Saturday, November 17, 2012

WAZANZIBARI WASEMA NCHI YAO KWANZA KIBUSHUTI SHEIN ASEMA CHAMA KWANZA NDIO KILICHO MUWEKA MADARAKANIMakamo Mwenyekiti wa Chama CHa Mapibnduzi Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein amesema sasa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaondoka na gia mpya katika kuimarisha na kuendeleza Chama katika ngazi zote ili kuona kinaleta mafanikio na kupata ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Amesema baada ya kumalizika uchaguzi wa ngazi za juu na kupata viongozi wapya kazi iliobaki ni kuimarisha chama kuanzia shina hadi taifa.
Amesema vikao vya chama ndivyo vinavyoimarisha na kuhuwisha chama kwani katika vikao hivyo ndimo mnamojadiliwa na kupangwa mambo yote ya kuendeleza chama.(SIO NCHI)
Dk Shein alitoa kauli hiyo leo jioni huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui alipokuwa akizungumza na wazee wa chama hicho mara baada ya kuwasili Zanzibar kutoka Dodoma kuhudhuria Mkutano Mkuu wa chama ambako alichaguliwa kuwa makamo wa Mwenyekiti wa CCM upande wa Zanzibar.
Amesema chama kitaendelea kuwaenzi wazee na kutumia busara zao katika kujenga uimara wa chama hicho na pia kupata hekima katika kukiendeleza na kukiimarisha ili kiendelee kuwa chama chenye misingi imara na kisichoyumba katika utekelezaji wa majukumu yake.(MAJUKUMU YA FITNA NA KUWABAGUWA NA KUWAGAWA WAZANZIBARI TUNARUDI KUULE TULIKO TOKA)
Hivyo aliwashukuru kwa jitihada zao za kukilinda na kukienzi chama hicho na pia kumchagua yeye kukiongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Ameahidi kufanya kazi bega kwa bega na wazee hao katika kukiendeleza chama cha mapinduzi.
Akizungumzia suala la utoaji maoni juu ya katiba mpya , Dk Ali Mohammed Shein amefahamisha kuwa nia ya kuwepo kura ya maoni ni kuimarisha muungano na sio kuvunja, hiyo ndio sera ya chama cha mapinduzi.(TUPENA BASI HIYO KURA YA MAONI)
Ameongeza kuwa katika mapendekezo hayo hapana pahali palipoandikwa au kusema kwamba Muungano uvunjwe. CCM ina sera yake ya kuimarisha muundo wa serikali mbili na sio vyenginevyo. Sera ya ccm iko wazi maelezo yake yapo wazi alisisitiza Dk Shein.(SEREKALI MBILI KUELEKE MOJA AU SIO KIBUSHUTI SHEIN..?)
Amesema watu wamekuwa wakitia chumvi juu ya suala hili hivyo si vyema kuwafuata kwani sisi tunasera yetu (CCM) na wao wanasera zao, sisi tuna chama chetu na wao wana vyao.(SERA YAO NI KUTAKA NCHI YAO CHAMA CHAO NI ZANZIBAR KWANZA WEWE SHEIN BADO NI KIBARAKA WA WATANGANYIKA UNAE TAKA SISI KUENDELEA KUWA WATUMWA NA KOLONI LA WATANGANYIKA.)
Alifahamsha kwamba chama ndio kiwe mbele na hakuna wa kuwababaisha wana ccm, kwani chama ndio kilichodhibiti nchi ibakie katika mikono ya wazalendo wa Tanzania si vyenginevyo.(NCHI NDIO IWE MBELE WEWE KIBUSHUTI)
Alitahadharisha kwamba wapo watu bado wanaitaka Zanzibar na kama wana ccm hatukuwa makini na tukafanya mchezo watu wataichukuwa nchi.(FITNA HIZOO SHEIN KIBUSHUTI ANAZILETA ILI AWAGAWE WAZANZIBARI)
Kuhusu amani na utulivu wanchi, Makamo mwenyekiti huyo alisema bado wako watu wanaichezea amani iliopo jambo ambalo ni hatari sana.Serikali haitavumilia kuona amani inachezewa.(ILI YAKUWAINGELIA WATU MAJUMBANI NA MISIKITINI MUKINAJISI KWA MAMBWA NA MABOMU NDIO AMANI SIO..?)
Alivipongeza vikosi vya ulinzi na usalama kwa kurejesha utulivu na kuendelea kulinda maisha namaliza raia.(YA LAZIMA UWAPONGEZA WANA DHULMA KAMA WEWE MWENYEWE ULIVYO THULUMU KURA UKAJIWEKA KTK URAISI HUKUSHINDA ILA DHULMA DHULMA NDIO LAZIMA UWAPONGEZE)
Amerejea kauli yake kwamba serikali haiwezi kuvumilia tena vitendo vinavyofanywa na Muwamsho na kusema kwamba serikali itaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa kikundi chochote ambacho kitaashiria uvunjifu wa amani hapa nchini.na kamwe serikali haitovumilia kuchezewa.Haturudi nyuma katika kulinda amani ya zanzibar ili sifa nzuri ya visiwa hivi isiondolewe.(IMEONDOKA ZAMNI SANA NA WEWE NDIO UNACHAFUWA ZAIDI KIBUSHUTI WEWE)
Nao wazee wa CCM wa Mikoa mitatu ya Unguja walitoa pongezi zao kwa Mkutano Mkuu wa Taifa na Ushindi wa asilimia mia moja (100%)kwa Dk shein na kusema kwamba hivi sasa chama kimeingia katika muelekeo wa uhakika zaidi wa kukipatia ushindi wa kishindo chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao. Kwani kutokana na sababu za kiitikadi kilichojitokeza ni kuzorota kwa utendaji katika chama hasa ngazi za chini katika kipindi kilichopita cha uongozi.
Wamesema sikweli maneno yaliosemwa na kiongozi mmoja wa kisiasa kamba doria zinazofanywa na askari kwa lengo la kudumisha amani vinafanya doria katika maeneo yenye wafuasi wa chama hicho na eti kwamba kinawabughudhi.(UKWELI NIUPI BASI SIMUSEME..?)
Waliwataka viongozi wa juu kukumbushana umuhimu wa kujikinga na fitna na kuziepuka taarifa za kubuniwa.

No comments:

Post a Comment