Tuesday, December 25, 2012

ZIJUWE AINA NNE ZA WATU HAPA DUNIANI


SHAMHUNA YUKO KATIKA AINA GANI KATIKA HIZI NNE WACHA KOMENTI YAKO

Kuna yule ajuae, na ajua yuajua
Tatizo mpelekee, lolote atatatua                                 
Yuajijua mwenyewe, kwamba yeye yuajua
Kuwa karibu na yeye, elimuye kuchukua
Mwengine ni ajuae, na hajui yuajua
Elimu i tele naye, hana asichokijua
Ela aonavyo yeye, yu juha wa kurembewa
Huyu na ashituliwe, hadhi yake kuijua
Na kuna asiyejua, na ajijua hajui
Mambongwa huyakimbia, watuni yeye hakai
Adhara aichelea, kuja tolewa nishai
Huyu si wa kuzomewa, ni wa kufunzwa kwa rai


Wa nne ni asojua, na hajijui hajui
’kiitwa kuhutubia, himahima hakatai
Maringo kujisifia, yukajifanya nabii
Huyu ni kushushuliwa, yukaambiwa hajui

Wa kwanza ni ajue, akajua yuajua
Wa pili ni ajuae, na asijue ajua
Wa tatu ni asojua, akajijua hajui
Wa nne ni asojua, yusijijue hajui

No comments:

Post a Comment