Tuesday, December 25, 2012

UAMSHO KWALI INAMUOGOPA M/MUNGU AU INAOGOPA SMZ NA MACHOGO...?



Amiri wa muda wa jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu Zanzibar  amekanusha madai yaliodaiwa kwamba waislamu wameiomba serikali iwatoe viongozi wakuu wa jumuiya ya uamsho kabla ya sikukuu ya krismas ambao wapo rumande kwa muda wa takriban miezi  miwili kwa sasa.
Hivyo amewaomba waislamu na wananchi kuwa wastahmilivu katika kipindi hiki ambacho maoni ya ukusanyaji wa maoni yamekamilika kwa upande wa Zanzibar hivyo amewaomba wazanzibar kusubiri utekelezwaji wa matakwa yao.
 Akizungumzia vipeperushi vilivyosambazwa hivi  karibuni vya kutoa onyo ikiwa maamiri hawaataachiwa huru ikifika siku ya krismas na mwaka mpya watachukua hatua. Hivyo Amesema vipeperushi hivyo havikutolewa na viongozi wa jumuiya hiyo na amewataka waislamu kuwa makini dhidi ya maadui wasioitakia mema Zanzibar.
 Amesema vipeperushi hivyo vilivyodaiwa vimetoka masjidi jibril mkunazini kwamba havihusiani na msikiti huo wala taasisi yeyote ya kiislamu Zanzibar,
 Aidha amebainisha ya kwamba vipeperushi hivyo vina lengo la kuwashawishi wananchi kuchochea vurugu ambazo hazina faida kwa maendeleo ya Zanzibar, hivyo Amewafahamisha wananchi na waislamu kwamba suala la kuingilia mahakama kwa sasa ni kosa kisheria  hivyo amewataka wazanzibar kutoshabikia masuala hayo wakati huu ambapo  kuna mambo muhimu yanayolikabili taifa.
Na baadhi ya waislamu ambao huswali msikiti huo wamewaomba wale wote amabo wanauchezea uislamu waache tabia hizo kwani misikiti ni nyumba tukufu kwa ajili ya ibada na sio kwa ajili ya kuwagawa wananchi..

No comments:

Post a Comment