Monday, December 17, 2012

BILALI ATAMUKIWA NA DUNIA NA KUANZA KUJIDAI KUWAPA USHAURI WAISLAMU ILI AENDELE KULA RAHA ZA DUNIA. BILALI KWANI WEWE MUISLAMU....???

NI

Makamu  wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal,  amewataka Waislamu nchini kuweka juhudi zaidi  katika elimu ya dini pamoja na ya dunia ili kuepuka matatizo mengi yanayosababishwa na ukosefu wa elimu hiyo.
Makamu wa Rais aliyasema hayo katika sherehe za mwaka mpya wa Kiislamu zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Alisema matatizo mengi yanayolenga Uislami yanatokana na ukosefu wa elimu ya dini hiyo,  pamoja na elimu  ya dunia.
“Jambo la kushangaza na la kutia huzuni ni Waislamu kukosa elimu,  aya  ya mwanzo alizoshushiwa  Mtume Muhammad,  ni kusoma,  hakuambiwa kusali  au kufunga,”  alisema na kuongeza:
“Uislamu na Waislamu hatunabudi kufuata kanuni za msingi ili tuusaidie Uislamu wenyewe na nchi yetu,  njia ya msingi ya kufanya hivyo ni elimu.
Aidha Dk. Bilal, aliwataka Waislam kufuata kanuni za msingi za dini yao, ili kuepuka machafuko yanayoweza kujitokeza.
“Utaratibu huu wa kiislam kuwa na kanuni za msingi ni  muhimu sana, na tutakapoacha kuufuata ndipo tutakapoanza kuuana na kuua kwa kisingizio cha dini. Kanuni za msingi za kiismlam ndizo zinazolinda dini ya kislam, Waislamu wenyewe pamoja na dunia nzima,” alisema.
Makamu wa Rais alisema: “Nimeeleza hayo kwa sababu  mimi na wenzangu serikalini tumeanza kuingia wasiwasi kwani hivi karibuni kumetokea vurugu ambazo hatimaye zimeashiria kuvunjika kwa amani ya nchi, mali zimepotea na wengine wamepoteza maisha kwa kisingizio cha dini.”
Pia alisema kila Muislamu lazima afundishwe namna ya kuwa Muislamu wa kweli na anayefahamu Qur-an,  na kufundishwa namna ya kuwa na amani na upendo  utakaowakomboa watu wote.

No comments:

Post a Comment