Thursday, December 6, 2012

MAAZIMIO NA CHUKII,FITNA,UBAGUZI WA CCM OFISI YA KISIWANDUWIMAAZIMIO NA CHUKI NA MAFUNZO YA SIKU MBILI YA MAKATIBU WENEZI WA MIKOA, WILAYA NA MAJIMBO YOTE YA UNGUJA TAREHE 04/05/2012 KATIKA UKUMBI WA AFISI KUU YA CCM KISIWANDUI.
1)MAPINDUZI
Tunalaani mbinu na njama zote zinazofanywa kwa makusudi na wapotoshaji ya kupotosha ukweli dhidi ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na manufaa yake kwa waafrika weusi na ndio wenye africa yaliyotuletea uhuru wa kweli wa kujiamulia mambo yetu na kutaka kuturejeshea utumwa, ubwana na utwana na kuturudishia waarabu kuja kututawala.
(2)HISTORIA
Somo la historia kuendelea kufundishwa ili vijana wajue ukweli wa historia ya ukombozi wa nchi yao ambayo Wazee wetu walipinduwa kwa majimbe na mashoka na mapaga ndio tukaipata pia walipitia katika misitu na nyika kutafuta Uhuru wa Mzanzibari hii munayo iyona leo imeja maendeleo.
(3)AHADI
Makatibu Wenezi tunaahidi kuwa kuanzia hitimisho la Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma wa 14/11/2012 na kupata safu mpya ya uongkozi, sasa kila Katibu Mwenezi kwa nafasi yake alipo atatekeleza , kuhamasisha Siasa na Itikadi sahihi ya CCM kwa maana ya CCM KWANZA mtu au watu baadae.
(4)PONGEZI
Tunapongeza kwa kuchaguliwa ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndugu Ali Mohammed Shein kuwa Makamo Mwenyekiti kwa upande wa Zanzibar na Ndugu Philip Jafet Mangula kuwa Makamo Mwenyekiti kwa upande wa Tanzania Bara kwa ushindi wa kishindo wakitaka wasitake ushindi lazima hata kwa mtutu tutachukuwa tu.
Pia tunaunga mkono hotuba za Mwenyekiti wa CCM taifa ndugu Jakaya Mrisho Kikwete alizotoa katika Mkutano Mkuu mjini Dodoma na pia tunaunga mkono hotuba ya Makamo Mwenye kiti wa CCM Zanzibar Ndugu Ali Mohammed Shein aliyoitoa katika viwanja vya Demokrasia Kibandamaiti tarehe 17/11/2012 na kukiomba chama kusimamia ipasavyo utekelezaji wa hotuba hizo.
(5)HATUA DHIDI YA VIONGOZI WAPOTOFU.
Tuna tamka na kutaka viongozi waliojidhihirisha wazi kukataa na kupinga masharti ya uanachama katika ibara ya 3(a-f) ya ilani ya itikadi ya CCM ya Muundo wa Serikali mbili na kuele moja katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wafukuzwe uwanachama mara moja.
(6)TAMKO
Baadhi ya wazee waasisi wa TANU na ASP kuacha kupotosha ukweli wa historia ya nchi na chama kwa ujumla ili kuwezesha vijana kufaidika na matunda ya Muungano wa Tanzania na Matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar kama walivyofaidi katika enzi zao matunda hayo.
(7)MIKAKATI
Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wanaotokana na CCM kuwashirikisha ipasavyo makatibu wa itikadi , siasa na uenezi wa ngazi husika katika kutekeleza shughuli na MIkutano mbalimbali ya kimaendeleo ili kuwawezesha kufahamu zaidi utekelezaji wa majukumu yao kwa manufaa ya CCM tu wengine warudi nchi walizotokea.
(8)SISITIZO
Tunasisitiza na kuhimiza kuwa azimio la mkutano mkuu wa CCM Dodoma wa kuiwezesha na kuiimarisha idara ya itikadi , siasa na uenezi ngazi ya Mikoa, Wilaya na Majimbo kwa kupatiwa Nyenzo na Taaluma zaidi katika kufanikisha Majukumu yao ipasavyo
(9)KUTEKELEZA AHADI
Serikali kupitia Watendaji wake wanaotokana na CCM kuharakisha kutekeleza ahadi zake kwa Wananchi hususan kuharakisha kumaliza tatizo la mgao wa umeme, Maji safi na salama, Huduma za afya na Elimu pamoja na kuimarisha sekta ya Kilimoili kuwawezesha wenezi kutangaza mafanikio hayo kwa Umma na kuwa kivutio cha kupata wanachama wapya.
(10)TAARIFA
Kwa kuwa rais wa Zanzibar ni rais Mtendaji ni muhimu kushuka kwa wananchi kujua kwa undani taarifa anazopewa na watendaji wake ili kuwezesha kuwa na taarifa sahihi za utekelezaji wa ilan ya CCM
(11)Hii nchi ni ya CCM na itaendelea kuwa ya CCM na yoyote atakae jaribu kuingowa au kujaribu kuiangusha CCM ashughulikiwe haraka ipasavyo asije akaharibu matunda tuliyo pewa na babu na baba zetu ya mapinduzi matukufu hapa zanzibar.

1 comment: