Tuesday, November 20, 2012

MUUNAUTAKA AU HAMUTAKI-JIBU HATUTAKI HIVYO NDIVYO ALIVYO ULIZA SHEIKH FARID ALIPOKUWA AKITOKA MAHAKAMA YA VUGA LEO NA KURUNDISHWA RUMANDE NA MAMIRI WENZAKE



Viongozi wa jumuiya ya uamsho wanaodaiwa kusababisha vitendo vya uvunjifu wa amani Visiwani zanzibar wamefikishwa kwa mara nyengine katika mahakama kuu ya vuga kwa ajili ya kutolewa ufafanuzi juu ya malalamiko yaliyotolewa na mawakili wao dhidi ya vitendo wanavyofanyiwa wateja wao wanapokuwepo gerezani. Ikiwa ni pamoja na kukosa uhuru kitu ambacho ni kinyume na haki za binaadamu.
Viongozi hao walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tatu kamili barabara asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa gari nne za askari wa kutuliza ghasia {ffu}, huku wakiwa wamevalia kikazi zaidi.
Mapema baada ya viongozi hao kushushwa katika gari lilokuwa limewabeba alisikika Sheikh Mussa Juma, ambaye ni mmoja wa washtakiwa hao, akiwaambia waandishi wa habari “Nyinyi waandishi wa habari njooni gerezani kuchukua habari jinsi tunavyonyanyaswa sio mnachukua hapa tu”
Kabla ya kuingizwa washtikiwa hao katika chumba cha kesi askari polisi walianza kuwatawanya wananchi waliofika mahakamani hapo pamoja na waandishi kwa njia za amani ili kuweza kuondoa usumbufu katika chumba hicho. Lakini wakati huo huo wakamchukuwa kijana mmoja ambae alikua akipiga picha matukio hayo kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Nae mwendesha mashtaka wa kesi hiyo george kazi ametoa ufafanuzi juu ya malamiko ya washtakiwa hao na kusema mahakama haina haki ya kuvilazimisha vyombo vya ulinzi kutenda haki kwa washtakiwa hao, hivyo amewaomba mawakili wa viongozi hao kufungua kesi katika mahakama kuu ya vuga kwa lengo la kudai haki hizo.
Aidha amesema bado upelelezi wa kesi yao bado unaendelea hivyo ameamuru washtakiwa hao kurejeshwa tena rumande hadi tarehe 29 mwezi huu.
Wakati washtakiwa hao walipokua wakiingizwa katika gari kwa ajili ya kurudishwa rumande sheikh mussa alirudia tena maneno yake aliyoyasema mwanzo huku akiungwa mkono na sheikh farid kwa kusema zanzibar itapatikana, na baaadae kuwauliza wananchi “mnautaka muungano” na wao kujibu huku wakipiga takbiri katika mlango wa mahakama “hatuutaki”
Wakati huo huo wakili wa washtakiwa hao bwana Salum Tawfiq ameziomba familia za washtakiwa hao kuendelea kupeleka baadhi ya huduma kama vile chakula ingawa hawaruhusiwi

No comments:

Post a Comment