Thursday, November 29, 2012

NCHINI ZANZIBAR KUBAKA SIO KOSA SIKU HIZI KUIDA ZANZIBAR NDIO KOSA-ASKARI WATATU WAMBAKA MTOTO NA KUACHIWA HURU PEMBA.MAHAKAMA YA WILAYA YA CHAKE CHAKE IMEWAPANDISHA MAHAKAMANI ASKARI WATATU KUTOKA KIKOSI CHA VALANTIA CHA KVZ KWA TUHUMA ZA UBAKAJI.
MWENDESHA MASHTAKA KATIKA MAHAKAMA HIYO MKAGUZI MSAIDIZI WA POLISI GONGO SHAABAN GONGO AMEWATAJA ASKARI HAO NI ADIBU AMABE AMEFAHAMIKA KWA JINA MOJA TU LAKINI HAKUWEPO MAHAKAMANI HAPO WENGINE NI ABDU KHAMIS NA HAFIDH YUSSUF MASOUD.
AIDHA MWENDESHA MASHTAKA HUYO AMEELEZEA MAHAKAMA CHINI YA HAKIMU MCHA HAMZA KWAMBA VIJANA HAO KWA PAMOJA WALIFANYA TUKIO HILO LA KUM’BAKA MTOTO WA MIAKA 18 SIKU YA JUMATATU YA 29-10-2012 SAA MBILI USIKU WALIPO KUWA KAZINI KATIKA ENEO LA ZSSF CHAKE CHAKE PEMBA.
WASHTAKIWA HAO HAWAKUTAKIWA KUJIBU LOLOTE KWAKUWA KUTOKANA NA MAHAKAMA HIYO KUTOKUWA NA UWEZO WA KISHERIA WA KUSIKILIZA KESI  KAMA HIZO.AIDHA AMEFAFANUA KUWA VIJANA HAO WALIFANYA KOSA HILO KINYUME NA SHERIA KWA MUJIBU WA KIFUNGU NAMBA 127{1} SHERIA NAMBA 6 MWAKA 2004  NCHINI ZANZIBAR KWA KUBAKA.
KESI HIYO IMEGHAIRISHWA HADI ITAKAPOTAJWA TENA 2-12-2012 AMBAPO YALITOLEWA MASHARTI YA DHAMANA KWA KILA MMOJA KUWA NA KIASI CHA SHILINGI LAKI TANO ZA MAANDISHI NA WADHAMINI WAWILI AMBAO KILA MMOJA AWE NA KIASI KAMA HICHO IKIWA MMOJA NI MFANYAKAZI WA SERIAKALI.JE SI VIHOJA HIVI ASKARI WATATU WANAMBAKA MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 18 NA KUPEWA THAMANA KAMA WANAKULA BATATA ZA UROJO VILE HUKU UAMSHO WANAITETEA NCHI HII ISIMEZWE NA WATANGANYIKA WANASOTA RUMANDE MPAKA LEO HAWAJEWA THAMANA WALA MAINI YA THAMANA IKO WAPI HAKI.....?WABAKAJI TENA ASKARI WAKO HURU WATETEA HAKI WANAISHIA JELA.

No comments:

Post a Comment