kifungo kile ulichowatia wale unaowaita wavunjaji wa Amani elewa si chochote bali ogopa kifungo cha Mola wetu hakuna anaekiweza. Iko siku madhila ya Watu wale utakuja kuyaona pekee yako bila Washauri wako au Chama chako.

No comments:

Post a Comment