Wednesday, November 28, 2012

SMZ YA ZAMANI.......NA SMZ YA SASA IPI ...YENYE KULETA MAINDELEO SMZ YA SASA KAZI KUNADI MAENDELE MAENDELEO KILA LEO WALA HATUYAONI.


IBEENI NYIEE WEEE LAKINI MUJUWA MUTAVIWACHA HAPA HAPA NA MUTAINGIA HUMO KABURI KAMA MZEE KARUME ALIVYO INGIA KISHA HAPO NDIO UTAJUWA UTAMU WA UWONGOZI WAHAFIDHINA WAKUBWA NYIE NA MATHALIM WAKUBWA


Siku moja aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya watanganyika, ambae pia huitwa baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa akitembelea kisiwa cha Pemba, kikazi. Katika safari yake hiyo ya mzunguko wa kikazi ilisadifu kupitia barabara ya mkoani kwendea Chake chake. Karibu na kichunjuu, hivi kuna krosi moja kubwa sana iliyokuwa na muundo wa herufi ‘S’.
Wakati wakipita pale na msafara wa magari na jinsi njia ilivyokuwa mbovu, na makarama ya krosi ile ilivyochongeka, Nyerere hakuamini kama anapelekwa Chake chake. Akauliza;‘Tunakwenda, tunarudi?’ Akaambiwa tunakwenda, il’hali gari ikiwa limeelekeza uso kule linakotoka na likiendelea na mwendo ule ule katika msafara. Nyerere akasubiri ajionee kioja, akatulia.
Miaka zaidi ya 30 tangu Nyerere aulize suali hili, na sasa ni karibu miaka 13 tangu Nyerere afariki, hakuna mmoja wetu aliepata kufikiria falsafa ya maneno haya, yaliyochukuliwa kama mzaha wa Nyerere tu wakati hule na hadi sasa. Kusema ukweli maneno haya hayakustahili kutiwa kapuni na kama kuna aliyefanya hivyo amekosea. Ndio maana mimi nilie yaweka hakiba leo nayavongonyowa na kuwatunukia. As’aa huenda mukazinduka.
Zanzibar, nchi kinyonga, mara nchi, mara si nchi, vyovyote tukavyoiita, itaitika. Hadi sasa Visiwa hivi vinapata umri wa miaka isiyopungua 48 tangu kuachwa na mkoloni mweupe na kuvamiwa na mkoloni mweusi. Miaka hii si kidogo hasa kwa kuyatathmini maenddeleo yetu na ya nchi kwa ujumla. Naamini huu ni wakati muafaka wa kujiuliza, ikiwa SMZ ndie mtawala mkuu wa visiwa hivi tangu miaka hio, na anaehubiri maendeleo kila uchao, tuiulize Serikali yetu ya SMZ suali lile lile, ‘TUNAKWENDA, TUNARUDI?’
Nchi hii ilikuwa ina maendeleo makubwa na ilikuwa na hakiba isiyomithilika katika mahakibizo ya fedha duniani mpaka zama za miaka ya mwisho ya 70. Serikali zetu za SMZ zilizopita zilikuwa zimetawaliwa kimabavu kweli kweli lakini mengi tuliyaona sasa hatuyoni tena. Ndani ya miaka minane ya Abeid Karume, tulipata majumba makubwa nchi nzima. Tukajengewa hosipitali na vituo vya afya.
Ndani ya miaka ya Karume, Jumbe hadi karibu ya Ali Hassan Mwinyi, wazee wakipewa pesa za matumizi zikiitwa ‘ulufea’ (Welfare benefits) na zikiwasaidia sana. Wakati wa tawala za SMZ za siku hizo sio sasa mukumbuke, hosipitali zilikuwa zimejaa madawa, usafi na huduma za kila aina. Skuli zetu zilijengwa hatua kwa hatua, hakuna alielipia mchango wa skuli, hakuna alienunua daftari, kalamu wala penseli. Hakuna mwanafunzi aliekosa huduma za afya za kichocho, vipimo kila muda Fulani.
Ilifika wakati kwa jinsi Serikali ilivyo kuwa ikiwajali wanafunzi, Waziri wetu wa Elimu wa mwanzo hapa Zanzibar, aliwahi kupendekeza kuwa vichwa vya Ng’ombe vyote vinavyochinjwa nchi nzima vipelekwe mashuleni wanafunzi wapikiwe supu, ili wapate wanywe wakati wa mapumziko (recess) nikichikesho ikisikia sasa. Bahati mbaya mpango huu ulivunjwa na Sheikh Karume, pale alipomwambia Waziri wa Elimu kuwa asijefanya hivyo mpaka ahakikishe kila mwanafunzi ameshapata kijiko na kibakuli cha kunywea supu. Mapango huu ukafa hapo, lakini ulikuwa na nia njema.
Enzi za SMZ ya wakati huo sio ya sasa vurugu mechi na wizi, kulikuwa na huduma za dakhalia (boarding). Ukipasi ukipelekwa huko kupatiwa mafunzo ya kuwa mtu utakaejitegemea. Tukipewa kula asubuhi mchana na jioni. Japo tukiita bondo, lakini tukipewa tena bure na kwa wakati bila kuchangishwa gharama. Wanafunzi wakiletewa meli bure kupanda au wakifanyiwa tiketi kabisa wakifika huchukuwa na kusafiri tu kwenda Unguja na Pemba. Tuache huko.
Hospitali, kula kunywa na huduma masaa ishirini na nne. leo kula ishaondolewa hospitali ya mnazi moja maendeleo hayo. Mgonjwa akipembejewa na madaktari wa kikwetu na wa kigeni wakati huo leo matusi mpaka utarudi kwenu na maradhi yako. Serikali haikuwa na meli zilizoenda kwa kasi wala madege, lakini watu wakisafiria meli za Serikali za uhakika na unafuu wa bei. Huo ndio wakati ambao tunaweza kuusema kuwa nchi yetu ilikuwa changa, na ilikuwa na matongo ya ukoloni mweupe kabla ya kutiwa matungoo ya mkoloni mweusi tanganyika, haikuwa na uoni wa mbali wala uwezo wa kutuletea maendeleo.
Tupige dira ya SMZ leo. Serikali yahubiri na kutangaza kila siku kuwa nchi hii imepiga hatua kubwa kimaendeleo ukilinganisha na Zamani hahahah nacheka kwenza ahahahahaha. Sikatai. Maendeleo wakati mwengine hupimwa kwa miwani ya macho, ambayo kigari kidogo huwa TATA, au FUSO. Maendeleo siku hizi hupimwa kwa kutazama ndege zipitazo juu ya anga letu, tivii pana majumbani, au kila mtu ana simu ya kiganjani. Maendeleo yetu hupimwa kwa viongozi kuwa katika magari makubwa ambayo wakiwa ndani ya magari hayo hawasikii ule uvundo unaonuka pale Darajani kituo cha dala dala wala hawawasiki wanachi walio waomba kura kabla hawajapata hayo magari makubwa.
Maendeleo hupimwa wakiwa katika magari ambayo pia yakipita njia mbovu hawahisi wala hawapati vumbi mle ndani. Na pia licha ya kuwa nchi ina joto la tanuri ya mbata siku hizi kwa uchafuzi wa mazingira, viongozi wetu wa SMZ hawalihisi joto hili na vuke kali, katika magari na majumba yao yaliyo ‘full kipupwe, full kiyoyozi, full kujiachia’. ahahahaha nacheka kwanza maana nikilia nitaumiya moyo bora nicheke. Raha zote hizi zilizowazunguka viongozi wetu unawategemea kuwa siku moja watasema kuwa nchi hii inarudi nyuma badala ya kwenda mbele..? Ungekuwa wewe ungetia ulimi wako puani ukasema ukweli huu wakati yote hayo huyaoni kwa maraha yaliyokuzunguka...?
Hebu linganisha hayo machache niliyoyasema yalifanywa, enzi za Karume, Jumbe na kidogo Mwinyi na uone. Sasa tudurusu kwa pamoja. Nitawauliza maswali munijibu mpaka nimalize, sawa...? Bismillah! Ule ‘ulefea’ bado upo..?, Skuli zetu zina vifaa...? madafatri na kalamu bure..? Dkahalia zipo...? Elimu bado ni bure..? Ndio ni bure maana haina maana yoyote, lakini inalipiwa. Samahani hili nimejijibu mwenyewe. Haya tuendelee.
Kule spitali dawa ziko...? Ndio lakini kwa pesa duuh nimejibu mwenyewe tena. Kile chakula vipi bado wanapatiwa wagonjwa...? Ahh! Bajeti ya Wizara ya afya ndogo..?, kimefutwa Chakula. Lakini Waziri wa Afya ana prado la milioni 70, na mafuta yake ya laki moja kwa wiki pengine. Hawasemi kuwa mawaziri waendeshe gari ndogo kama Starlet, na Vizt kujenga taifa. Heri wafe wagonjwa wao waendeshe magari mazuri. Ndio sisi bwana, wakoloni weusi. Nani anajali kama wagonjwa wanakufa kwa kutukanwa tu kule Spitali, kwa kukosa dawa tu na hata kula sasa..? Hawa ndio viongozi wetu bwana, ni zaidi ya majoka ya mdimu.
Madakatri jee wanashuhulikia wagonjwa...? Hapana, wanawatukana wala hakuna anejali serikalini kwani wao hawatibiwi hapa hata wakiumwa na tambazi (uvimbe) huenda nje ya nchi. Kwanini..? Tumeendelea hivyo. Tuendelee, au mshachoka...? Mmeona wapi Serikali kujenga tena majumba ya watu na makazi...? Hapana. Ule usafiri wa meli dhamana za Serikali ukalipo..? Hapana zilizopo ni za matajiri na hata tukizama SMZ husema, haina la kufanya. Tumezama, tunazama, na tutaendelea kuzama. Ndio maendeleo!!!!
Ya kale hayako tena, kweli. Lakini pia ya sasa hayapo na wala tusiyatarajie. Nchi hii kama ingekuwa gari, mmoja kati ya madereva hawa saba tuliojaaliwa na Chimwaga kutuongoza, lazima bila shaka alizitowa gia zote na kuibakishia gia ya kurudi nyuma tu (reverse gear). Na ndio hivi tunapelekwa msobe msobe. SMZ wakisimama majukwaani, huhubiri chuki, na uhasama na uongo mwingi kisha wakikutana katika vyombo vya habari husema wameleta maendeleo. Hivi ni kweli jamani. Sikupata nafasi ya kuchambuwa sana lakini mpaka hapa tu jiulize ndugu yangu.
‘TUNAKWENDA, TUNARUDI?’

No comments:

Post a Comment