Friday, December 28, 2012

WAZANZIBARI TUMEPINDULIWA 1964 NA SASA TUNAPINDULIWA KIKATIBA


KAMA KWELI WAZANZIBARI TUNAITAKA ZANZIBAR YETU YENYE MAMLAKA KAMILI BASI KWANZA TUMUONDOWE DIKTETA SMZ KAMA ALIVYO ONDOLEWA GADDAFI,BEN ALI,HUSSENI MUBAROUK,SALEH NA WENGINEO LA SIVYO ITAKUWA TUNACHEZA MDUWARA TU.


Tarehe 19 December ilikuwa siku ya mwisho kwa Tume ya Kukusanya maoni ya upatikanaji wa katiba mpya. Tume ilifanikiwa kutemebelea nchi nzima na kukutana na wananchi walioweza kutoa dukuduku lao na vipi katiba mpya itapatikana.
Kwa mujibu wa hadidu rejea za tume hityo zilizotolewa ni kwamba baada ya kumaliza kazi ya ukusanyaji maoni kwa wananchi kutakuwa na mabaraza ya katiba.
Hivi sasa hapa Zanzibar kuna taarifa za kuaminika kwamba baadhi ya wizara zimetowa toleo maalim (circular) la kuwataka wafanyakazi wa serikali watowe maoni yao ya kwa njia za maandishi. 
Toleo limepelekwa idara mabalimbali za serikali kuwataka wafanyakazi waandike maaoni yao juu ya mchakato wa katiba. Hili ni lakushangaza kwamba waliotoa toleo hili sio Tume ya Katiba wala halimo kwenye hadidu rejea za Tume hiyo. Hivyo kutia wasiwasi muelekeo wa upatikanaji wa katiba mpya Tanzania kugubikwa na magube ya kimapinduzi.
Zipo dalili za dhahiri za kukengeukwa na kudharauliwa maoni ya wananchi kama vile walivyotumia juhudi zao, wakavunja shughuli zao, wakatumia muda wao, na mwisho kile walichosema kuanza kukidharau. 
kauli ya Prof baregu ni ushahidi tosha na mwanzo wa kuthibisha hili. Dharau yake kwa maoni ya wananchi hasa Wazanzibar, sio suala la kuvumiliwa. Ipo haja kwa nguvu zote tuisute tume pale itakapozidisha dharau zake kutothamini maoni ya wananchi.

No comments:

Post a Comment